Mauaji ya kinyama ya watoto karatu

Rwamuhuru

Member
Dec 22, 2010
50
0
Ni hali ya kusikitisha na isiyoaminika.

Mwanaume mmoja (jina nimeshindwa kulipata sawia) amefanya tukio la kinyama kwa kuua watoto wake wanne, 2 wa kike na 2 wa kiume kwa kuwanywesha sumu na kisha kuwakatakata kwa mapanga kabla ya yeye mwenyewe kujinyonga kwenye tukio hilo lilotokea jana

Jioni hii nilipita kwenye nyumba ambayo tukio hilo limetokea na inasemekana walikuwa na ugomvi na mkewe na siku ya jana kabla ya kufanya mauaji hayo alimpiga mkewe na kumng'ata kidole mpaka kukatika kisha akamkunja shingo kiasi cha mwanamke kupoteza fahamu kabla ya yeye mwanamke kuzinduka na kuaamua kukimbia na kwenda kijijini kwao.

Baada ya tukio hilo, inasemekana mwanaume aliamua kuwa hatataka kumuona tena huyo mwanamke wala uzao wake na aliamua kwa hasira kwenda kuchukua watoto wake (Mmoja mkubwa yuko darasa la 5 na anaefuatia inasemekana yuko darasa la 1 na wadogo wa mwisho ambao ni mapacha wako shule ya awali) na kuwatoa shule na kurudi nao nyumbani ambapo inaonekana mkubwa alishtuka baada ya kumuona baba yake hayuko vizuri na akaacha ujumbe wa maandishi kuwa kama watakufa basi ni baba yao.

Mnamo majira ya jioni jana inasemekana jamaa aliwawekea sumu watoto wake wote wa4 na kama haitoshi aliwaua wote kwa kuwakata na shoka (kama sio panga) na kisha kuwapanga kwa umri. Baada ya kutekeleza mauaji hayo aliamua kujiua na yeye mwenyewe.

Kilichofanya watu kushtuka ni kitendo cha ng'ombe wa baba muuaji kuonekana wakiranda nje usiku na majirani waliamua kwenda kujua ni nini kinaendelea na walipoona kimya waliamua kuvunja mlango na kuuona mwili wa baba muuaji na kuona nyumba nzima imetapakaa damu na walipoendelea kutafuta walikuta watoto wamewekwa kwenye chumba kingine wakiwa wamepangwa kwa umri

Kwa sasa mili wa watoto na baba yao muuaji iko sehemu ya kuhifadhia maiti na kesho ni mazishi ya watoto hawa.

Hakika ni tukio la kusikitisha na unyama wa hali ya juu dhidi ya watoto hawa wasiokuwa na hati ayoyote

 

:crying:
My, my, my....this is the sadest story i have heard this year
Hivi inakuwaje mtu anakuwa mkatili namna hii......no this is beyond human sense, there must be something behind the man

Hata kama ni ugomvi na mke, watoto hawa wanakosa gani jamani...hakika binadamu tumekuwa wabaya zaidi kuliko hapo awali

May you Rest in Peace kids....am standing a minute of silence to pay you my respect
 
Mungu Baba, hakika watoto hawa wameuawa kinyama. Wapumzike kwa amani....inocent creatures....
 
aisee insikitisha sana matukio ya namna hii yamezidi jamani kwanini lakini tumefikia huko watoto wa kuwazaa inauma sana rip watoto!!kweli vyombo husika vyote vikae chini na kuangalia tatizo ni nini!kila siku habari baba aua watoto!kweli inauma jamani!khaah
 
sijui ni ugumu wa maisha kwanini tumefikia mahali hata watoto wetu tunachinja kama kuku ukitazama ule utu na ubinadamu umepotea hii habari inasikitisha sana tumekuwa wanyama na zaidi ya wanyama wa mwituni
 
Mmmh! Nimebaki speechless kwa kweli. May they rest in peace maskini...!
 
oh lord have mercy on us! kwa kweli nimeumia sana juu ya hawa malaika wa mungu wasio na hatia. mungu awaweke pema peponi. amina.
 
Duh, very sad.

Mungu tusaidie viumbe wako tuwe na busara na hekima, uchaji kwako. Roho hizi zilale mahala pema.
 
Oooh! my god RIP watoto msio na hatia.ugomvi wa wanandoa unaadhiri sana watoto,serikali liangalieni hili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom