Mauaji ya Pemba 2001: Majina ya Watuhumiwa.

Hoja ni nzito, waliotajwa kama wauwaji ni walikuwa au wapo katika madaraka, na wenyewe wanasema "Jusice is the interest of teh people in power" kwa maana hiyo kilichofanyika Pemba ni Justice hivyo hakuna wa kushatakiwa kwa kuwa kwenye kutenda haki hashtakiwi!, Watanzania bado hawajaandaliwa kwa hilo.

Kwani justs ni sawa na haki?
Huko Rep. of S. Africa, Mandela kuwekwa ndani haikuwa justs? Maana katiba yao iliruhusu hivyo. Je ilikuwa haki?
 
hawa nao lazima waongezwe:

Maalim seif sharrif hamad
prof. Lipumba maana wao waliwatuma wananchi waaandamane lakini wao wakasepa. No hata hawawakumbuki marehemu!!!
bila hawa kuwa na imani na sisi tungeuliwa zaidi sababu watu walikua tayari kwa lolote na kulipa kisasi
sasa unapowatia kwenye list nawe pia utakua ndie
 
Mbona mnataka kumsahau Hamadi Rashidi? Si alihongwa ubunge na Mkapa miezi michache tu baada ya mauaji ili asiwe anakumbusha kumbusha?
 
Seif Hamad kishapewa Benz unafikiri atafikiria hayo??? Hamna kazi yoyote anayofanya zaidi ya kuzindua majengo kwa niaba ya Shein....SAWASAWA.
 
Mnamo tarehe 27 Januari 2001, makumi ya wananchi wa Pemba waliuawa na vyombo vya usalama katika maandamano na mamia kadhaa kukimbilia uhamishoni nchini Kenya..kuna mambo mengi sana yamepatwa kusemwa, lakini jambo la msingi kabisa; ambalo ni kwa watuhumiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, halijapata kutimizwa..kubwa la kujifunza ni kwamba viongozi wetu wa kisiasa ni njaa kali sana, nathubutu kusema CUF kinaongozwa na viongozi waliokosa dira, wenye tamaa ya madaraka na waliochoka kimawazo..ingekua ni chama makini, naamini wangepiga sana kelele ili waliopanga na kutekeleza mauaji yale wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria..thamani ya maisha ya binadamu haipimwi kwa unafiki wa MUAFAKA, ambao mwisho wa siku hautaleta tija wala kubadilisha hali ya maisha ya mzanzibari wa kawaida..wito wangu ni kwamba, Zanzibar si mali ya CUF au CCM pekee, ni mali ya Wazanzibari wenyewe, hivyo basi, kama ambavyo tumeshuhudia jinsi viongozi na maafisa mbalimbali duniani kote wanavyowajibishwa kwa uvunjifu wa haki za binadamu katika nchi zao husika, ni wakati muafaka sasa kwa wenye mapenzi mema na machungu ya kweli kwa Zanzibar, kusimama na kupigania utendekaji wa haki kwa waliotimiza na walioathirika na mauaji ya Pemba mwaka 2001..iwe ni kwa kuanzisha uchunguzi wa ndani au wa nje, mwisho wa siku ni kwamba haki lazima itendeke!!!

Binafsi naamini wafuatao wanalazimika kutoa maelezo kuhusu kwa nini wasiwe ni washukiwa katika kupanga mauaji hayo:

1. Benjamin Mkapa
2. Omar Mapuri
3. Omar Mahita
4. Apson Cornel
5. listi iendelee tafadhali........

Na wewe usijisahau kwenye hii orodha.

Wapemba waliuawa kwa sababu wali-riot na mbaya zaidi walianza wao kwa kumchinja askari polisi. Waliofanya hivyo walikuwa ni kundi kubwa la wananchi wakiwa wameshika silaha za jadi huku wakiimba nyimbo za kuhamasishana. Ndiyo maana rais wa wakati huo bw. Mkapa aliwauliza watanzania kuwa fikiria ungekuwa ni wewe upo lindoni na polisi mwenzio mara ghafla linatokea kundi la wananchi wenye hasila na kumvamia mwenzio. Kisha wanamchinja na kuachanisha kichwa na kiwiliwili mbele ya macho yako. Baada ya kumaliza wanakufuata wewe huku wakiimba 'tunataka silaha zetu', ungefanya nini na bunduki yako iliyojaa risasi. Definitely, ni ku-fire tu, hakuna cha msalia mtume. Ndivyo walivyofanya askari kule pemba.
 
Hawa nao lazima waongezwe:

Maalim Seif Sharrif Hamad
Prof. Lipumba maana wao waliwatuma wananchi waaandamane lakini wao wakasepa. No hata hawawakumbuki marehemu!!!
alfred kizuguto aliekua rpc wa zenj na kamishna wa police zenj,na ma rpc wa kaskazinipemba nakusini pemba wawakati huo,
 
Kesi ilishakwisha kwani CUF wanaongoza nchi sambamba na CCM. Kwa nini mnataka kuwachonganisha tena?
 
Hawa nao lazima waongezwe:

Maalim Seif Sharrif Hamad
Prof. Lipumba maana wao waliwatuma wananchi waaandamane lakini wao wakasepa. No hata hawawakumbuki marehemu!!!

Nilikuwa sijacheka siku nzima leo ila hii thead imenifanya uso u relax. Kwa bahati mbaya watu hawawajui wana siasa walivyo. Mtu anaanzisha chokochoko halafu anatanguliza familia yake Ulaya na yeye huyooo anawafuata. Anaongoza mapambano kutoka kwenye Five star hotels za ulaya. Hali ndivyo ilivyo karibu kila sehemu kwenye machafuko. Inasemekana watu wachache ndio walifanya tofauti ikiwemo Jonas Savimbi wa Angola. Yeye aliongoza tokea msituni na miaka ya mwanzoni aliwapa wafuasi wake vyeo kutokana na competence na siyo nepotism au kujuana. Unita ilikuwa na nguvu sana kipindi hicho. Alichokosea ni kuwa puppet wa CIA ambao baade walimgeuka.
Vinginevyo siasa ni kusizikiliza halafu kutumia ubongo wako kuzichuja. Ni rahisi sana hata kwa mwelevu kutumiwa na wanasiasa kwa malengo yao.Yakitimia ndio bye bye. Unasahaulika.
 
Hawa wadaku wa Chadema sio ndio wanajifanya watetezi sana wa wanyonge? Mbonba hili la kuuliwa waPemba wamelikalia kimya au kwa sabau tu ni waIslam?
 
..Raisi wa Zanzibar, na Waziri Kiongozi, wakati mauaji yanatokea, ndiyo chanzo na wahusika wakuu.

..wengine ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Zanzibar.

..viongozi wa CCM na CUF ambao wamekuwa wakichochea hali ya kubaguana na mifarakano ktk jamii ya wa-Zanzibari.
 
Safi sana aliyeleta Hoja hii! inafurahisha sana ila inasikitisha pia!
jamaa wengi walipoteza maisha watuhumiwa lazima watakuwepo kwenye suala hilo Hebu tulifanyie kazi kuhakikisha walinyang'anywa uhai wao whaki inatendeka kwa walio sababisha kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
Kwani justs ni sawa na haki?
Huko Rep. of S. Africa, Mandela kuwekwa ndani haikuwa justs? Maana katiba yao iliruhusu hivyo. Je ilikuwa haki?
just and unjust are relative terms, depending on who is defining on which environmnet. Human being cannot know the truth as it is but as it appears to him!
 
Nikisoma michango ya wote hapo juu unaona live kuwa wengi wamekwepa kumjadili mkapa, kwa hiyo hata hiyo ccm inayozungumziwa si ccm halisi bali ni JK na uislam wake, mkapa ameua watu zanzibar na wala si kuanzia tar 27.1 2001 kama ilivyoandikwa hapo juu bali walianza kuua tar 26 asubuhi na mapema imamu na muumin mwengine wakitoka mskitini kuswali swala ya asubuhi
Pia aliua waumini wakiislam pale Mwembechai na kuwaita ni kikundi cha wahuni.
si vyombo vya habari wala nyinyi wachangiaji mlioinua midomo yenu kuuelezea uovu huu, lakini leo tena kwa masalahi yenu mnajifanya eti mnamachungu sana na wale wazanzibar. Inaudhi sana.kwa nini wachangiaji wengi wamekwepa kumjadili mkapa kama mhusika mkuu wa kadhia hizi? watu wamerukia kuwataja akina Lipumba ambao wakati mwengine wameishia mpaka kuvunjwa mikono na kuwekwa ndani wakidai katiba mpya na akani Seif wakiswekwa ndani bila sababu za msingi na huku vyombo vya habari vikishabikia?
Mkapa hakujadiliwa kwa sababu ipi? ukristo wake? If that is the case then let me call this is CHADEMA FORUM THE HOME OF CHRISTIAN THINKER.
Msipobadilika nawahakikishia hapa patakuwa hapatoshi kwani sasa hivi kila mmoja anajua kuwa hiki ni kijiko na hii na beleshi na anaiita hivyo bila ya kumumunya maneno na matendo.. I'm sure time will tell.
 
Back
Top Bottom