Mauaji ya Mahmoud Al-Mabhouh Mmoja wa Viongozi wa Kundi la Hamas la Palestina

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,627
154,986
MAUAJI YA MAHMOUD AL-MABHOUH

MMOJA WA VIONGOZI WA KUNDI LA HAMAS LA PALESTINA:

SEHEMU YA KWANZA:

Mahmoud al-Mabhouh (kwa Kiarabu: محمود المبحوح‎, Maḥmūd al-Mabḥūḥ); alizaliwa tarehe 14 Februari mwak 1961 – na kuuawa tarehe 19 Januari mwaka 2010, katika mauaji yaliyofanyika katika chumba cha hoteli huko Dubai.

Al-Mabhouh— mwanzilishi mwenza wa Izz ad-Din al-Qassam Brigades, tawi la Kijeshi la Hamas—alikuwa anatafutwa na serikali ya Israeli kwa kuwateka na kuwaua askari wawili wa Israeli mwaka 1989 pia akihusika na ununuzi wa silaha kutoka Iran kwa ajili ya kutumika huko Gaza; hii ilikuwa sababu kubwa ya kuuawa kwake.

Mauaji yake kwa sehemu yaliutikisa ulimwengu hii ni kutokana na madai kwamba yaliamrishwa na serikali ya Israeli na kutekelezwa na mawakala wa Mossad wakitumia udanganyifu na hati za kugushi za kusafiria kutoka nchi mbalimbali za Ulaya na Australia.

Picha za washukiwa 26 na majina yao mara moja ziliwekwa katika orodha ya watu wanaotafutwa na Interpol.

Polisi wa Dubai waligundua kuwa washukiwa 12 walitumia hati za kusafiria za Uingereza, huku washukiwa wengine sita walitumia hati za Ireland, wanne za Ufaransa, mmoja ya Ujerumani, na watatu za Australia. Interpol na polisi wa Dubai waliamini kuwa washukiwa hao waliiba vitambulisho vya wahusika halisi, hasa Waisrael wenye uraia wa nchi mbili. Wapalestina wawili, ambao Hamas iliamini kuwa ni maafisa usalama wa zamani wa Fatah na ambao kwa wakati huo walikuwa wameajiriwa na Fatah kama maafisa waandamizi, walitiwa mbaroni jijini Dubai, kwa kushukiwa kuwa mmoja wao aliandaa mazingira ya kilojistiki kwa timu ya wauaji. Pamoja na madai hayo ya Hamas, mamlaka za Dubai hazikusema chochote kuhusiana na tukio hilo au kuwatambua Wapelestina hao wawili waliokuwa wanashukiwa.

Kulingana na ripoti ya mwanzo, Al-Mabhouh alileweshwa kwa madawa, kisha akapigwa na shoti ya umeme na kukabwa. Luteni Jenerali Dhahi Khalfan Tamim wa jeshi la polisi Dubai Alisema washukiwa walimfuatilia Al-Mabhouh Dubai toka akiwa Damascus, nchini Syria. Waliwasili kutokea sehemu mbalimbali za Ulaya na kukaa hoteli tofauti, bila shaka kukwepa kugundulika na ukiondoa washirika wake watatu wanaoshukiwa kuwa "walisaidia kutengeneza mazingira" ambao waliondoka kwa boti kwenda Iran miezi kadhaa kabla ya mauaji, washukiwa wengine wote walitawanyika baada ya mauaji kwenda nchi mbalimbali.

Mkuu wa polisi wa Dubai alisema ana uhakika wa asiliana 99% kwamba mauaji yale ilikuwa ni kazi ya Mossad wa Israel. Tarehe 1 Machi mwaka 2010, alieleza kwamba alikuwa na "uhakika" kwamba wale wote wanaoshukiwa kufanya mauaji hayo walikuwa wamejificha nchini Israel.

Alisema kwamba Dubai wataomba hati ya kumkamata Meir Dagan, Mkuu wa Mossad, iwapo itathibitika kwamba Mossad ilijihusisha na kuwajibika na mauaji hayo. Uongozi wa Hamas nao ulisema Israel inahusika, na wakaapa kulipiza kisasi. Hamas, ambao wao binafsi walikuwa katika orodha ya Marekani kama taasisi ya kigaidi ya kigeni, pia kuorodheshwa na Jumuia ya nchi za Ulaya kama taasisi ya kigaidi ya kigeni, na pia kuchukuliwa kama taasisi ya kigaidi na serikali za Israel, na Japan, na kuchukuliwa kama tawi la Kijeshi na serikali za Uingereza na Australia, waliomba kwamba Israel nayo ijumuishwe katika orodha ya magaidi na Jumuia ya Ulaya kwa sababu ya kuhisiwa kwamba Israel walihusika na mauaji hayo.

Hata hivyo, baadaye mwezi Machi, Mkuu wa polisi wa Dubai alisema, "Sasa nina uhakika kabisa kwamba walikuwa Mossad", na akaendelea kusema "Nimempelekea Mwendesha Mashtaka wa (Dubai) maombi ya kumkamata (Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin) Netanyahu na Mkuu wa Mossad" kwa mauaji. Khalfan alisema pia kuwa Mshirika mmoja wa Hamas aliwapa maelezo Mossad. Hii ilikanushwa na Hamas ambao waliilaumu Fatah kwa kuisaidia timu ya wauaji ya Mossad.

Mwezi Machi, mwaka 2010, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Uingereza, David Miliband, alimfukuza nchini humo afisa ubalozi wa Israeli baada ya Wakala wa Makosa ya Uhalifu nchini Uingereza kugundua kuwa Israel waligushi nakala za hati za kusafiria za Uingereza.

Tarehe 24 May, mwaka 2010 serikali ya Australia ilimfukuza nchini humo afisa ubalozi wa Israeli baada ya kujiridhisha kwamba "bila shaka yoyote ile Israel ilikuwa nyuma ya mpango wa kugushi hati nne za kusafiria za Australia" zilizohusiana na mauaji hayo. Hatua kama hiyo ilichukuliwa pia na Ireland. Israel ilikataa kusema chochote kwa namna walivyokuwa wanashitumiwa kwamba vyombo vyake vya usalama vilikuwa nyuma ya mauaji hayo.

Tarehe 30 Septemba mwaka 2010, Mkuu wa polisi wa Dubai Dahi Khalfan alisema kwamba amepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wakala mmoja wa ujasusi wa Israel Mossad wakimuhusisha na kitendo chake cha kufichua mipango yote ya mauaji ya al-Mabhouh, lakini pamoja na kwamba hali hiyo ilitokea ilibaki bila uthibitisho.

MAUAJI YA MAHMOUD AL- MABHOUH:

MMOJA WA VIONGOZI WA KUNDI LA HAMAS LA PALESTINA:

SEHEMU YA PILI:

Wasomaji wapendwa leo tunaendelea na sehemu ya pili kuhusu mauaji ya al Mabhouh mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la Hamas.

Kama tulivyokwishakuona katika sehemu ya kwanza kuwa tarehe19 Januari, mwaka 2010, al-Mabhouh aliuawa katika chumba chake alichokuwa amepanga katika hoteli jijini Dubai, baada ya kuwa amefuatiliwa na washukiwa karibu 29 (huku washukiwa 26 ambao picha kutoka kwenye hati zao za kusafiria zikiwa zimetolewa hadharani, ambapo Wapalestina wawili walitiwa mbaroni, pamoja na mshukiwa mwingine ambaye hakujulikana jina lake naye alikamatwa pia), hao washukiwa 26 walibeba hati za kusafiria za kugushi na zenye udanganyifu kutoka sehemu mbalimbali za mataifa ya Ulaya.

Gazeti la Sunday Times liliripoti kuwa uondokaji wa al-Mabhouh kutoka Damascus kwenda Dubai katika ndege ya Emirates Flight namba 912 saa 4:05 asubuhi ya siku ya tarehe 19 Januari, mwaka 2010 ulikuwa unafuatiliwa na wakala wa ujasusi aliyekuwa chini pale uwanja wa ndege jijini Damascus.

Salah Bardawil, Mbunge wa Hamas, alisema al-Mabhouh alijiweka mwenyewe katika hatari kwa kufanya booking ya safari yake online mtandaoni na kuwajulisha familia yake huko Gaza kwa njia ya simu hoteli ambayo angefikia na kukaa katika safari yake hiyo.

Licha ya ripoti kwamba al-Mabhouh alisafiri kwa hati bandia ya kusafiria yenye jina bandia la "Mahmoud Abdul Raouf Mohammed", Hamas na maofisa wa Dubai walisisitiza kwamba al-Mabhouh aliingia katika nchi hiyo kwa utambulisho wake halisi saa 9:15 alasiri.

Kawaida al-Mabhouh angekuwa analindwa na walinzi wake, lakini kuwasili kwao kulicheleweshwa kwa sababu walinzi hawakupata tiketi katika ndege ile aliyopanda Boss wao, kwakuwa "Hakukuwa na chumba kwa ajili yao katika ndege," alisema Talal Nasser, msemaji wa Hamas jijini Damascus. "Kwa hiyo, alisafiri peke yake, na walinzi wa usalama walitegemewa kujiunga naye siku inayofuta."

Kwa mujibu wa makala ya gazeti la Ufaransa la Le Monde wakimnukuu afisa mwandamizi wa shirika la ujasusi la Ufaransa, Mossad walipanga mipango ya kumuua Mabhouh nje ya Paris. Mossad inadaiwa waliweka zamu na kituo cha kumdhibiti katika hotel kwenye kitongoji cha Bercy nje kidogo ya jiji la Paris wakiwa wametegesha kompyuta na simu za usalama.

Mkuu wa Polisi wa Dubai, Luteni Jenerali Dahi Khalfan Tamim, alieleza kwamba al-Mabhouh alipowasili Dubai alikuwa safarini kuelekea China. Alipowasili Dubai, al-Mabhouh alichukua taxi kwenda Al Bustan Rotana Hotel na alipanga chumba namba 230. Aliomba chumba ambacho kisichokuwa na kibaraza na dirisha lililozibwa, hivyo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuingia kupitia sehemu hizo bali kwa kupitia mlangoni tu. Aliondoka hotelini kati ya saa 10:30 na 11:00, jioni baada ya kama ya saa moja hivi toka alipowasili hotelini. Nini alifanya katika muda wa masaa matatu au manne yaliyofuatia inabaki kutokujulikana.

Mkuu wa Polisi wa Dubai alisema hakukutana na mtu yeyote katika emirate na kuwa alikwenda kufanya manunuzi tu. Wakati huo huo, timu ya wauaji walivunja na kuingia katika chumba chake. Saa 2:24 usiku al-Mabhouh alirudi chumbani, na mara nusu saa baadaye alishindwa kujibu simu kutoka kwa mkewe.

Picha kutoka kwenye kamera za usalama za hotelini zilitolewa kwa jamii kuwaonyesha washukiwa, ambao waliwasili katika ndege tofauti, na namna walivyokutana hotelini. Wakati inaonekana washukiwa waliamua kutumia vifaa binafsi vya mawasiliano miongoni mwao ili kukwepa kufuatiliwa, washukiwa hao ilidaiwa na polisi wa Dubai kutuma na kupokea ujumbe wa SMS kwa namba za simu nchini Austria. Wakati al-Mabhouh alipowasili kwenye mida ya saa 9:00 alasili, washukiwa wawili waliovalia mavazi ya tennis walimfutilia katika ukumbi ili kugundua chumba alichopanga, na pia kujua namba ya chumba hicho.

Maelezo ya Polisi wa Dubai yalidai kuwa mawasiliano yalikuwa yanafanyika na mtu wa kati (third party), ambaye alipigiwa simu kutoka hoteli tofauti na kuambiwa apange chumba 237. Kwa mujibu wa video za usalama, mtu aliyepanga chumba 237 hakuingia chumbani, lakini alionekana akimpa funguo za chumba mshirika aliyekuwa sehemu ya mapokezi ya hoteli, na mara moja akaondoka Dubai, kabla ya mauaji. Al-Mabhouh, baadaye, alitoka hotelini na wakati baadhi ya washukiwa wakiwa wamebaki wanamuangalia, ilifikiriwa kwamba mshukiwa (washukiwa) walijaribu kuweza kuingia kwenye chumba chake.

Mshukiwa mmoja aliyekuwa anaangalia alionekana kwenye video akimchelewesha mtalii mmoja aliyekuwa anataka kutoka katika lifti katika gorofa ya pili kwa wakati huo, bila shaka kuwapa nafasi watu wengine katika timu hiyo kufanya tukio. Wakati huohuo mshukiwa mwingine ilidaiwa alikuwa anamchanganya mtalii mwingine na, kwamba washukiwa wanne waliingia kwenye chumba cha muhanga na kumsubiri arudi. Ushahidi wa hili ni ukweli kuwa watu wanne waliwasili kwa lifti na kuingia njia ya ukumbini ambako chumba cha muhanga na chumba cha wauaji ndiko vilikokuwa kwa wakati huo, na watu walewale wanne walionekana wakiondoka baada ya mauaji kufanyika.

Shuguli ya usomaji ambayo ilifanyika katika vyumba vya milango ya kufuli za elektroniki za hoteli ilionyesha kwamba kulikuwa na jaribio lililofanywa kuvuruga programu ya kufuli la mlango wa elektroniki wa al-Mabhouh kwa wakati huo. Wachunguzi waliamini kwamba kufuli la elektroniki katika mlango wa al-Mabhouh huenda programu yake ilivurugwa na hivyo wauaji kuweza kuingia katika chumba chake kwa njia hiyo. Makufuli kama ya VingCard Locklink brand, yanaweza kuingiliwa na program zake kuvurugwa moja kwa moja kwenye mlango wa chumba cha hoteli.

Kwa mujibu wa Polisi wa Dubai, alifariki kwenye muda wa saa 3:00 usiku huo. Tarehe 20 Januari, mwaka 2010, siku iliyofuata, mfanya usafi wa hoteli alijaribu kuingia chumbani, lakini akakuta mlango umefungwa kutokea kwa ndani. Kisha mtu wa usalama wa hoteli aliitwa ili kuufungua mlango. Baada ya mlango kufunguliwa, mwili wa al-Mabhouh uligunduliwa kwenye kitanda. Kwenye droo karibu ya kitanda, waliweka chupa ndogo ya dawa kuonyesha kana kwamba amekufa tu kifo cha kawada.

Pichani ni chumba kimojawapo cha hoteli ya Al Bustan Rotana Hotel, Dubai nchini United Arab Emirates.

Itaendelea sehemu ya tatu.

Maka Patrick Mwasomola,

Karakata,
Uwanja wa ndege,
Dar es salaam.
Tanzania.
 
KAMANDA MWANDAMIZI WA KIJESHI WA KUNDI LA HAMAS LA PALESTINA:

SEHEMU YA TATU:
UCHUNGUZI:

SABABU ZA KIFO:

Mwanzoni, mamlaka za Dubai ziliamini al-Mabhouh alikufa kifo cha kawaida. Fawzi Benomran, afisa wa Polisi wa Dubai, alisema, "Ilikuwa na maana kwamba ilionekana kama ni kifo cha kawaida tu kilichotokea usingizini." Iliwachukua siku 10 kwa Polisi wa Dubai kufikia uamuzi kwamba al-Mabhouh alikuwa ameuawa. Benomran alielezea sababu hasa ya kifo chake kama "mojawapo ya kesi ya kutatanisha" ambayo idara yake ilikuwa inakabiliana nayo.

Gazeti la Khaleej Times likimnukuu afisa mwandamizi wa Polisi ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema kwamba wauaji wanne waliojiziba sura waliipiga na shoti ya umeme miguu ya al-Mabhouh kabla ya kumkaba na kumziba na mto wa kulalia na kumfanya kukosa pumzi. Stori nyingine iliyoripotiwa na Uzi Mahnaimi ilisema kwamba timu yake ilimuua al-Mabhouh kwa kumdunga sindano ya dawa ya shambulio la moyo, kisha wakaendelea na kupiga picha nyaraka zake kabla ya kuondoka.

Familia ya Al-Mabhouh ilisema kwamba timu ya madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wake waligundua kwamba alikufa katika chumba chake hotelini baada ya kunyongwa na kupigwa na shoti nyingi za umeme kichwani, na sampuli za damu zilizochunguzwa na maabara moja ya Ufaransa zilithibitisha kuwa kupigwa na shoti ya umeme ndiko kulikosababisha kifo. Kwa mujibu wa wakala wa shirika la habari la Reuters, athari za sumu zilikutwa wakati wa uchunguzi wa maiti ya al Mabhouh. Mamlaka za Dubai zilisema uamuzi waliochukua ni kuwa hayo ni mauaji ya binadamu na walikuwa wanashirikiana na Idara ya Polisi ya Kimataifa ya Makosa ya jinai kuchunguza tukio hilo.

Ripoti za habari nyingine zilitoa sababu mbalimbali za kifo, ikiwemo kukabwa na mto wa kulalia na sumu. Katika mkutano na waandishi wa habari wa Kimataifa Jenerali Tamim, mkuu wa uchunguzi, alisema kuwa sababu hasa ya kifo bado hawajaweza kuithibitisha.

Hata hivyo, tarehe 1 Machi mwaka 2010, Polisi wa Dubai walisema kwamba wauaji walimlewesha kwanza na madawa.

Meja Jenerali Khamis Mattar al-Mazeina ambaye ni kama naibu Polisi kamanda wa Dubai alitoa taarifa za kifo cha al-Mabhouh baada ya kufanya uchunguzi wa kijasusi. Al -Mabhouh alichomwa sindano katika mguu wake na sumu ya succinylcholine, ambayo inalegeza kwa haraka misuli, na kuifanya ipooze . Inasababisha kupoteza ujuzi wa kupambana, lakini haifanyi kupoteza uwezo na kuwa hoi au kuzimia. Kisha al-Mabhouh akakabwa na kuzibwa pumzi na mto wa kulalia. Al Mazeina alisema "wauaji walitumia njia hii ili kusudi ionekane kwamba alikuwa kifo cha kawaida."

Chini ni picha za kamera za ulinzi za hoteli aliyouawa al-Mabhouh jijini Dubai, iliyotolewa na Idara ya Polisi ya Dubai.

Itaendelea sehemu ya nne.
 
MAUAJI YA MAHMOUD AL- MABHOUH:

KAMANDA MWANDAMIZI WA KIJESHI WA KUNDI LA HAMAS LA PALESTINA:

SEHEMU YA NNE:

WASHUKIWA:

Tunaendelea tena na simulizi kuhusu namna Kamanda wa kundi la Hamas la Palestina alivyouawa na Majasusi wa Mossad wa Israeli, hotelini jijini Dubai mwaka 2010.

Katika sehemu ya tatu tuliishia pale Meja Jenerali Khamis Mattar al-Mazeina ambaye ni kama naibu Polisi kamanda wa Dubai alipotoa taarifa za kifo cha al-Mabhouh baada ya kufanya uchunguzi wa kijasusi. Alisema Al -Mabhouh alichomwa sindano katika mguu wake na sumu ya succinylcholine, ambayo inalegeza kwa haraka misuli, na kuifanya ipooze . Inasababisha kupoteza ujuzi wa kupambana, lakini haifanyi kupoteza uwezo na kuwa hoi au kuzimia. Kisha al-Mabhouh akakabwa na kuzibwa pumzi na mto wa kulalia. All Mazeina alisema "wauaji walitumia njia hii ili kusudi ionekane kwamba alikuwa kifo cha kawaida."

Sasa tuendelee na simulizi hiikatika sehemu hii ya nne:

Mkuu wa Polisi wa Dubai, Luteni Jenerali Dahi Khalfan Tamim, alitangaza maamuzi yake ya mwanzo tarehe 18 Februari, mwaka 2010 kwamba, "Uchunguzi wetu umegundua kwamba Mossad walihusika na mauaji ya al-Mabhouh ... Kwa asilimia 99% kama siyo 100% kwamba Mossad wanasimama nyuma ya mauaji haya."

Baada ya kutambua majina na picha 11 za washukiwa, tarehe 20 Februari mwaka 2010, alisema jeshi lake lina ushahidi wa moja kwa moja wakiwahusisha moja kwa moja Mossad na mauaji, akaongeza kuwa mojawapo ya ushahidi mpya uliokuwepo ni mawasiliano ya simu miongoni mwa washukiwa wa mauaji.

Tarehe 24 Februari mwaka 2010, Polisi wa Dubai waliwatambua watu 15 zaidi kama washukiwa waliojihusisha pia na mauaji ya al-Mabhouh.

Kwa mujibu wa Mwandishi Uzi Mahnaimi, (Jasusi wa zamani wa Mosaad ) uamuzi wa kumuua al-Mabhouh uliidhinishwa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, baada ya kuwa ameshauriwa na Meir Dagan, Mkuu wa Mossad, katika mkutano uliofanyika mapema mwezi Januari mwaka 2010.

Baadaye mwezi Machi, mwaka 2010 Mkuu wa Polisi wa Dubai alisema "Sasa nina uhakika kabisa kuwa walikuwa ni Mossad," na akaenda mbali zaidi na kusema "Nimempelekea Mwendesha Mashtaka wa (Dubai) maombi ya kuwakamata (Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin) Netanyahu na Mkuu wa Mossad," kwa kuhusika na muji ya Mahmoud al-Mabhouh.

Polisi wa Dubai walisema wauaji walitumia muda mfupi sana emirate, wakiwasili siku moja kabla ya mauaji, wakamuua al-Mabhouh kati ya muda aliowasili saa 9:15 alasiri na saa 3 usiku ule, na mara moja wakaondoka nchini kabla hajagundulika kuwa ameuawa.

Utambulisho walioutumia washukiwa 11 uliwekwa hadharani.

Namba kamili ya washukiwa ilisimama kuwa 18, wote hao wakiwa wameingia nchini kwa kutumia hati za kusafiria za kugushi au hati za kusafiria za udanganyifu.

Polisi wa Dubai, ambao walisema kwamba wafanyakazi wao wa uwanja wa ndege walifundishwa na watu wa Ulaya namna ya kugundua nyaraka za kugushi walisema kwamba hati za kusafiria za Ulaya zilizotumika hazikuwa za kugushi.

Serikali za Uingereza, Canada, na Ireland walisema hati za kusafiria zilizozihusisha nchi zao majina yake, "ama yalipatikana kwa udanganyifu [au] ziligushiwa."

Hati zote zilizoibiwa zilikuwa kutoka katika nchi ambazo hazihitaji visa kuingia UAE (United Arab Emirates).

UNITED KINGDOM:

Hati sita za kusafiria zenye majina ya Paul John Keely, Stephan Daniel Hodes, Melvyn Adam Mildiner, Jonathan Louis Graham, James Leonard Clarke, na Michael Lawrence Barney, na hati nyingine sita za kusafiria zikiwa na majina ya Daniel Marc Schnur, Gabriella Barney, Roy Allan Cannon, Stephen Keith Drake, Mark Sklur, na Philip Carr.

Tarehe 24 May mwaka 2010, mshukiwa mwingine wa Uingereza jina lake lilitolewa- Mwingereza Christopher Lockwood. Ikaja baadaye kugundulika kuwa mshukiwa huyu aliiba kitambulisho cha mwanajeshi wa Israeli aliyeuawa katika vita ya Yom Kippur (Yom Kippur War).

JAMHURI YA IRELAND:

Hati tatu za kusafiria zenye majina ya Gail Folliard, Kevin Daveron, na Evan Dennings na nyingine tatu zenye majina ya Ivy Brinton, Anna Shauna Clasby, na Chester Halvey.

Idara ya Mambo ya Nchi za nje ya Ireland iilitangaza kwamba hati zote za kusafiria zilizotumiwa na washukiwa si halali na ilisema kwamba "ilishindwa kumtambua yeyote kati ya watu wale watatu kama ni mwananchi halisi wa Ireland".

Kwa mujibu wa idara hiyo, Ireland haikuwahi kutoa hati za kusafiria zenye majina hayo.

Wakati majina na sahihi zikiwa ni za kugushi, namba za kwenye hati za kusafiria zilikuwa halisi, na zilikuwa ni za raia wa Ireland.

Raia wanne kati ya watano walifuatwa na Idara ya Mambo ya Nje, ambao wote walikuwa wanaishi nchini Ireland; hakuna hata mmoja wao ambaye alisafiri kwenda Mashariki ya Kati, kupoteza hati zao za kusafiria au kuibiwa.

UFARANSA:

Hati moja ya kusafiria yenye jina la Peter Elvinger (inayohisiwa ilitumiwa na kiongozi wa wauaji, na mratibu wa mipango), kujumlisha na hati nyingine tatu zenye majina ya David Bernard LaPierre, Mélanie Heard, na Eric Rassineux.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ufaransa, hati ya kusafiria yenye jina la Elvinger haikuwa halali.

Serikali ya Ufaransa ilimuhoji Balozi wa Israel jijini Paris tahehe 18 Februari na Wizara ya Mambo ya Nje ilitoa taarifa kuelezea, "kusikitishwa kwao na uhuni, uongo na udanganyifu wa matumizi ya hati za utawala wa Ufaransa."

UJERUMANI:

Hati moja yenye jina la Michael Bodenheimer. Maofisa wa Ujerumani mwanzoni walisema kwamba namba ya hati ya kusaifiria waliyoipokea kutoka katika mamlaka za Dubai ni ama haikukamilika au haipo kabisa.

Baadaye, ikaja kugundulika kwamba hati hiyo ilikuwa halali.

Kwa mujibu wa Idara ya uchunguzi ya shirikisho la Ujerumani, mtu mmoja wa Israeli kwa jina la Michael Bodenheimer alipata uraia wa Ujerumani mwezi Juni mwaka 2008 baada ya kuwakilisha nyaraka za uhamiaji jijini Cologne kwa kutumia anuani ya kabla ya Vita vya Pili vya Dunia ya bibi na babu yake na cheti cha ndoa cha wazazi wake. Alieleza kwamba yeye ni raia wa Israeli na alitoa anuani yake kama "ofisi yake halisi" ya muda na kwamba aliinunua huko Herzliya (na mpaka kufikia tarehe 22 Februari ofisi hiyo ilikuwa haipo tena).

Michael Bodenheimer aliyekuwa anaishi nchini Israel na kumiliki uraia wa nchi mbili za Marekani na Israeli alisema hajui ni kwa jinsi gani kitambulisho chake kiliibwa. Mtu mmoja mwenye hati ya kusafiria yenye jina la kusafiria la Uri Brodsky alitiwa mbaroni huko Poland mapema mwezi Juni mwaka 2010. Alikuwa jijini Cologne na Michael Bodenheimer na Ujerumani ikaomba apelekwe nchini Ujerumani.

AUSTRALIA:

Hati tatu za kusafiria zanye majina ya Nicole Sandra Mccabe (ambaye kwa wakati huo alikuwa na mimba kubwa kwa mujibu wa mama yake), Adam Korman na Joshua Aaron Krycer.

Adam Marcus Korman, mwenye uraia wa Israeli na Australia ambaye alikuwa akiiishi nchini Israel, alisema kwamba alishtushwa na kukasirishwa kwamba kitambulisho chake kilikuwa kimeibwa. Kwa nyongeza, majina mengine matatu ni majina ya raia wa Israel. Jina la mtu mmoja aitwaye Joshua Krycer aliyekuwa anafanya kazi kwenye hospitali moja iliyoonekana ipo jijini Jerusalem.

Majina yaliyotumika katika hati za kusafiria za UK yalikuwa yanamilikiwa na washukiwa waliokuwa wanaishi nchini Israel na kuwa na umiliki wa nchi mbili (dual citizenships).

Uchambuzi wa mauaji hayo katika gazeti la Kiyahudi la Chronicle ulisema hivi, "ni kipande cha kwanza cha maelezo ya ukweli ambayo yanaiunganisha Israel na operesheni hiyo."

Kwa mujibu wa gazeti la Palestina la Palestine Chronicle Post, Mossad wanajulikana kwa kutumia vitambulisho vya Waisraeli wenye uraia wa nchi mbili.

Mwaka 1997, mawakala wawili wa Mossad wakisafiria hati za kusafiria za Canada wakiwa Waisrael wenye uraia wa nchi mbili walisafiri kwenda Amman Jordan katika jaribio la kuhusu kumuua kiongozi wa Hamas Khaled Meshaal.

Kwa mujibu wa mtu wa zamani wa katsa (katsa ni Jasusi wa Mossad aliye (field) ambaye kazi yake ni kutoa taarifa kwa Mossad na kufanya kazi ya uwakala wa ujasusi kwa niaba ya Mossad), Victor Ostrovsky, ambaye ni raia wa Canada, mwanzoni Mossad waliomba ruhusa kutumia hati za kusafiria zenye uraia wa nchi mbili kwa Waisrael, lakini "Ninaamini kwa kiasi fulani, waliacha kuomba."

Mkazi wa Jerusalem-ambaye ni raia wa Uingereza ambaye jina lake lilitumika katika moja ya hati za kusafiria aliliambia Shirika la habari la Reuters kwamba hakuwahi kwenda Dubai na hakuwa na mawasiliano yoyote na Mossad au mauaji. Alisema kwamba hakujua ni "kwa jinsi gani hii ilitokea au ni nani ambaye alichagua jina langu au kwa nini". Kwa nyongeza, Waisrael wengine watatu ambao majina yao yalitokea katika hati za kusafiria waliripoti katika runinga ya Israel, ya Israeli Channel 2 news kwamba hawakuwa wanaelewa tukio lile, na hawafanani kabisa na washukiwa wote.

Katika kuamkia kilele cha ugunduzi kwamba hati za kusafiria za Uingereza zilitumika kikamilifu katika operesheni ile, Idara ya UK ya Makosa Makubwa (Serious Organised Crime Agency) (SOCA) walianzisha uchunguzi wao binafsi kuhusiana na jambo hili, na wakapanga kuanza kuwahoji Waingereza wamiliki wa hati za kusafiria ambao vitambulisho vyao viliibiwa.

Ofisi ya Mashauri ya Kigeni ya Uingereza pia ilimuhoji Balozi wa Israel tarehe 18 Februari, mwaka 2010 ili awape maelezo kuhusiana na jambo hilo. Serikali ya UK ilikanusha madai kwamba Mossad waliwajulisha kuhusu kwamba hati zao za kusafiria zingetumika katika operesheni hiyo.

Picha 11 za washukiwa wa mauaji ziliongezwa kwa polisi wa kimataifa yaani Interpol kama orodha ya watu wanaotafutwa sana mnamo tarehe 18 Februari, mwaka 2010 pamoja na maelezo yakibainisha kwamba zimechapishwa toka ilipogundulika kuwa vitambulisho walivyokuwa navyo washukiwa vilikuwa vya kugushi.

Maofisa wa uwanja wa ndege wa Dubai walifanya vipimo kwa kuskani retina kwa washukiwa hao 11 wanaohisiwa kufanya mauaji walipoingia nchini na polisi wa Dubai walisema watachapisha vipimo hivyo vya skani na kuwakabidhi INTERPOL.

Mtandao wa habari wa YNetnews ulisema baadhi ya timu ya wauaji ilikimbilia nchini Iran baada ya mauaji.

Washukiwa kumi na saba walitumia kadi za MasterCards zilizotengenezwa na MetaBank ya Storm Lake, kutoka Iowa nchini Marekani lakini zikiwa zimetolewa na Payoneer Inc ambao ndiyo walitumika kununua tiketi zao katika nchi nyingine kabla hawajawasili Dubai. Credit cards nyingine zilionyesha kushirikiana na shirika la Uingereza la Nationwide Building Society, IDT Finance ya Gilbraltar, na benki ya Ujerumani ya Germany DZ Bank AG. Payoneer ni kampuni iliyoanzishwa na Israeli ambayo kwa sasa ipo jijini New York pamoja na ofisi za R&D na wafanyakazi wake wengi wakiwa jijini Tel Aviv, nchini Israel. Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Yuval Tal, ni mwanachama wa zamani wa vikosi maalumu vya ulinzi vya jeshi la Israeli (IDF Special Forces). Payoneer inamilikiwa na makampuni matatu ya mitaji: Greylock Partners, Carmel Ventures, na Crossbar Capital. Greylock, ambao wana ofisi nchini Marekani na Herzliya, nchini Israel, ilianzishwa na Moshe Mor, Kapteni afisa usalama wa zamani wa jeshi la Israeli. Carmel Ventures ni mfuko wa mtaji wa Israeli wenye makao yake huko Herzliya, Israel. Unaendeshwa na Charlie Federman, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BRM, vilevile mfuko huo wa mtaji huko Herzliya pia ulianzishwa kwa pamoja na Nir Barkat, Meya wa zamani wa Jerusalem. Makao Makuu ya Mossad yanapatikana Herzliya.

Gazeti la New York Post mwanzoni liliripoti kwamba Tal alitoweka toka kampuni yake ilipogundulika kwamba ndiyo waliotoa baadhi ya credit cards kwa wauaji, huku majirani zake wa Brookly wakiwaambia polisi wa New York, New York Police Department (NYPD) kwamba ameondoka nchini humo. Hata hivyo alionekana tena siku moja baadaye.

Polisi wa Dubai walipata vipimo vya DNA kutoka kwa mmoja wa watu hao na baadhi ya alama za vidole kutoka kwa mtu mwingine ambaye ni mshukiwa. Mkuu wa Polisi wa Dubai Luteni Jenerali Dhahi Khalfan Tamim alisema kwamba kuna mkanda wa video wa saa 648 ambao washukiwa 27 wanaonekana na kutangaza kwamba polisi wamefanikiwa kupata vipimo vya DNA vya washukiwa.

Pichani chini ni video ya wanachama wa kundi la Hamas wakiadhimisha miaka kumi toka kuuawa kwa al-Mabhouh hotelini jijini Dubai mwaka 2010.

Itaendelea sehemu ya tano.
 
MAUAJI YA MAHMOUD AL- MABHOUH:

KAMANDA MWANDAMIZI WA KIJESHI WA KUNDI LA HAMAS LA PALESTINA:

SEHEMU YA TANO:

KUKAMATWA KWA WASHUKIWA:

Wapalestina wawili, Ahmad Hasnin, mratibu wa usalama wa Fatah-iliyokuwa inatawala mamlaka ya Palestina (Palestinian Authority) (PA), na Anwar Shekhaiber, mwajiriwa wa mamlaka ya Palestina (PA) huko Ramallah, walitiwa mbaroni nchini Jordan na kukabidhiwa Dubai kama washukiwa washiriki wa mauaji, wakishukiwa kuwa walitoa msaada wa kilojistiki kama vile kutoa magari ya kukodi na booking za hoteli.

Hamas walidai kwamba kutiwa kwao mbaroni kwa watu hao ni uthibitisho wa kuiunganisha mamlaka ya Palestina (Palestinian Authority) na mauaji hayo, wakati Mamlaka ya Palestina "waliwaka" wakiwalaumu Wapalestina hao waliokamatwa kuwa ni wanachama wa Hamas.

Watu wawili hao iliripotiwa kuwa walikuwa na uhusiano miongoni mwao na waliwahi kuishi Gaza mpaka pale Hamas waliposhika mamlaka kamili ya kumiliki Ukanda wa Gaza mwaka 20006. Mmoja alikwenda moja kwa moja Dubai, ambapo mwingine alijiunga naye baadaye baaada ya kuwa kwanza amekwenda Ramallah, ambako alihukumiwa kifo na mahakama ya Mamlaka ya Palestina, adhabu ambayo kiujumla ilipigwa chini na watu wanaoshirikiana Israeli. Kuandikishwa kwa Ahmad Hasnin na Mossad kutakuwa kulifanywa wakati alipofungwa kwa mwezi mmoja na Israel mwezi Juni mwaka 2007 kwa kujihusisha kwwake na kundi la Al Aqsa Martyrs' Brigades, tawi la kijeshi la Fatah. Alikwenda UAE mwaka 2008, kwa mujibu wa chanzo cha familia.

Mamlaka za Dubai zilisema mmoja wa Wapalestina hao aliyekuwa anashikiliwa alikutana na mshukiwa mmoja wa mauaji katika muda na sehemu isiyojulikana, wakati huyo wa pili ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu na yeye alikuwa tayari alishahukumiwa adhabu ya kifo na upande mmojawapo wa Palestina kati ya Hamas na Fatah. Mshukiwa wa pili alikuwa anatafutwa na Hamas. Wote wawili walishikiliwa ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu atawanyonga.

Ripoti ya Haaretz iliyoegemea kutoka katika taarifa ya chanzo kimoja kisichotajwa cha ubalozi wa nchi ya Kiarabu ulisema kwamba polisi wa Dubai waliiomba nchi ya Syria kumkamata Mohammed Nasser na watu wengine wa Hamas ili kuwahoji. Kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari, Nasser alikuwa Dubai siku kadhaa kabla mauaji ya al-Mabhouh hayajafanyika na alikuwa anajua ratiba yake na mahala atakapokuwa.

Mkuu wa Polisi wa Dubai Dahi Khalfan siku ya tarehe 3 mwezi Machi mwaka 2010 alisema amemuomba Mwendesha Mashtaka wa Dubai atoe hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Mkuu wa Mossad, Meir Dagan kwa mauaji.

Vilevile alitangaza kuwa Canada ilikuwa imemtia mbaroni mshukiwa ambaye "alikuwa mmoja wa kundi la watayarishaji ambao waliingia nchini na kuondoka kabla uhalifu haujafanyika." Mshukiwa iliripotiwa kwamba ni mmoja kati ya washukiwa ambao Intepol imetoa waraka wa kona nyekundu kwa niaba ya UAE. Hata hivyo siku iliyofuata Ubalozi wa Canada nchini UAE ulikanusha habari hii lakini ulisema kwamba unawasiliana na mamlaka nyumbani nchini Canada kuthibitisha hadhi ya kukamatwa kwa mtu huyo.

ALEXANDER VARIN aka ALEXANDER VERIN aka URI BRODSKY:

Tarehe 4 Juni mwaka 2010, Polisi wa Poland walimtia mbaroni mtu mmoja katika uwanja wa ndege jijini Warsaw akiwa amebeba hati ya kugushi ya kusafiria yenye jina la Uri Brodsky, ambaye alikuwa anatafutwa na mamlaka za Ujerumani. Hati ya Umoja wa Ulaya ya kukamatwa kwake kutoka Ujerumani ilionyesha kuwa Brodsky, aka Alexander Verin (au Varin), alikuwa "mshukiwa aliyejihusisha na njia haramu za kutoa hati ya kusafiria" ya [Ujerumani] kwa mtu mwingine aliyejulikana kama Michael Bodenheimer, ambaye anadhaniwa alishiriki katika mauaji ya Mahmoud al-Mabhouh. Mahakama ya Poland iliidhinisha kupelekwa Ujerumani kwa Brodsky tarehe 7 Julai, mwaka 2010 kwenda kusikiliza kesi iliyokuwa inamkabili. Hata hivyo, kupelekwa kwake kuliidhinishwa katika kile kilichosemwa kuwa Brodsky hatakabiliana na mashtaka ya Ujerumani kuhusu ujasusi – badala yake atakabiliana tu na mashtaka ya kujipatia nyaraka kwa njia za udanganyifu. Brodsky alisafirishwa kwenda Ujerumani chini ya ulinzi tarehe 12 Agosti, mwaka 2010 na kuachiwa kwa dhamana ya Euro €100,000 tarehe 13 Agosti, mwaka 2010 na kusafirishwa kwenda Israel tarehe 14 Agosti, mwaka 2010. Mwendesha Mashtaka wa Ujerumani alionyesha kwamba Brodsky hatakabiliwa na Mashtaka yoyote, lakini badala yake "suala hilo lingeweza kushugulikiwa kimaandishi," na kwa kiasi kikubwa matokeo yake ingekuwa kupigwa faini. Mwishoni mwa mwaka 2010, Ujerumani iliifuta kesi hiyo ya udanganyifu wa hati kwa kumpiga faini ya Euro €60,000; hata hivyo, hati ya Ujerumani kuhusu ujasusi ilibakia kuwa inafanya kazi.

KUKAMATWA KWA MSHUKIWA MKUU:

Tarehe 11 Oktoba mwaka 2010, gazeti la Taifa la Abu Dhabi lilichapisha mahojiano na Mkuu wa Polisi wa Dubai Luteni Jenerali Dahi Khalfan Tamim, ambapo katika mahojiano hayo alidai kwamba nchi moja ya Magharibi ilikuwa imemtia mbaroni kiongozi mkuu mshukiwa wa mauaji ya al-Mabhouh kama miezi miwili hivi iliyopita. Balozi wa nchi hiyo ya Magharibi alikuwa hataki kuitaja nchi hiyo na kutaja jina la mshukiwa aliyetiwa mbaroni. Tamim alielezea kuchanganyikiwa kwake na uhaba wa habari hizo: "Kwa nini kila wakati ambapo Israeli imekuwa ikijihusisha na uhalifu, kila mtu anakaa kimya? Tunataka kila mmoja anayejishugulisha na kesi hii kujihusisha nayo kama kesi inayohusu usalama, na siyo kuyapa kipaumbele mambo mengine tu.

Pichani chini, ni picha za washukiwa 26 ambao waligushi hati za kusafiria na kufanya udanganyifu na kuingia Dubai kutekeleza mauaji hayo mwezi Januari mwaka 2010, kama zilivyotolewa na mamlaka za Dubai mwaka huo.

Itaendelea sehemu ya sita.
 
Back
Top Bottom