Hossam
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 3,538
- 2,155
Huko Tengeru Arusha, Binti mmoja wa miaka 33 amemuua baba yake na kumcharanga kwa panga na shoka vipandevipande kisha akamdumbukiza katika choo cha shimo siku ya Jumapili iliyopita. Alifikia uamuzi huu baada ya baba huyo kumkatalia binti huyo kuuza sehemu ya shamba lao ili akanunue corolla. Baada ya kuhojiwa aliko baba yake, binti huyo alidai 'baba kenda samunge kupata kikombe', lakini majirani baada ya siku mbili tatu walishtushwa na harufu kali kutoka katika choo cha wanafamilia hao na kulazimika kuripoti polisi tukio hilo. Polisi na wanausalama walifika eneo hilo na kuanza kazi ya kukifumua na ndipo walipobahatika kuopoa mguu na mkono; kazi bado inaendelea.
Source: MATUKIO - WAPO FM
Source: MATUKIO - WAPO FM