Mauaji ya kutisha mkoani Mbeya: Mwanamke akatwakatwa na mapanga, mwingine apigwa risasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya kutisha mkoani Mbeya: Mwanamke akatwakatwa na mapanga, mwingine apigwa risasi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 15, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  MAUAJI YA KUTISHA MKOANI MBEYA MWANAMKE AKATWAKATWA NA MAPANGA, MWINGINE APIGWA RISASI NA MMOJA ACHOMWA KISU CHA TUMBO  [​IMG]
  Mwili wa Marehemu Tabu Bakari Mwangela (58), ukiwa umeharibika vibaya baada ya kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika katika Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
  [​IMG]
  Ndugu wa marehemu wakilia baada ya kuuona mwili wake Tabu Bakari Mwangela (58), aliyeuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika katika Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  Waombolezaji katika msiba wa marehemu Tabu Bakari Mwangela (58), aliyeuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika katika Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
  ----

  Watu watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya kwa matukio matatu tofauti yaliyotokea Machi 7, mwaka huu likiwemo tukio la mtu kipigwa risasi, kukatwakatwa na mapanga na jingine la kuchomwa kisu tumboni.
  Tukio la kwanza limetokea Kijiji cha Kongoro Mswisi, Kata ya Mswisi ambapo mwananchi mmoja aitwaye Adam Jason Mwajeka (25), ameuawa kwa kupigwa risasi tumboni na watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi Februari 7, mwaka huu majira ya saa mbili usiku baada ya majambazi hao kuvamia baadhi ya maduka na kupora pesa za mauzo katika maduka kadhaa.
  Majambazi hao waliokuwa na silaha walianza kwa kumzuia mwanamke anayefahamika kwa jina la Tumpale Ally (32), ambaye ni mke wa Milele Kaponda kisha kumpora pesa za mauzo shilingi milioni 2 za kitanzania, mita chache kabla ya kuingia nyumbani kwake. Wakati wakibishana mwanamke huyo alimuita mumewe na alipojaribu kutoka kumsaidia, majambazi hao walifyatua risasi mbili hewani Tumpale aliachia pesa hizo kunusuru uhai wake.
  Haikuishia hapo majambazi hao walivamia duka la Leonard Edwin Mwampyate (34), na kupora pesa shilingi milioni tatu na laki tano, pamoja na simu ya mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi elfu themanini na tano, pia dukani alikuwepo nduguye Goliath Mwangonji ambaye walimwamuru kutoa pesa kutoka mfukoni ambapo walimpora shilingi lakini mbili na elfu ishirini.
  Aidha waliingia duka jingine linalomilikiwa na Bwaba Luka Mwasamaki na kupora shilingi elfu sabini na walipokuwa wakitoka, walimfyatulia risasi Adam Mwajeka tumboni na kufariki papohapo na katika harakati za kujiokoa Elimu Konga (32), alipigwa risasi ya mguu na majambazi hao wakapata nafasi ya kutokomea gizani.


  Miongoni mwa watu walionusurika katika tukio hilo ni pamoja na Diwani wa Kata hiyo Bwana Furgence Mhegele na Askari wa usalama wa barabarani aliyetayetambuliwa kwa jina moja la Salehe, na mazishi ya Adam yamefanyika kijijini hapo huku Bwana Eliamu amelwanzwa katika Hospitali ya Chimala Mission.
  Tukio la pili limetokea Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani hapa, Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Tabu Bakari Mwangela (58) ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika.
  Mwili wa marehemu umegunduliwa baada ya watu waliokuwa na ahadi ya kuuziana shamba kumsubiri kwa muda mrefu shambani kwake, ndipo walipoamua kumfuata nyumbani kwake na kukuta mlango ukiwa wazi, wakijua marehemu hayupo mbali ndipo walipomuuliza jirani yake aitwaye Devotha Jeremia, na kudai hafahamu alipo.


  Watu hao waliamua kugonga dirisha bila mafanikio yoyote na ndipo waligusa mwili wa marehemu kwa kwa kupitisha mkono dirishani na kuamua kumuita nduguye aitwaye Matrida Matiya (59), alipoingia nadni alikuta marehemu akiwa juu ya kitanda chake ndani ya chandarua na alipopenyeza mkono alikutana na damu kwenye kiganja na ndipo alipogungua kuwa nduguye kauawa.


  Bi Matrida alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Balaza la Kata Bwana Peter Elias Sankala, ambaye naye alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa Kijiji Ngumbushe Mwalyego na kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Igurusi ambao walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa mwili wa marehemu kwa kumtumia Daktari na kuukabidhi kwa ndugu na mazishi kufanyika kijijini hapo.Chanzo:H@ki Ngowi
   
 2. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  MBEYA, RUKWA, MARA, SHINYANGA ni mikoa yenye mambo ya ajabu ajabu sana, ebu cheji

  1. Kuchunana ngozi
  2. Kupigana nondo za vichwa
  3. Mauaji ya maalbino
  4. Mauaji ya vikongwe
  5. Mauaji ya wazee wenye macho mekundu
  6. Vita vya wenyewe kwa wenyewe Tarime

  Hivi hawa ni Watanzania kweli????
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mbona hujaisema Arusha ambako mauaji karibia kila siku, hao pia ni wa tz?
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Kwa KWELI INASIKITISHA SANA!!!!!!!!!!!!!!!!! Mimi SINA KAULI HAPA!!!!


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 5. Lussadam

  Lussadam JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 13, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 386
  Trophy Points: 180
  na pia hujaonesha Dar es salaam ambayo inaongoza kwa ufisadi ambao ni mbaya sawa au zaidi ya uliyoonesha hapo juu.??????
   
 6. PakiJinja

  PakiJinja JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Inasikitisha sana, hii ni kuashiria kuwa thamani ya vitu vitu/mali ni kubwa sana ukilinganisha na thamani ya utu/uhai.
  Hii ni tatizo kubwa hata Kenya pia ni hivyo.
  R. I. P nyote na mliofiwa poleni.
   
Loading...