Mauaji ya Nyamongo na majibu rahisi ya Kagasheki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Nyamongo na majibu rahisi ya Kagasheki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nanu, May 20, 2011.

 1. N

  Nanu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nimesikia kwenye vyombo vya habari majibu rahisi aliyoyatoa Mh. Kagasheki kuhusu vurugu na mauaji ya raia huko Nyamongo tarime kuwa wananchi wameandamana kwa kushawishiwa. Mimi nadiriki kusema haya ni majibu rahisi ya kisiasa ambazo hazilengi kumaliza wala kujua hasa chanzo cha vurugu hizo na hivyo vurugu kama hizi tutaendelea kushuhudia ama huko Nyamongo au sehemu nyingine za nchi yetu.

  Naomba ni mwulize Kagasheki na IGP Mwema, kama watu wameshawishiwa kufanya vurugu ziko wapi vyanzo vyenu vya inteligensia? Kwanini hamjachukua jukumu kuzuia machafuko hayo?

  Kwa kusema watu wameshawishia na hasa ukilenga siasa nadhani ni majibu ya haraka sana na hayajafanyiwa utafiti wa kina na inalenga kupunguza nguvu ya jeshi la polisi na vyombo vingine husika zisifanye uchunguzi wa kina na kuja na majibu ya chanzo na jinsi ya kuzuia migogoro hii yasitokee tena au mara kwa mara katika nchi yetu. Tunahitaji uchunguzi ufanyike na taarifa itolewe kwa umma wa Watanzania kuhusu chanzo cha vurugu hizo na tunafanya nini kuzuia yasitokee tena.

  Tuepuke kutibu dalili za ugonjwa bali tutibu chanzo cha ugonjwa.

  Mtoto akiwa anatapika au kuharisha ukimpa dawa ya kuzuia kutapika au kuharisha ataacha kutapika au kuharisha kwa muda tu lakini baada ya nguvu ya dawa kupungua au kuisha ataanza tena kutapika au kuharisha kwa sababu hujachunguza kwanini anatapika au kuharisha ili uzuie chanzo cha kutapika au kuharisha. Umetibu dalili tu na mtoto hatapona.

  Ni vizuri basi kuzuia tatizo kwenye chanzo halisi na chanzo halisi utaijua tu kwa uchunguzi wa kina usiotengeneza majibu kabla ya kuchunguza.
   
 2. p

  potash Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naibu waziri wa mambo ya ndani ndugu Juma Kagasheki amekuwa akisema kwenye vyombo vya habari kuwa kuna mmbunge wa chama fulani tena kutoka nje ya mkoa wa Mara ambaye yuko mkoani Mara na ndiye chanzo cha vurugu hizo kwani amekuwa akichochea raia kukataa kuwazika ndugu zao.

  Yeye akiwa kama kiongozi kwa nini asimtaje waziwazi kuwa ni nani na anatoka chama gani na ikibidi akamatwe na kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi? Lakini kwa staili hii ya kagasheki naona hayo tunayoyasikia na kuyaona kwenye vyombo vya habari yana ukweli na yawezekana serikali hii ina ajenda ya siri na hawa wawekezaji. Mpaka hivi sasa si Nahodha wala Kagasheki ambao wanadhamana ya mambo ya ndani ya nchi hii amedhuru Tarime na kujionea hali halisi ya mambo.

  Ni shujaa waziri kivuli wa mambo ya ndani Godbless Lema tu ndiye kafika huko na kufika kwake kuona hali halisi ya mambo eti anachochea vurugu. Mmekaa Ofisini mnazungumza bila kudhuru eneo la tukio.Jambo hili ni aibu kubwa raia sita kuuawa siyo jambo dogo?

  Serikali ya CCM angalieni yaha manake kuna ukurutu unaozidi gamba.
   
 3. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  We waache tu ccm. Wanazidi kujiharibia kwa kutowajali walalahoi. Hizi kauli wanazotoa haziwasaidii kujivua magamba
   
 4. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I'm confused!suala la wananchi wa nyamongo kukataa kuzika miili ya watu waliouawa kwa risasi limejitokeza kabla ya mhesh Lema kwenda nyamongo.Inakuaje leo mtu yuko dar anakula bata anasema eti Lema ndiye anasababisha wananchi kugoma kuzika?Lema ameenda nyamongo jana,na wananch wamegoma kuzika tika jumanne wiki hii,wakati huo lema hakuwapo mkoani mara.Imefika wakati Serikali iwajibike kwa uzembe wa watumishi wake.Haiingii akilini kwa mtu mwenye dhamana kama kagasheshi akakurupuka kutoa majibu mepesi kwa suala zito kama hili.Hivi kuna siri gani kati ya serikali na wawekezaji?Mbona imefika wakati serikali haiwajali watu wake kwa sababu ya wawekezaji?Watanzania tuamke tuwaadhibu hawa wapuuzi waliolea mvinyo wa wawekezaji......Tunaweza tukiamua.
   
 5. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,089
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  kama kawaiday y wanamagamba na magamba yao. kuchukulia kirahisi mambo ya kimsingi kabisa...
   
 6. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mwaka jana kulipotokea malalamiko kuwa wananchi wanaathiriwa na sumu kutoka mgodini north mara kgasheki huyuhyu alienda huko na akatuambiwa alidanganywa na uongozi wa mgodi - mara mambo yakageuka tukaambiwa yeye ndiyo alidanyanganya.

  Ukafuata ukimya hadi ilipoundwa tume ya bunge kuchunguza ambayo mpaka leo hatujaambiwa ukweli ni upi - kwa maana nyingine walifunika NA
  haya ndiyo matokeo ya kufunika mambo!
   
Loading...