Mauaji ya kutisha huko Dodoma na Tarime: Wawili wachinja wake zao na mwingine amuua mama yake

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Watu watatu wamefanya mauaji ya kutisha, wawili wamechinja wake zao, na mwingine amemuua mama yake.

Matukio ya Dodoma

Samson Joramu(44), mkazi wa Chololo, Kata ya Kikombo, alimchinja mke wake, Rehema Joram (43) kabla ya kujiua kwa kunyonga katika shamba lake.

Watu walioshuhudia walisema, Joramu baada ya kumuua mkewe alijinyonga na aliandika ujumbe uliokutwa mfukoni kwake, ukisomeka: “Mama tunza wanangu, mimi nimekufa.” Kadhalika aliandika orodha ya watu anaowadai.

Katika tukio jingine, Amos Kalenda, mkazi wa Kikombo, Dodoma anadaiwa kumuua mama yake mzazi, Joyce Kalenda kwa kumchinja. Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa ni mama huyo kumnyima chakula.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa akizungumzia tukio hilo alisema kuwa: “Ni kweli taarifa za vifo kutoka Kikombo ninazo, yule mmoja alimuua mama yake kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili jana (juzi), na huyu mwingine alimuua mke wake asubuhi ya leo (jana) kisha naye akajinyonga,” alisema.

Tukio la Tarime

Mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime, Wambura Mariba (50) mkazi wa Matongo, Nyamongo, Tarime, anadaiwa kumuua kwa kumchinja mkewe, Maria Wambura(40) kwa madai anamroga.

Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Andrew Satta alisema tukio hilo lilitokea Juni 8 saa tisa alasiri.

Satta alisema baada ya mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, alichoma moto nyumba zao mbili, zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi.

“Baada ya tukio hilo kutokea, wananchi walijichukulia sheria mkononi na kumjeruhi mtuhumiwa kichwani na kitu chenye ncha kali,”alisema Satta.

Wakizungumzia tukio hilo ndugu wa marehemu, Samwel Wambura alisema tukio la mwanamke huyo kuuawa, lilitekelezwa mbele ya watoto wake wakati akiwaandalia chakula.

“Alipomaliza kumuua, alianza kuandaa moto achome nyumba ili mwili wa mkewe uungulie ndani, majirani waliwahi kuuchukua mwili, lakini alianza kuwafukuza huku akiwa ameshika panga,” alisema na kuongeza: “Wananchi baada ya kuona tukio hilo walipiga simu kituo cha polisi ambao walifika na kumkamata mtuhumiwa.”

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto, Kagumiwa Kaijage alisema, alipokea mwili wa marehemu ukiwa umekatwa shingoni na mtuhumiwa amelazwa hospitali hapo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali mwilini.
 
Hahaha... Yaaan inabd ucheke kwa uzuni. Yaaan siku hizi kuchinja it's a normal thing. Huyo kamuua mama ake kisa chakula. Dah
 
Wangejua kwamba Baada ya Kuijua wanakuata uso kwa uso na Mungu,aiseee,wangeona bora wakae kwanza Duniani ili watubie.
Waliouwawa RIP
Na waliouwa na kujiua Mungu waongezee adhabu kali sana
 
Nilijua tu kuwa katika matukio yote lazima moja litokee tarime au mara kumbe kweli. R.I.P wote mliodhulumiwa nafsi.
 
Japo watu hawapendi ku-specify tabia za watu wa jamii fulani na maeneo husika ila ukweli ndo huo kila jamii ina tabia yake common, yani Mara kusikia matukio ya mauaji ni kitu cha kawaida mno plus Iringa , Dodoma. sijui tatizo ni nini. mbona Mtwara haisikiki katika matukio haya? dah watu wa huko wanahitaji elimu hakika.
 
Japo watu hawapendi ku-specify tabia za watu wa jamii fulani na maeneo husika ila ukweli ndo huo kila jamii ina tabia yake common, yani Mara kusikia matukio ya mauaji ni kitu cha kawaida mno plus Iringa , Dodoma. sijui tatizo ni nini. mbona Mtwara haisikiki katika matukio haya? dah watu wa huko wanahitaji elimu hakika.
Uliza yanayotokea mwanza uache kukalili kuua ni hukra ya mtu nasio mkoa wa mara pekee
 
Itungwe sheria kuhusu utaratibu wa kumiliki silaha za jadi na kucheki afya ya akili kila baada ya miezi sita.
 
Back
Top Bottom