Mauaji ya mara kwa mara ya wanajeshi wa JWTZ huku Congo, kuna mkono wa Rwanda?

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,774
2,000
Habari wanajf,
Kumekuwepo na matukio ya Mara kwa Mara yanayohusisha Wanajeshi wetu walioko Kongo kwa ajili ya kulinda amani, kuuawa na washambuliaji wanaodhaniwa kuwa ni waasi.

Lakini ikukumbukwe kuwa kumekuwepo na tetesi za muda mrefu kuwa majeshi ya Rwanda ndiyo yanayoendesha chokochoko huko Kongo kwa Maslahi ya Uchumi wa Rwanda, na mtakumbuka pia kipindi Kikwete Alipopeleka majeshi huko Rwanda na kuwafurusha waasi uhasama kati ya yeye na Kagame uliibuka kwa kasi ya 4G.

Sasa kutokana na Cinario hiyo je, kuna uwezekano Rwanda ndiyo inayohujumu Majeshi yetu huko Kongo?

Ingawa inaweza isiwe kweli lakini ningeomba wahusika walifanyie uchunguzi suala hili na pia uhusiano wa majeshi yetu na nchi hii uangaliwe kwani huenda wanachota mbinu na namna ya kuatack majeshi yetu huko Kongo kwa ajili ya maslahi yao

Nawasilisha
 

Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,251
2,000
Wabaya katika Operation hii ni hawa tunao waita Wahisani ama Wafadhili katika Umoja wa Mataifa (UN).
Wametoa maagizo kutoshambulia pale mnapo letewa Mashambulizi kutoka kwa Waasi...!

Tangu kutekelezwa kwa Maagizo/Maelekezo hayo, hali inazidi kuwa mbaya kwa walinda Amani, sasa sijui ni nani ananufaika kuwepo na idadi kubwa Vifo vya Wanajeshi wetu.
 

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,774
2,000
Wabaya katika Operation hii ni hawa tunao waita Wahisani ama Wafadhili katika Umoja wa Mataifa (UN).
Wametoa maagizo kutoshambulia pale mnapo letewa Mashambulizi kutoka kwa Waasi...!

Tangu kutekelezwa kwa Maagizo/Maelekezo hayo, hali inazidi kuwa mbaya kwa walinda Amani, sasa sijui ni nani ananufaika kuwepo na idadi kubwa Vifo vya Wanajeshi wetu.
Hapo chacha!
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,776
2,000
Uganda na Rwanda walikuwepo wakiiba Rasilimali za Congo kwa kipindi kirefu kwa kukitumia kikundi cha kijeshi cha M23 ndipo kikwete na Kabila wakabuni mbinu za kupata madini ili na wao wagawane kikwete akapeleka Jeshi imara wakawafukuza M23 kabila na kikwete wakawa wakigawana madini yote kimya kimya Kitendo ambacho kilimkera sana Kagame akafikia hatua ya kumtishia maisha kikwete na ndipo kikwete akaanzisha Oparation kimbunga kuwafukuza wanyarwanda wote wanaoishi Tanzania kienyeji mpaka kagame akapagawa na kuomba Suluhu, lakini akaendelea kuwa na kinyongo moyoni na sasa kaamua kuwaua JWTZ kwa kutumia vikundi vinginevyo ili magufuli aamue kuwatoa Congo kisha yy na Mseveni warejee congo na m23 kuendelea kuiba Rasilimali za Congo . Rwanda na Uganda wanajua mchezo wote unaofanyika sasa.
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
3,831
2,000
Rwanda na Uganda lao ni moja. Wote wananufaika na yanayotokea DRC.

Nahisi kinachofanyika sasa ni kuifanyaTanzania iamue kuondoa majeshi yake huko DRC ili waendelee na wizi wao wa madini.
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,776
2,000
Kuna kitu watakuwa wanafanya hao wabongo.
Lazima kutakuwa na kitu huwa wanafanya huko
Congo ina utajiri mkubwa wa madini
Jeshi la Tanzania lipo congo kwa ajili ya kulinda Dili la kikwete na Kabila baada ya kuwapora Mseveni na kagame, kinachofanyika sasa ni Uganda na Rwanda kuwatuma comandoo wakawavalisha sare za vikundi vya waasi wanaenda congo kuwaua Asikari wa JWTZ ambao hawaruhusiwi kupigana vita kwa sheria za UN , baada ya kuuawa kwa wingi kinachofuata ni magufuli kuwarejesha Nyumbani kisha Kagame na Mseveni watarejea Congo kuendelea kuiba madini na Rasilimali Zingine.
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,776
2,000
Rwanda na Uganda lao ni moja. Wote wananufaika na yanayotokea DRC.

Nahisi kinachofanyika sasa ni kuifanyaTanzania iamue kuondoa majeshi yake huko DRC ili waendelee na wizi wao wa madini.
Ndiyo Ukweli wenyewe na kama Tanzania wanataka kubakia salama ni bora wavunje sheria za UN waamue kuingia vitani kwa nguvu wawashambulie hao waasi kwa siraha kali na mbinu za kisayansi mpaka wawatokomeze wote kinyume na hapo kuna Ajenda ya Siri kati ya magufuli na Kagame.
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,776
2,000
Kuna manufaa gani kuweka wanajeshi wetu kongo??Warudi nyumbani!!Anae nufaika aende yeye na wanae!!
Kwa sasa hakuna manufaa zaidi ya hilo fungu la UN wanalolipwa jwtz kupigwa panga na viongozi huku wanajeshi wenyewe wakijipatia vipato humo na mwenye Dili kikwete na Kabila wakivuna Madini yao, inaelekea Kabila hajampatia mgao magufuli ndiyo maana Magufuli kaamua ale Dili na Kagame wapate kugawana Madini kibao wenyewe huku Jeshi la Rwanda na Uganda wakifanya kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom