Mauaji ya kutisha moshi

dm2000inter

Member
Oct 27, 2010
29
10
Naandika mwili ukitetemeka baada ya kushuhudia miili minne ya marehemu. Jamaa mmoja wa Mamba kokirie Moshi Vijijini,Macmilan Msami (49) amemchinja mama yake mzazi kama kuku kwa kutumia panga. Hakuishia hapo akawaendea watoto wake wawili Emanuel (9) na Ezekiel (12) akawachinja kwa tyle hiyo hiyo. Kisha akazikusanya maiti katika chumba kimoja akapiga usingizi hadi asubuhi. Dada yake alipofika akamkuta amekaa mlangoni anamuuliza vipi mama yupo akamjibu we ingia ndani ujionee mwenyewe. My God! ni maiti ndani ya madimbwi ya damu. Tukio hili si hadithi wala usifikiri unaota la hasha limetokea jana saa 2:00-4:00 usiku. Maiti zipo Kilema Hospital. Kibaya zaidi Wananchi wenye hasira kali nao wakamkamata jamaa wakamchinja na kuchoma moto mwili wake. Kafa na siri yake moyoni ya kiini cha kutekeleza unyama huu. Mungu aziweke roho za marehemu(si na ya muuaji) mahali pema peponi,Amen.
 
Mungu wangu hii ni bongo kweli? Ila sijasikia kwenye vyombo vya habari ngoja tucheki kesho manake najua magazeti mara nyingi yanapata tetesi hapa na kisha wanafuatilia ili waandike!
 
Mungu wangu hii ni bongo kweli? Ila sijasikia kwenye vyombo vya habari ngoja tucheki kesho manake najua magazeti mara nyingi yanapata tetesi hapa na kisha wanafuatilia ili waandike!
Kweli imetokea itv waliirusha ktk habari.
 
mkuu angalia usije ukatuhumiwa na wakubwa wa humu JF kuwa unachochea vita muraaa
 
Hapa ndipo ninapoamini kuwa watanzania ni wakatili sana ila wametulia tu.ona mauaji ya albino yalivyokuwa ya kinyama.
Nahofia sana yakitokea machafuko nchi hii, hapo ndipo tutakaposhuhudia unyama wa kutisha.
 
Watu wanasubiri tu chchem walete zao waone moto watu wamechoka na ahadi za kitoto!
Kaua hakupenda ni maisha magumu!!!
 
RIP marehemu.
Pamoja na yote nalaumu serikali kutowatendea haki wananchi wake, inatakiwa kuwapa elimu wananchi ili waweze kuwa na mbinu mbali mbali za kupambana na vikwazo vya maisha.
 
Back
Top Bottom