Mauaji ya Pemba 2001: Majina ya Watuhumiwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Pemba 2001: Majina ya Watuhumiwa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdau, Dec 16, 2010.

 1. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Mnamo tarehe 27 Januari 2001, makumi ya wananchi wa Pemba waliuawa na vyombo vya usalama katika maandamano na mamia kadhaa kukimbilia uhamishoni nchini Kenya..kuna mambo mengi sana yamepatwa kusemwa, lakini jambo la msingi kabisa; ambalo ni kwa watuhumiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, halijapata kutimizwa..kubwa la kujifunza ni kwamba viongozi wetu wa kisiasa ni njaa kali sana, nathubutu kusema CUF kinaongozwa na viongozi waliokosa dira, wenye tamaa ya madaraka na waliochoka kimawazo..ingekua ni chama makini, naamini wangepiga sana kelele ili waliopanga na kutekeleza mauaji yale wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria..thamani ya maisha ya binadamu haipimwi kwa unafiki wa MUAFAKA, ambao mwisho wa siku hautaleta tija wala kubadilisha hali ya maisha ya mzanzibari wa kawaida..wito wangu ni kwamba, Zanzibar si mali ya CUF au CCM pekee, ni mali ya Wazanzibari wenyewe, hivyo basi, kama ambavyo tumeshuhudia jinsi viongozi na maafisa mbalimbali duniani kote wanavyowajibishwa kwa uvunjifu wa haki za binadamu katika nchi zao husika, ni wakati muafaka sasa kwa wenye mapenzi mema na machungu ya kweli kwa Zanzibar, kusimama na kupigania utendekaji wa haki kwa waliotimiza na walioathirika na mauaji ya Pemba mwaka 2001..iwe ni kwa kuanzisha uchunguzi wa ndani au wa nje, mwisho wa siku ni kwamba haki lazima itendeke!!!

  Binafsi naamini wafuatao wanalazimika kutoa maelezo kuhusu kwa nini wasiwe ni washukiwa katika kupanga mauaji hayo:

  1. Benjamin Mkapa
  2. Omar Mapuri
  3. Omar Mahita
  4. Apson Cornel
  5. listi iendelee tafadhali........
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mmh,
  Sasa inabidi wafikishwe ICC ya arusha ama the Hague,
  Je! Nao waundiwe tume huru iwachunguze?
  Maana kuna wengine hasa aliyekuwa IGP akiitwa 'laana-khum' na mwenyekiti wa CUF katika moja ya kampeni zake hapa DSM.
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  haki itendeke
   
 4. m

  mchakachuaji1 Senior Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Arusha sio ICC ni ICTR yaani International Criminal Tribunal for Rwanda.
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Omari Ally Juma (Marehemu)
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa sijui, kumbe ile ya Arusha ni maalumu kwa kesi ya Rwanda tu!!
   
 7. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Aman Abeid Karume.
   
 8. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waroho wa madaraka wanachekelea na suti kama vile waliokufa cio binadamu TUWAPIGANIE NDG ZETU
   
 9. B

  Beyond Thinking Member

  #9
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja ni nzito, waliotajwa kama wauwaji ni walikuwa au wapo katika madaraka, na wenyewe wanasema "Jusice is the interest of teh people in power" kwa maana hiyo kilichofanyika Pemba ni Justice hivyo hakuna wa kushatakiwa kwa kuwa kwenye kutenda haki hashtakiwi!, Watanzania bado hawajaandaliwa kwa hilo.
   
 10. papason

  papason JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Maalim na Lipumba....................Nukumbuka siku nne kabla ya mandanamo maalim alikimbilia Europe na Lipumba alijificha pale Buguruni wakawa wana organize maandamano ya pemba thru remote control wakati wao ndio walitakiwa kuwa kwenye first line ya maandamano, tena through mufaka wao feki CCMm iliwaambia 'kuwasahau mashujaa wao' kama moja ya kipengele cha cha muafaka na wao wakakubali hivyo kwa uoga wao unawafanya kuwa watuhumiwa #2
   
 11. c

  chidide Member

  #11
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa nao lazima waongezwe:

  Maalim Seif Sharrif Hamad
  Prof. Lipumba maana wao waliwatuma wananchi waaandamane lakini wao wakasepa. No hata hawawakumbuki marehemu!!!
   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Juma Duni Hajji nadhani yeye alikuwa ni chambo kwa hao wenye red hapo juu, kweli maalim alikuwa nje kwa kile kisemwacho 'kuwaeleza wahisani wazuie misaada kwa SMZ'
   
 13. papason

  papason JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280


  Walai sheria lazima ichukue mkondo wake ikiwashilikisha maalim seif na Prof Lipumba ili uwe mfano wa wasiasa 'makanjanja', wanao wadanganja wanaharakati waandamane na wao wakula kona,

  Tena binafsi nawashangaa sanaa vijana wa CUF kulifumbia macho jambo hili?
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  msisahau kumuingiza Prof Lipumba na Maalim Seif
   
 15. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Miongoni mwa victim sio wanachama wa CUF pekee,, kuna na yule askari aliekatwa kichwa,, waliohusika pia wafikishwe kwenye sheria,,
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wamfukue tu hata mifupa yake isomewe mashtaka
   
 17. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  seif sharif@lipumba wavune walicho kipanda hapo hakutakuwa na muafaka bali miafaka yote iwe ushahidi dhidi yao INSHAALAH!
   
 18. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  kuna hoja ambazo huwa sichangii kabisaaaaaaaaaaa

  hata kwa bunduki
   
 19. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Kigezo kimojawapo cha kufikia muafaka kingekuwa kushitakiwa kwa walioamuru mauaji ya 2001. Au hata kuwataja hadharani ili waaibike kwa jamii (name & shame). Viongozi wa CUf wakawa kimya...

  List iendelee;
  5. Amani Karume.
  6. Maalim Seif Shariff Hamad.
  7. Prof Lipumba.


  Ocampo njoo! Mahakama za Bongo zitachakachua kama kawa...
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Nimesema sichangii
   
Loading...