Mdau
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,789
- 470
Mnamo tarehe 27 Januari 2001, makumi ya wananchi wa Pemba waliuawa na vyombo vya usalama katika maandamano na mamia kadhaa kukimbilia uhamishoni nchini Kenya..kuna mambo mengi sana yamepatwa kusemwa, lakini jambo la msingi kabisa; ambalo ni kwa watuhumiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, halijapata kutimizwa..kubwa la kujifunza ni kwamba viongozi wetu wa kisiasa ni njaa kali sana, nathubutu kusema CUF kinaongozwa na viongozi waliokosa dira, wenye tamaa ya madaraka na waliochoka kimawazo..ingekua ni chama makini, naamini wangepiga sana kelele ili waliopanga na kutekeleza mauaji yale wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria..thamani ya maisha ya binadamu haipimwi kwa unafiki wa MUAFAKA, ambao mwisho wa siku hautaleta tija wala kubadilisha hali ya maisha ya mzanzibari wa kawaida..wito wangu ni kwamba, Zanzibar si mali ya CUF au CCM pekee, ni mali ya Wazanzibari wenyewe, hivyo basi, kama ambavyo tumeshuhudia jinsi viongozi na maafisa mbalimbali duniani kote wanavyowajibishwa kwa uvunjifu wa haki za binadamu katika nchi zao husika, ni wakati muafaka sasa kwa wenye mapenzi mema na machungu ya kweli kwa Zanzibar, kusimama na kupigania utendekaji wa haki kwa waliotimiza na walioathirika na mauaji ya Pemba mwaka 2001..iwe ni kwa kuanzisha uchunguzi wa ndani au wa nje, mwisho wa siku ni kwamba haki lazima itendeke!!!
Binafsi naamini wafuatao wanalazimika kutoa maelezo kuhusu kwa nini wasiwe ni washukiwa katika kupanga mauaji hayo:
1. Benjamin Mkapa
2. Omar Mapuri
3. Omar Mahita
4. Apson Cornel
5. listi iendelee tafadhali........
Binafsi naamini wafuatao wanalazimika kutoa maelezo kuhusu kwa nini wasiwe ni washukiwa katika kupanga mauaji hayo:
1. Benjamin Mkapa
2. Omar Mapuri
3. Omar Mahita
4. Apson Cornel
5. listi iendelee tafadhali........