Mauaji ya kinyama tena - Ulanga, Morogoro!!!

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,225
WAKATI kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mwanza, Clement Mabina akiua naye kuuawa na wananchi kutokana na mgogoro wa ardhi, watu wengine watatu wameuawa na polisi jana, huku kituo cha polisi, baiskeli na gari vikichomwa moto katika mgogoro unaohusishwa na masuala ya ardhi katika Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro. Akizungumza na Tanzania Daima juu ya tukio hilo, Diwani wa Malinyi, Said Tira, alisema kilichosababisha mauaji hayo ya jana kilianza wiki moja nyuma, baada ya wafugaji kumuua mwananchi anayedaiwa kutoa taarifa polisi juu ya kuwapo kwa mifugo katika eneo lisiloruhusiwa.
Alisema baada ya wafugaji wanaodaiwa kuwa watatu kumuua mwananchi huyo, wananchi nao walijikusanya na kwenda kuchoma moto nyumba za wafugaji hali iliyosababisha askari kuwakamata.
Aliongeza kuwa katika hali hiyo wananchi walitaka kujua sababu za wafugaji walioua kuachiwa, huku wananchi waliochoma nyumba za wafugaji wakiendelea kukamatwa na kuwekwa rumande.
“Ni kweli hapa nipo katika eneo la tukio na nimewashuhudia wananchi watatu wakiwa wamefariki, mmoja amepigwa risasi ya kichwani mwingine kifuani na mwingine begani,” alisema Tira.
Alisema wakati wananchi walipokusanyika kutaka kujua sababu za wakulima kukamatwa na wafugaji kuachiwa, askari wa kituo cha Malinyi walianza kurusha risasi hewani na kisha kuelekeza kwa wananchi na kwamba risasi zilipowaishia ndipo wananchi wakavamia kituo na kuchoma baadhi ya mali zilizokuwepo kituoni na kuwatoa watuhumiwa waliokamatwa.
Alitaja baadhi ya vitu vilivyochomwa kuwa ni ofisi iliyo katika kituo cha polisi Malinyi, pikipiki, baiskeli pamoja na gari.
Polisi washindwa kutunza siri
Taarifa nyingine kutoka Malinyi zinaeleza kuwa baadhi ya polisi ndio chanzo cha tatizo hilo kutokana na kushindwa kutunza taarifa za siri walizopewa na wakulima juu ya kuwapo mifugo iliyofichwa katika baadhi ya maeneo.
Mtoa taarifa alieleza kuwa baada ya polisi wa Malinyi kupewa taarifa hizo walikutana na wafugaji na kuwataja watu waliotoa taarifa za siri ambapo wafugaji hao waliamua kuwavamia na kusababisha kifo cha mwananchi mmoja kabla ya tukio la jana.
“Kuna mwananchi alitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa licha ya zoezi hili la kuondoa mifugo kuonekana limekamilika, lakini bado kuna wafugaji wamehodhi mifugo mingi katika eneo lao. Jamaa wa usalama wakarejesha habari kwa wafugaji,” kilisema chanzo kingine kutoka Malinyi.
Alisema baada ya mauaji ya awali na wananchi kuamua kuchoma nyumba za wafugaji, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Francis Miti alienda Malinyi Igawa na kuongea na wafugaji kwa faragha kisha akawafuata wakazi wa Malinyi na kukemea hulka za kujichukulia sheria mikononi.
“Alipokuja DC akasema kwa kuwa kila upande umejichukulia sheria mkononi anaomba hali hiyo iishe na isijirudie, lakini jana akaleta askari na kuwakamata wananchi wanaohisiwa kumchoma moto mfugaji, hili jambo liliwaudhi wananchi,” aliongeza mkazi mwingine wa Malinyi.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga alipoulizwa juu ya tukio hilo, alikataa kuzungumza na kusema jambo lolote aulizwe Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro.
Hata alipoulizwa juu ya kuwapendelea wakulima katika suala hilo, Miti aliendelea kushikilia msimamo wake na kusema kama kuongea ataongea leo.
Kamanda wa Polisai Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile hakuweza kuzungumzia hali ya Malinyi baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokewa kwa muda mrefu.
Polisi Makao Makuu yatoa ufafanuzi
Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi, SSP Advera Senso, alisema chanzo cha mauaji hayo ni wananchi kukataa kutii amri halali ya polisi na kutaka kuvamia kituo kwa ajili ya kuwatoa watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Senso alisema tukio hilo lilitokea jana saa 3:00 asubuhi baada ya kundi la watu kutoka maeneo mbalimbali ya Malinyi kuvamia kituo cha polisi.
Senso alisema kutokana na tukio hilo, IGP Said Mwema ametuma timu maalumu inayoongozwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja kwa ajili ya kuongeza nguvu katika msako wa kuwakamata watu waliohusika na tukio hilo.
“Tukio hilo linaashiria vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani na limesababisha vifo, majeruhi na kujenga hofu miongoni mwa jamii, na sisi hatuwezi kuvumilia hali hii. Tutawakabili wote waliohusika na kuwafikisha katika mkono wa sheria,” alisema Senso.
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,160
1,250
Wakulima na wafugaji kama suala hili halitoshughulikiwa kuna makubwa zaidi mbele
 

mvunjamiwa

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
454
195
Inasikitisha sana. Hii haya mambo yataisha lini? Binafsi natazama kuwa ufugaji usiokuwa na utaratbu ndio chanzo cha haya yote. Ni ulimbukeni kuwa na mifugo mingi isiyoeleweka itakula wapi. Sera zetu juu ya ufugaji zinasemaje? Ikumbukwe kuwa ongezeko la idadi ya watu linaenda sambamba pia na ongezeko la mifugo lakini ardhi inabaki kuwa ni ile ile. Busara isipotumika katika kudhibiti ongezeko lisilo la lazima la mifugo ni hatari sana. Ulanga ni kati ya maeneo machche ambayo mimi naamini kuwa kuna ardhi nzuri yenye rutuba na inayofaa kwa kilimo. Kuwachanganya wakulima na wafugaji kunahitaji busara sana!
 

MZEE WA ROCK

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
622
195
eti utii bila shuruti. yaani haka kamsemo kananikela sana wao kushindwa kutunza siri ndio utii? kweri policcm tatizo katika hii nchi
 

nemasisi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
1,954
2,000
Serikali itenganishe wakulima na wafugaji hizi chuki zimeshafikia mahali pagumu sana kuzisuruhisha
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
Hivi vitu vina uzunisha sana mtu unaposoma haiwezekani kila mara watu tuwe tunasoma vitu vilevile kuhusu wakulima na wafugaji, ugomvi ule ule wenye madhara yaleyale. Na hapo utakuta chanzo kikubwa sio ardhi maana hiyo ni ya kumwaga kwetu sanasana ni maji.

Watanzania ni watu selfish sana at heart, maana hiwapo tunasema over 70 percent yetu sisi ni wakulima therefore lazima kero nyingi zipo maporini kuliko mijini, kuanzia elimu, miundombinu and the welfare of those who rely on farming. Sisi tumekazana na siasa maji taka za CDM na CCM zisizo na kichwa wala miguu zaidi ya watu kugombania mkate wakati si kwa ajili sahihi za kutafuta suluhisho la matatizo ya taifa.

Watu wanatakiwa kuwa wanasiasa kwa sababu ya kutatua matatizo makubwa ndani ya jamii, hiwapo mkulima kashindwa kuwezeshwa impact zake ni vijana kukimbia maisha hayo na kuja mijini ambapo hakuna sehemu za kuwaweka zaidi ya ku exhaust tu resources zilizopo na ndio nguzo za siasa za tanzania watu masikini, sijui amna ajira, mara umeme, mishahara; what about the needs of those 70%+ of us it is as if they dont count politically.

Vijiji vipo vilevile tangia sijui miaka gani there are no initiatives to improve the local infrastructure and adding resources huko to encourage local development and quality of life in those places hili mkulima nae ajivunie. Watu maskini ndani ya Tanzania hawana thamani kabisa apparently. Yaani mkulima ni mzuri kwa kupiga kura tu apart from that no one cares, sasa sijui tuna demand mabadiliko gani wakati over 70% of us, our needs are ignored and at times not mentioned at all wengine wanakwenda vijijini kwa madhumini ya kura tu, that is so pathetic.
 

KIJOME

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
3,085
1,225
Chagonjwa anakula posho tu kwenye matukio kama haya na hamna solution yoyote,faidini bhana mapolisisiem na madisisiem(mrishwa gamba a.k.a degrii za chupi)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom