Mauaji ya Mwangosi, sakata la Ulimboka na MwanaHalisi kulipukia TGNP

Taarifa zinasema Mwakilishi wa Dk. Ulimboka atakuwapo pia TGNP leo na suala la Ulimboka litaanikwa upya. Wanatajwa kuwapo wadau mbalimbali watakaozungumza akiwamo Jenerali Ulimwengu na wahadhiri kadhaa wa Vyuo Vikuu nchini na Saed Kubenea naye atakuwapo.
 
kwa taarifa nilizo nazo mpaka sasa ni kwamba kesho jumatano septemba 12, 2012 saa nne asubuhi kuna kongamano kubwa linaloshirikisha waandishi wa habari, madaktari, asasi zote za kiraia, madhehebu ya dini, nk. Madhumuni ya hiyo platform ni kupinga mauuaji ya daudi mwangosi na kutoa tamko la pamoja pia kuhusu kufunguliwa kwa gazeti la mwanahalisi.

Karibuni wote tusikose jamani.

Update:
Taarifa zinasema mwakilishi wa dk. Ulimboka atakuwapo pia tgnp leo na suala la ulimboka litaanikwa upya. Wanatajwa kuwapo wadau mbalimbali watakaozungumza akiwamo jenerali ulimwengu na wahadhiri kadhaa wa vyuo vikuu nchini na saed kubenea naye atakuwapo.
Hawana kazi za kufanya tuwakumbushe majukumu yao?? Maana hawawezi kuwa sirazi kwa upuuzi kama huo, pili kwanini ulimboka awakilishwe na mtu??

Wameshamfanya mtaji wa kisiasa?? Alafu inshu iwe kufungiwa gazeti la mwanahalisi kwani gazeti lahabari lilikuwa ni hilo tu mbona yapo raia mwema, tanzania daima, nipashe, mwananchi.

Nina uhakika kama sio kongamano la chadema basi litakuwa kongamano la freemansons
 
Kuwa nchi changa au kongwe sio kigezo cha wananchi kutodai haki zao. Wakati wa kugombania uhuru sababu kama zako hizi walikuwa wakoloni wakizitoa kila kukicha, mara nchi changa haina experience, mara nafasi bado haijafika etc. Laiti Mwagosi angekuwa baba yako kamwe usingeweka statement yako hapo.

Huu ni wakati pekee wa kupush reforms kwa jeshi la polisi hususan kikosi cha kuzuia ghasia kinachoongozwa kibabebabe. Excessive force inayotumiwa na polisi inanikumbusha kipindi kile Apartheid kule Afrika Kusini, kila maonevu yanapozidi na ndio subira ya wananchi inapoondoka.

Kifo cha Mwangosi iwe ndilo fundisho kuu la serikali kwamba maisha ya Mtazania ni ya kutukuzwa na kuheshimiwa.
 
Radhia Sweety, ningefurahi kuona ndugu yako mmoja ameuawa na polisi ili tuone kama utatoa comment kama hii. mwangosi ni mtu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa mungu.

Anastahili kuombolezewa sawa na ambavyo tutaomboleza baba ako mzazi na mamako mzazi watakapouawa na polisi siku wakiwa katika BUSINESS ZAO wakiwa hawajui kwamba kuna mkutano wa cdm karibu. tena yawezekana wakawa wametoka sokoni tu kisha walambe risasi kisha tutaona kama hautaomba msaada wetu kuomboleza pamoja nawe.

KAMA NI MKRISTO UNGESOMA SEHEMU Musa alipoulizwa na waebrania (waisrael) wenzake kule misri kwamba JE WEWE UNAFIKIRI UKO TOFAUTI NASI HADI UFANYE HAYA? AMA KWA SABABU WEWE WAISHI KWA FARAO NDO UNAWEZA FIKIRI UKO JUU YA WAISRAEL WOTE? Yaani unafikiri ndugu zako wapo juu ya risasi? wanaweza tu pia kuuawa wakati wakipita mbele ya polisi.
 
Kwa taarifa nilizo nazo mpaka sasa ni kwamba kesho Jumatano Septemba 12, 2012 saa nne asubuhi kuna kongamano kubwa linaloshirikisha waandishi wa habari, madaktari, asasi zote za kiraia, madhehebu ya dini, nk. madhumuni ya hiyo platform ni kupinga mauuaji ya Daudi Mwangosi na kutoa tamko la pamoja pia kuhusu kufunguliwa kwa gazeti la mwanahalisi.

karibuni wote tusikose jamani.

Update:
Taarifa zinasema Mwakilishi wa Dk. Ulimboka atakuwapo pia TGNP leo na suala la Ulimboka litaanikwa upya. Wanatajwa kuwapo wadau mbalimbali watakaozungumza akiwamo Jenerali Ulimwengu na wahadhiri kadhaa wa Vyuo Vikuu nchini na Saed Kubenea naye atakuwapo.


YES...let the wheel rolls...! Acha gurudumu lizunguke lenyewe...hadi haki lazima itawale...kila ULIMI utasema na MAWE kupaaza sauti pale HAKI inapochezewa....!
POLISISIEMU wanaingizwa choo cha kike na 'chama zee' GOP hii CCM ya wala-rushwa na wanakubali kichwa-kichwa, na kudhani taifa litasimama na kuogopa! LA HASHA! DAIMA MBELE!
 
Radhia acha hizo na kama huna la kuchangangia mjadala bora ukae kimya. Sio lazima kuchangia kabisa. Binafsi siwafahau kwa ukaribu akina Ulimboka, Mwangosi. N.k but we can. Just relax. While innocent people wanauawa na kunyanyaswa na watu kama wewe kana kwamba nchi haina wazawa, nasema wazawa maana sioni kama tuna serikali na pia najaribu kufikiria kidogo tu kwamba hivi mtu kama Radhia akipata mamlaka itakuwaje? Familia yake ikoje? Tumuogope Mungu!
 
TGNP-Tanzania Gender Networking Programme....Labda kwa kua kila mtu kaguswa kwa hili u can go on.
 
Tumechoka maandamano jamani. Hii nchi ni changa sana na inachohitaji ni watu wachapa kazi si watu wakimbia kazi kwa kisingizio cha Mwangosi. Hivi kila mtu akisema aandamane kwa ajili ya Mwangosi tutafika kweli?

Haaaaaaa haaa.
Ucnichekeshe uchanga wa nchi nini South Afrika na South sudan ndo nchi changa. Sumbua akili.
Adam smith anasema, Changes is unavoidable,if there is no changes no development. All who not accept movement 4 changes has stagnant mind.
 
Tumechoka maandamano jamani. Hii nchi ni changa sana na inachohitaji ni watu wachapa kazi si watu wakimbia kazi kwa kisingizio cha Mwangosi. Hivi kila mtu akisema aandamane kwa ajili ya Mwangosi tutafika kweli?

Na uhakika umezungukwa na harufu ya ufisadi, hivyo unafaidika na system iliyopo, maisha yako ni yale ya ari mpya kasi mpya maisha bora kwa watanzania, na unafurahia wengine kuwa maskini, kulala njaa, kufa na kuuliwa bila sababu. Tukio la Mwangosi ndo lingemtokea baba, kaka, mama nk yako sijui ugewaambia watz wachape kazi? ya wakwezi waachie wakwezi, maendeleo ya individual siyo mendeleo ya nchi, we nenda kachape kazi peke yako uone wapi pakufisadi.
 
Radhia unastaili kifo, nakueleza na wala simung'unyi maneno, kama kweli mwangosi unaona alistaili kufa kwa staili ile na sasa unataka mjadala ufungwe,tegemea lolote ndani ya siku saba..wewe nduguyo,au mtu yeyote anaekugusa..take my word.
 
Tumechoka maandamano jamani. Hii nchi ni changa sana na inachohitaji ni watu wachapa kazi si watu wakimbia kazi kwa kisingizio cha Mwangosi. Hivi kila mtu akisema aandamane kwa ajili ya Mwangosi tutafika kweli?

Watanzania ni wavivu sana! kutwa wangu wangu kulalama eti hawatendewi haki. Haki ipi kwa uvivu wa hivyo?
 
Kwanini wasiisaidie familia ya marehemu kufungua kesi mahakamani? Kwanini kongamono halifanyiki Iringa kwenye wahanga? Kwanini wahanga wa ubabe wa polisi wasio maarufu wameachwa pembeni?

Enterpreneurship iko very diverse...
 
Ndio linanza kwa Wimbo wa Tanzania nakupenda wakiongozwa na Rose Mary Mwakitwange
 
Tumechoka maandamano jamani. Hii nchi ni changa sana na inachohitaji ni watu wachapa kazi si watu wakimbia kazi kwa kisingizio cha Mwangosi. Hivi kila mtu akisema aandamane kwa ajili ya Mwangosi tutafika kweli?
Watu wote wangekuwa na mtazamo kama wako. Hakuna maendeleo yoyote ambayo yangetokea katika ulimwengu huu. Wanamapinduzi sio watu waoga kama wewe. Unasubiri nchi iwe kubwa ndiyo udai haki yako? Kuwa na fikra za mwanamapinduzi kwa ajili ya mustakabali wa taifa letu. Hakuna nchi iliyowahi kukombolewa kutoka katika matatizo ya aina yeyote ile ka watu kukaa kimya na kuendelea kufanya kazi chini ya mazingira kandamizi. Ni lazima watu wainuke na kudai haki zao kupitia njia zote zinazokubalika kisheria na maandamano ikiwa ni mojawapo ya njia hizo. Wewe unataka tukae kimya wakati tunaumizwa na wachache wanaoneemeka kwa kutukandamiza? Kwa vyovyote vile ni lazima utakuwa unanufaika na mfumo uliopo na ndiyo maana hutaki upingwe.
 
watakuwapo wazungumzaji, Ayubu Rioba, Sungusia toka LHRC, na wengineo
 
Hivi hapa nchini mauaji yameanza kwa Mwangosi. Sipingi suala la kongamano ila nahoji kuwa kama taasisi zote hizo zingeanza mshikamano huo mapema yalipoanza mauaji ya Znzbar na Mwmbchai mnadhani jeshi hili lingekuwa bado halijabadilika. Hizi sio statements ni maswali ambayo yeyote anawezakukomment.

Hapajaharibika kitu, mauaji yote hayo unayotaja yametuumiza sana. kama tulichelewa kuanza, TUANZE SASA !
 
Ananza Rioba anasema hakubaliani na kufungiwa kwa Mwanahalisi na haikubaliki sana, ananukuu JF ambayo alikua anaitegemea sana alipokua nje hivi karibuni. akakumbusha majambazi 800 kuvamia mgodi Tarime akassma waandishi wakaandika waliovamia ni majambazi na kwamba waliuwawa watano
 
Back
Top Bottom