Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika!

Hivi Ben Disraeli alikuja waziri mkuu wa Uingereza 1967 kweli?

itakuwa miaka ya1800 na sio 1900. Huyu alikuwa anajulikana kama Benjamin Disrael earl of Beaconsfield. Aliwatesa sana warusi na hatimae aliuteka mfereji wa suez na kuilazimisha Egypt kuwa ubia. (ref an illustrated history of Modern Europe 1789 - 1984 by Denis Richards - 7th edition - Nondo za Malangali Seco)
 
Faiza unauhakika na hilo unasema kua nyerere kamua karume na chama chake tanu
kuna tetesi nyingi. mojawapo wanasema karume alimweka kizuizini baba mzazi wa himid. akiwa mtiifu wa mapinduzi himid alimwendea karume kumsihi na kumuomba amwache huru baba yake na kumhakikishia asingekuwa opponent mapinduzi. karume akamkubalia bila kutekeleza. baadae himidi akaja ambiwa baba yake alishauwawa tena kikatlisana kwaamri ya karume. ndipo mwanaume akaamua kufanyayaliyompata karume. mwosha huoshwa
 
Huyu ni Mtoto wake, Mwenyewe Thabit Kombo ameshafariki na huyu Mzee ndie aliempendekeza Ndg Ally Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar baada ya kutimuliwa Aboud Jumbe wakati wa Mchafuko wa Hali ya kisiasa Zanzibar kipindi ambacho Mwl Nyerere alimfukuza Jumbe bila ya kupanga Mrithi wake ndo Mzee Thabit akiwa tayari mlemavu wa Macho akaokoa Jahazi.

nyerere alitaka salim awe next president. akijua atapata pingamizi akatakamuomba mwinyi kuwa atamtaja lakini atie geresha na kwamba anamwachia nafasi hiyo salim. kabla ya siku kuwadia mwinyi akaenda kuomba ushauri kwa thabiti komno. kombo akamshangaa - yani wewe hutaki uraisi wa mungano 0 ama kweli. huyu anataka kukufanya wewe punda wa dobi. akirogwa kutaja jina lako kubali. siku ya siku mzanaki with full confidence akataja jina la mwinyi na mwinyi akakubali ikifuatiwa na wawawwawa kama walivyo magamba - mwinyi akawa candidate halali wa u presidure wa TZ
 
Wote tunafahamu Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheikh Karume (Mungu amrehemu) aliuawa huko ZNZ, mwenye kujua muuaji au alipanga mauaji hayo atujuze
 
Mkihoji sana mtaambiwa mnawatukana waasisi wa taifa hili na Kinana na Nape watawafungia safari kwa shs 600m kuwajibu. Halafu mtaleta mfarakano wa matumizi ya fedha Lumumba bure. Hebu acheni "chama chetu" kitulie jamani.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Sheikh Karume aliwaua au kuwatesa wafuasi wa ZPPP na ZNP au hizbulwattan sambamba na kuwafukuza. Wengi wao walifungwa na kuitwa WAFUNGWA WA KISIASA, na utaratibu ilikuwa kusomwa mashtaka na kutolewa hukumu ya Mabaraza la Mapinduzi lililoongozwa na Karume yeye mwenyewe. Na wafungwa wa kisiasa walipewa vifungo vya MIAKA 10, kiasi kwamba unapoenda kusomewa mashtaka kila mtu alitarajia ufungwe miaka 10, hakukuwa na utawala wa sheria wala katiba.wafuasi wa hizbu waliokimbilia Tanzania Bara kujishughulisha na mambo mengine kabisa hawakukaa kwa amani japo hawakuwa na jeshi wala ushawishi wowote Tanganyika, daima walikamatwa na kurejeshwa Zanzibari na kupewa vifungo vya miaka 10. wafungwa wengi walimaliza au kufunguliwa miaka ya mwisho au mwaka aliouawa kiongozi wa serikali ya mavamizi.na waliapizwa wakisika wanajihusisha na siasa au harakati zozote zinazoweza kupimwa za kutaka madaraka basi safari hiyo sio kifungo cha miaka 10 ni KUPIGWA RISASI.
 
Mauaji ya Sheikh Karume ni halali kwa kiasi kikubwa sababu hakutaka kuimarisha umoja ndani ya taifa lake na badala yake alijenga jamii yenye mifarakano hasa kwa wafuasi wa ZPPP na Hizbu. Kuwafukuza kazi na wengine kuwataka watoke warudi kwao mwaka 1964 waarabu walioingia Zanzibari karne ya 11 yaani mwaka 1100's. Baada ya mapinduzi watu wenye asili ya kiarabu walinyang'anywa mali na vitu vyao walivyokuwanavyo kwa zaidi ya miaka 500. HUU ULIKUWA NI UKATIRI WA HALI YA JUU hata kama kweli au kwa kiasi fulani walipata vitu hivyo kwa unyonyaji Zanzibari ni nyumbani kwao hawana sehemu nyingine.

Hujuma ndani ya ASP dhidi ya viongozi aliowaona kuwa na ushawishi kuweza kuhatarisha utawala wake kuwaua, kuwatesa, kuwafunga jela, kuwafukuza Zanzibari kwa kuwateua kuwa Mabalozi, Mawaziri serikali ya Muungano. Hiyo ilijenga chuki kubwa baina yake na mavamizi wenzake, TAYARI AMEJENGA MAADUI WAWILI.

MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibari, kupitia historia na miaka niliyosoma hapa na sehemu nyingine ni wazi Sheikh Karume alijiunga katika muungano kutokana na wasiwasi wa serikali aliyoipindua kuweza kurejea tena Zanzibari na kumshambulia, vilevile hakuwaamini Umma Party. Njia pekee ya kuimarisha usalama ni kujiunga Muungano na majeshi ya Tanganyika yalienda Zanzibari kuimarisha ulinzi.

Mwl.Nyerere alijitoa sana katika Muungano kwa lengo wazi ambalo daima Afrika na Dunia ilijua dhamira yake ya kutaka umoja na mtengamano Barani Afrika. Lakini Sheikh Karume alikuwa na malengo tofauti na dhamira kisasi dhulma, hujuma kwa waarabu utumwa wa ndoa na kutawala bila kufanya uchaguzi kwa miaka 50. yaani 1964 hadi 2014, nani anaweza tabiri huenda Mungu angembakiza yangetokea machafuko makubwa.

NANI ALIMUUA SHEIKH KARUME?
Nikirejea mipango ya kuuawa kwa Sheikh Karume, hasa majukumu waliyopewa kundi lililokuwa Zanzibari kujipanga kwa kuiba silaha na baadae kuwa katika wakati mgumu baada kundi lililokuwa Dar es Salaam kushindwa kutimiza majukumu yao.
Kwa mipango iliyokuwepo awali ni dhairi lengo kuu ilikuwa kuipindua serikali ya Sheikh Karume na sio kumuua, ikiwa mpango wa kupindua ulishindikana kwa nini mauaji ya Sheikh Karume?
Ndio kusema wengi wao hasa waliokuwa na jukumu la kutekeleza upinduaji wa serikali ya Sheikh Karume walikuwa na kisasi mioyoni mwao (kutbarek bin kisasi). Kwa sababu waliamini uhai wao upo kulipiza kisasi hawakujali lile litakalowakuta hata baada ya kutekeleza hazma yao.

Kumbuka kundi lililokuwepo Zanzibar walianza kuchunguzwa na kutafutwa hasa baada ya kugundulika upotevu wa silaha hivyo basi wangeacha kufanya lolote wangeuawa au wangejaribu kutoroka wangekamatwa na baadae kuuawa kama kina Abdallah Kassim Hanga. Hivyo mauaji ya Sheikh Karume yalifanywa na watu waliokuwa na msukumo, wasiwasi wa dhahama baada ya jaribio lao kushindwa. Na mwenye hasira dhidi ya Sheikh Karume ni dhairi alijitolea KUFA kulipiza kisasi cha kifo cha BABA YAKE.

Hitimisho, Abdulraham Babu alikuwa na nia ya kupindua lakini alishindwa na kukatisha safari yake ya Zanzibari. Katika mazingira haya Mwl.Nyerere hakuhusika na mipango yoyote ya kumuua Sheikh Karume lakini kwa kero na usumbufu wake hata kama aliambiwa MZEE kuna hili jambo linaendelea huendwa alijibu SAWA. Kuona jambo linaelekea kutendeka pasina ushiriki wako ukalinyamazia ni sawa na kulibariki au kuridhia"asukumalatu ridhaa".
Kwahiyo Sheikh Karume aliuawa na watu waliokuwa na chuki naye, kwa kuwa aliwaudhi watu wengi ni dhairi kifo chake kilikuwa ni furaha, au kilitoa ahueni na kubadilisha upepo wa kisiasa.
 
hadithi ya karume yataka kitako na fikra pevu huru.
Kuna masuala ya kujiuliza.
Karume alikua makamo wa rais wa Tanzania na Raia wa Zanziabr
aliuliwa kwa kupigwa shaba mchana kweupee
walomuua ni wana jeshi sio raia
kati ya walokwenda Kisiwandui makao ya ASP ni wanajeshi watatu
Luteni Humudy
Captain Chwaya
Captain Ahmada

Humudy alipigwa riasasi na walinzi walokua nje. na Ahmada na Chwaya wakakimbia kwa gari lao.
Inasemakana walipigana mpaka risasi zikawaishia. na Jeshi lilikua na uwezo wa kuwakamata hai na wangetosha kuwa mashahidi wazuri lakini wote waliuliwa wakiwa wazima.Ushahidi ukapotea mpaka leo...sawa na kifo cha Raid Kennedy wa USA Aliemuua alipokamatwa alipigwa risasi na jamaa wa usalama na yeye baadae akapigwa risasi ..mpaka lei kisa chake kimebaki ni conspiracy theory tu.

turudi kwetu na Karume
mara baada ya mauaji yale watu wengi sana walikamatwa na kuteswa na walokusudiwa sana ni Umma party chama kilicho jiunga na ASP mara baada ya mapinduzi. Hawa ndio pekee walokua wasomi na mwiba mkuu kwa karume na hata muungano
hawa ni kina Babu
salim ahmed salim
Diria
issa sultan issa
qulateein
nk
baadae wakaundiwa kesi ya uhaini na wengine kufungwa miaka kadhaa, wengine maisha na wengine kifo. Lakini baadae wote walisamehewa na kutoka jela.

sasa tujiulize iweje watu walo muua makamo wa rasi wa Tanzania wasamehewe ?

hapa kwa mawazo yangu kesi ile ilikua funika kombe mwanaharamu apite kama alivowahi kusema Babu...
kifo chake ni kitendawili na mazingara yanaonesha hakukuwa na jaribio lolote la kutaka kupindua serikali kulikua na mipango mengine ambayo itabaki kuwa siri ya walo andaa
 
Ni mada nzuri sana. Aliyoyapata ni kutokana na alichowahi kutenda maishani mwake. What goes around comes around. Na kama ulivyosema kuwa watatokea watu kutoka nje watakaotafiti hizo issue na kufichua mengi, upo sahihi. Wapo ambao wameanza kufuatilia hiyo case na kuandikia kitabu chake.

Pia Kuna sehemu ni kaburi la maelfu ya watu na juu yake pakajengwa ili kuficha siri. Kuna watafiti soon watakuja kuanza kufukua baadhi ya masalia na kupima miili na chanzo cha vifo vyao. Pia kuna kitabu kimeandikwa na mu-Asia ameelezea yote hayo kwani wakati huo alikuwa ni mdogo na anaishi Zanzibar na wazazi wake walifukizwa na serikali za Karume na wengine kutendewa ukatili.

Kuna siri nyingi sana zinafichwa na uhuru wa watanzania katika kufuatilia ni mdogo sana. Hatuna uhuru. Tunatawaliwa na sisi wenyewe bila kujijua. Hizi issues ukizifuatilia hata kama ni msomi mhusika unakataliwa na unaweza kuhatarisha maisha yako.
 
Ni mada nzuri sana. Aliyoyapata ni kutokana na alichowahi kutenda maishani mwake. What goes around comes around. Na kama ulivyosema kuwa watatokea watu kutoka nje watakaotafiti hizo issue na kufichua mengi, upo sahihi. Wapo ambao wameanza kufuatilia hiyo case na kuandikia kitabu chake.

Pia Kuna sehemu ni kaburi la maelfu ya watu na juu yake pakajengwa ili kuficha siri. Kuna watafiti soon watakuja kuanza kufukua baadhi ya masalia na kupima miili na chanzo cha vifo vyao. Pia kuna kitabu kimeandikwa na mu-Asia ameelezea yote hayo kwani wakati huo alikuwa ni mdogo na anaishi Zanzibar na wazazi wake walifukizwa na serikali za Karume na wengine kutendewa ukatili.

Kuna siri nyingi sana zinafichwa na uhuru wa watanzania katika kufuatilia ni mdogo sana. Hatuna uhuru. Tunatawaliwa na sisi wenyewe bila kujijua. Hizi issues ukizifuatilia hata kama ni msomi mhusika unakataliwa na unaweza kuhatarisha maisha yako.
naomba kujua jina la hicho kitabu tafadhali.ili nikakidurusu
 
Back
Top Bottom