Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika!

This is very interesting information! Lakini Unaweza kudokeza chanzo cha tuhuma zako hizo, ama ndio wale wale?
 
unataka kusema aliewai kuwa mkuu magogoni ndo anahusika na mchezo wote


mhnn!... josaya binafsi ninavyojua ulichoandika ni mwendelezo siasa za chuki na uchonganushi kati ya jamii za watanzania. aliegusia ukweli kuhusu mada hii ni aliesema kuhusu mtoto wa mfalume kufanya mauaji kwa kulipiza kisasi nje na kushauliwa na wabara. maana uhuru wa znz ni mjibu ya hili. mfalume aliisahau sana unguja aliko kuwa mzee karume na masikini wengi sana na pemba kulikuwa wakati huo wa mfalume saaafi. unaweza kufikilia vzr zaidi kwanzia hapo. unahisi au kufahamu mapinduzi ya zanzibar husherekewa zaidi wapi kati ya pmba na ungja.

Mwendelezo wa siasa za chuki ni sumu kwa Taifa letu.
 
Nyerere ndie muuwaji tena kwa maagizo ya walewale waliomtuma aungane na zanzibar. Pale mzee karume alipoona muungano umejaa ubabaishi na alipotoa kauli ya kuwa muungano ni kama koti likituzidi tunalivua ndipo Nyerere alipoamua kumuua. Alipotekeleza mauaji yake ndio akampa Aboud Jumbe kiti cha Urais lakini hata jumbe mwenyewe alipoanza kuhoji baadhi ya mambo ya muungano nae akapigwa chini na kuanza kupotezewa kama vile hakuwa rais wa nchi bali mwenyekiti wa kijiji. Amshukuru Dr. Jakaya kikwete kwakumkumbuka alipopata madaraka na kumjengea nyumba mbili moja zanzibar na kigamboni. Nyerere hautokuja punzika kwa amani kwa damu uliyoimwaga kwa watu wasio na hatia. Mungu akulaani na akuchome maradufu.
 
Nyerere ndie muuwaji tena kwa maagizo ya walewale waliomtuma aungane na zanzibar. Pale mzee karume alipoona muungano umejaa ubabaishi na alipotoa kauli ya kuwa muungano ni kama koti likituzidi tunalivua ndipo Nyerere alipoamua kumuua. Alipotekeleza mauaji yake ndio akampa Aboud Jumbe kiti cha Urais lakini hata jumbe mwenyewe alipoanza kuhoji baadhi ya mambo ya muungano nae akapigwa chini na kuanza kupotezewa kama vile hakuwa rais wa nchi bali mwenyekiti wa kijiji. Amshukuru Dr. Jakaya kikwete kwakumkumbuka alipopata madaraka na kumjengea nyumba mbili moja zanzibar na kigamboni. Nyerere hautokuja punzika kwa amani kwa damu uliyoimwaga kwa watu wasio na hatia. Mungu akulaani na akuchome maradufu.
Duh!!! Ya kweli haya. Inaalilahi Waina ilaihi rajiuun.
 
kuna three type of secrety, cofidential ,normal ,top secrety.....but these are top secrety zmzeealimundoa karume kwa sababu ya muungano. na mzee pia alimuondoa sokoine coz alivuta mipaka ya utawala, rais wa nchi anaruhusiwa kuua in case of national interest na wala si dhambi..rais anaweza akaua km akiridhika na security detail anazopewa na tiss
 
Ikiwa leo ni miaka 42 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, ndugu Abeid Aman Karume, aliyeuwawa kwa risasi na watu wanaosadikika ni wapinga maendeleo. Mengi yamezungumzwa ikiwemo suala la Nyerere kuwa nyuma ya mauaji hayo. Hoja kuu ikiwa ni kwamba Karume alitaka kuuvunja muungano. Hali iliyopelekea kutofautiana kwa wawili hao,Je ni kweli Nyerere alihusika na kifo hiko kama ambavyo imezungumzwa sana, karibuni tujadili...
 
Hakuna ushahidi hivyo ni propaganda kwani waliomuua walikamatwa lakini hawakumtaja Nyerere hivyo hakuna hoja katika huu uzi wako.
 
Japo kuwa inasemekana walikuwa wameshatofautiana sana kiasi cha kuwa wanawasiliana kupitia mtu wa tatu lkn hakuna ukweli wa Nyerere kuhusika na mauaji ya Karume.
 
abdulrahaman babu mmoja wa watu walioshukiwa kumuua Karume, aliachiwa huru na Nyerere baada ya kukaa gerezani kwa muda mfupi, nayo ni moja ya sababu ambazo watu waliibua minong'ono kuhusu Nyerere na kifo cha Karume...
 
Mzee Muhammed Baramia alikuwa memba wa Chama cha Umma na alihusika katika kesi ya mauwaji ya marehemu Mzee Abeid Amani Karume. Hivi sasa ni memba wa Chama cha Wananchi (CUF) na ni Imamu wa Msikiti.



Halikuwa jaribio la kwanza. La 1972 tulipanga tangu 1968. Madhumuni khasa ilikuwa kukamata serikali ya Zanzibar. 1968 tulijiona kidogo. Sababu ni tuliona kuna mabadiliko against [dhidi] yetu. Upepo ulikwisha anza kutugeukia. Karume kaifanyia hii nchi kama moja kwa moja yake, hasikilizi mtu, anafanya anavotaka. Mwisho wake ilikuwa baada ya wale kina Hanga, kina Twala, kina Saleh Saadalla, nani…, sasa alikuwa anamtaka Babu. Ndo akasema hasa, "lipo Hizbu kubwa huko Dar es Salaam, tunalitaka hapa." Kwenye mkutano wa hadhara.

Kweli Babu alikuwa Katibu Mkuu wa Hizbu na ndo maana Karume akasema "Hizbu kubwa." Sasa anaanza kumtia hewani, kumuandama. Anamtaka yeye kwa kuwa aje au atavunja muungano. Alimwambia Nyerere hivo. Akiogopa kwa sababu wataalamu wote yeye hawataki. Kina Twala, kina Hanga…Yeye na Sefu Bakari kuwa waendeshe nchi wanavotaka, wafanye wanavotaka, hivo ndo ilivokuwa. Baada ya kutangaza hivo sisi tukaitana, hapa Zanzibar na Dar es Salaam, mikutano ilikuwa mingi. Hata mie nafsi yangu nilimwambia Sefu Bakari "mbona upepo unatubadilikia?" Akanyamaza kimya. Nilimkumbusha wakati wa interrogation [kuhojiwa]. Umesahau? Manake alinihujumu "hata wewe, wewe ulikuwa Afro-Shirazi na ghasia?" Nkamwambia "mmetugeukia."

Tukaendelea mpaka tuka-panga mipango. Kila nkiwatia kwenye line hawaingii, kina Natepe, kina nani, lakini Sefu Bakari sikuweza hata kujaribu kwa sababu alikuwa pro-Karume [akimuunga mkono] bila ya kiasi, Ali Mahfoudh alikuwa pro-Karume, akisikia chochote vilevile hatari. Wengi katika Baraza la Mapinduzi walikuwa pro-Karume. Hata Khamis Abdalla Ameir, Ali Sultani, tuliwaogopa. Badawi [Quallatein] baada ya kuhujumiwa Pemba, yeye alikuwa Waziri Mdogo, kahujumiwa na Karume, akageuka. Akabadilika akawa pamoja na sisi.

Babu akitushtakia sisi kuhusu Khamis Abdalla Ameir. Ilikuwa linakuja jambo mbele ya Baraza la Mapinduzi dhidi ya Babu, basi Khamis akinyamaza kimya na wala hakuripoti kwa Babu kwa kuwa iko hivi hivi hivi. [Saidi] Bavuai ndo alokuwa anamwambia Babu, mambo yako hivi hivi hivi. Ukisemwa hivi hivi hivi.


Basi tukenda tukafanya mkutano mpaka karibu ya mwisho tena sasa tayari mambo lakini sasa sie watu wenyewe kidogo. Mimi nafsi yangu nimewaambia Hizbu, nimewaambia wale walokuwa Mobile Force wale, Afro-Shirazi nnowaweza wale, nimewaambia. Madhumuni ilikuwa tupinduwe kijeshi. Ikafeli kwa sababu walewale tulowaambia waje, kina [Amour] Dugheshi, kina nani, wote wamefanya woga. Ila yeye Babu ndo amesema kaja mpaka pwani hapo, akarudi. Kina Tahir Ali, wamepanda boti hasa waje. Walipopanda wakaona mambo yameshavuja wakarudi. Mambo hayo lini. Alkhamisi tuliwaambia watu wote waje, tuliagana Youth Tournament inakuja hiyo, kwa kuwa na nyie kabisa, Alkhamisi tuwe tayari. Lakini alokuja mmoja tu. Hashil Seif. Bas.

Ndo baada ya kuona tumefeli ndo akapanda Cariboo bado hajajulikana, akarudi Dar es Salaam akakamatiwa hukohuko. Na wengine wengi wamekuja lakini tulikataa kuwataja majina.


Babu ilikuwa aongoze ile coup d'état [mapinduzi ya kijeshi]. Viongozi wangelikamatwa, akamatwe Karume akatangaze kwenye radio, aseme kuwa ameshindwa, na nini. Tulikuwa tuna wenzetu ndani ya jeshi. Walipoona tumefeli wakapinda wote. Sasa wakajifanya wao shrewd against [mahodari dhidi] yetu. Hao wanajeshi waliofanyiwa kampeni na Ahmada, Humudi, etc (na kadhalika)



Sisi tumepanga wiki moja ya kule store [ghala] ya silaha ni yetu sisi, na wiki moja yao wao, Afro-Shirazi. Wale walioko zamuni, wote wale wetu sisi. Kina Sindano, hao walokufa. Na wiki ya pili wanakuwa wao. Sasa sisi tulianza tangu Jumatatu kutowa silaha. Zikakaa kwa Humudi, kiasi mia, silaha mbalimbali, bastola, bunduki, machine gun. Aliziweka kwake. Humudi alimtowa mkewe akenda zake Dar es Salaam, ukumbi mzima zikawekwa silaha. Tungeweka kwa Ahmada ingelikuwa hatari. Niliwaambia tukiziweka kwa Ahmada na yeye Captain in charge wa mambo ya silaha atasachiwa. Na kweli, walishughulika juu ya Ahmada hawakumgusa Humudi. Mpaka saa tisa za jioni silaha hazijajulikana ziko wapi.

Mpaka saa kumi. Mpaka magharibi sisi tunaripuwa hazijajulikana zile silaha ziko wapi. Siku ile walipokamata wale ma-ASP ilipojulikana silaha zimeshaibiwa siku ya Ijumaa, manake wiki nzima zimekaa, siku ya Ijumaa zilipohisabiwa hakuna, kina Ali Mahfoudh wakataka kutupiga curfew ile Ijumaa usiku, sisi tukasema hatuwahi.


Humudi ndo alipata ripoti hiyo saa nne asubuhi ndo akatuletea. Kuwa tukamatwe sote siku ileile ijumaa. Saa tisa tumekutana kwa Humudi ndo tukaamuwa. Hapo alikuweko Miraji, Chwaya, Harakati, Humudi, Ahmada, kina Falahy walikuwa chumba cha pili, hawajajuwa tunazungumza nini. Ishajulikana, hapana njia isipokuwa tumpige Karume na Sefu. Kwa sababu wale hawakuja, tutafeli, kina Amari Kuku, Ali Mshamgama, wogawoga, hawakuja kwenye mkutano saa tisa. Wote hawakuja. Potelea mbali. Wale wengine, khasa Saidi [Sindano] alokamata store silaha alikwishasema "tumeshakufa."

Kwa sababu Sindano keshakimbia tangu saa nne ilipojulikana, anatafutwa. Sasa watu wetu tena wakaanza khofu. Kupatikana gari ndo Harakati akenda kuazima kwa Khamis Abdalla Ameir, manake ndo dereva wake. Nna safari yangu nataka kwenda. Sasa Khamis hajuwi anataka gari kwa sababu gani. Hajui, kampa, haya nenda. Chwaya kachukuwa gari ya People's Bank yeye ndo dhamana.

Tena kina Ahmada wakaingia katika gari ya Chwaya, pamoja na…Gari ya Khamisi, Harakati, Saidi alouliwa Vuga. Na Rashid Falahy akaingia palepale Makao Makuu [ya Afro-Shirazi]. Sasa kumi na moja unusu tuseme wametoka, kumi na mbili wameshafika pale, wakaripuwa. Gari ya Chwaya, rangi ya bluu bluu ilitokea Malindi, ya manjano, ya Khamis, ina kipande cha MBM (Memba wa Baraza la Mapinduzi) kimeandikwa, ikapitia njia ya Majestic Cinema.


Iliamuliwa kuwa tumuuwe Karume, tusimuuwe Thabit Kombo. Tumtishe tu basi. Kwa sababu kuweka mgawanyiko, iweko ubaguzi, Karume na Kombo. Wote tungewaweza ati pale lakini tumefanya makusudi tuweze kubaguwa. Afro na Shirazi labda italeta mgongano. Manake Karume ndo "Afro", yule Thabit Kombo "Shirazi."

Soma zaidi:

Source: Kitabu: Kwakeri Mkoloni, Kwaheri Uhuru Mlango wa Kumi na Saba: Hayeshi Majuto Yao | Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
 
sinema ndo inaanza, Siasa, Kisasi au Muungano??? wenye taarifa mbalimbali ziwekeni tuzijadili
 
Hakuna ushahidi hivyo ni propaganda kwani waliomuua walikamatwa lakini hawakumtaja Nyerere hivyo hakuna hoja katika huu uzi wako.

Tumia alkili wee mburura unadhani ni nani angeweza kumtaja nyerere yule mzee alikuwa mshenz alidhani yeye ataishi milele..
 
Taarifa ambazo zipo ni kwamba, Karume na wajumbe wengine wa Baraza la mapinduzi baada ya kumwangusha sultani, jambo la kwanza walilofanya ilikuwa ni kugawana wabinti wa kiarabu, na hakuna aliyeruhusiwa kukataa. Kulikuwa na binti ambaye, mjumbe mmojawapo wa baraza la mapinduzi alimtaka, baba wa binti alikataa. Karume akaamuru Baba wa binti huyo auwe. Baba yule aliuawa, na binti alichukuliwa kwa nguvu. Kaka yake wa yule binti alikuwa mpole, akajiunga na jeshi na baadaye alifikia cheo cha luteni, akaamua kulipiza kisasi kwa maauaji ya Baba yake yaliyofanywa kwa amri ya karume.

Askari yule ndiye aliyeongoza mauaji ya karume, na yeye ndiye pekee yake alifia pale kwenye ofisi za chama wakati wengine walifia kwenye nyumba waliyokuwa wamejificha, kutokana na majeraha. Sasa ni nani angefungwa au kunyongwa wakati muuaji na wale walioshirikiana naye, wote waliuawa? Mwalimu alimtoa Babu baada ya kuridhika kuwa hakuhusika na mauaji ya Karume. Mauaji ya karume yalisababishwa na tamaa ya wasichana wa kiarabu.

Kumhusisha mwalimu na maauaji ya Karume ni fikra duni kabisa. Karume aliuawa kutokana na uroho wa wajumbe wa baraza la mapinduzi kutamani mabinti wa kiarabu ambao wakati huo walikuwa hawataki kuolewa na watwana (waafrika).

abdulrahaman babu mmoja wa watu walioshukiwa kumuua Karume, aliachiwa huru na Nyerere baada ya kukaa gerezani kwa muda mfupi, nayo ni moja ya sababu ambazo watu waliibua minong'ono kuhusu Nyerere na kifo cha Karume...
 
Hakuna ushahidi hivyo ni propaganda kwani waliomuua walikamatwa lakini hawakumtaja Nyerere hivyo hakuna hoja katika huu uzi wako.

Hapana walokwenda kumuua ni vijana wa jeshi wawili Humoud na Ali Hatib Chwaya
Humoud alijeruhiwa kwa risasi akakamatwa lakini kwa sababu zisizo eleweka badala ya kuhojiwa akapigwa risasi.
Chwaya huyu alikimbia kwa gari na kukamatwa shamba kwao akiwa mzima ...baada ya kuwahangaisha sana jeshi na polisi karibu 3000 walokua wakimsaka. Njia walotumia kumpata ni kama cinema za rambo.walikusanya kijiji kizima ikiwa pamoja na mama baba mke ndugu shemeji na marafiki wakatangaza kwa vipaza sauti kuwa wataua mmoja mmoja au ajitokeze...ndipo akajitikeza akiwa mzima kabisa lakini naye akiwa njiani chini ya ulinzi akapigwa risasi...
Hivyo ushahidi muhimu wa wauaji ukafinyangwa na ikabaki kukamata watu wengine kubabaisha lengo.
Kisa cha karume ni sawa na mauaji ya Kennedy..muuaji wake Osward alipigwa risasi akiwa mikononi mwa FBI
Kuna utata mkubwa lakini kuuliwa kwa karume sio kisasi wala kupindua serikali...ndio maana mshukiwa mkubwa babu aliachiwa na nyerere akenda ulaya na kanali Ali Mahfoudh akapewa ulaji kwa Samora
 
Tumia alkili wee mburura unadhani ni nani angeweza kumtaja nyerere yule mzee alikuwa mshenz alidhani yeye ataishi milele..
Boss umburula wangu uko wapi hapa??Ila asante kama ukubaliani na mawazo ya mtu usimtukane maana yawezekana wewe u-mtoto wa haramu ukuja kwa njia ya kawaida!kama umezaliwa kinondoni mkunguni basi hapa ntakushikisha adabu hapa wengine ni baba zako japo mamako hakukwambia hilo kwakuwa alikuwa hajui niyupi alompa mimba kwakuwa mamako alikuwa kama paka mapepe!Uishie huko fuata misingi ya JF usije hapa nakuongea upuuzi kama umekalia kitu kigumu!
 
Ni miaka kibao imepita tangu mwenzetu huyu auwawe lakini sijawai kupata majibu yakuridhisha mtima wangu nani hasa alimuua huyu mzee na kwa nini? Nipeni japo mwanga kwenye hili swala wandugu manake nakosa hata mwanga wakuelezea hili ninspokuwa nalecture wanafunzi wangu.
 
Back
Top Bottom