Mauaji ya kikatili visiwa vya Ziwa Victoria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya kikatili visiwa vya Ziwa Victoria

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng`wanakidiku, Jul 9, 2009.

 1. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu wa JF leo nipo mwanza, na juzi nilibahatika kutemebele kisiwa kimojawapo katika ziwa victoria kiitwacho IJINGA.

  Miongoni mwa mambo niliyoyaona katika kisiwa hicho ni utulivu na hari ya hewa ya kuvutia ambayo kama ingekuwa kwa Dar basi pangekuwa na Mbezi Beach nyingi.

  Katika maongezi na wakazi wa kisiwa hicho amabacho kina utulivu mzuri nikaambiwa kuna kisiwa kimoja amboacho kipo ndani ya ziwa victoria kuna jamaa amejimilikisha kisiwa na huwa anaua mtu yeyote anayetofautiana naye na hajawahi kuchukuliwa hatua yoyote na wakazi wa hicho kisiwa wanahofu ya kutoa taarifa vyombo vya sheria wakihofia usalama wao.

  Sasa nimelimwaga hapa JF ili kama kuna waandishi wa habari basi watafute undani wa hili suala ili lianikwe kwa jamii na vyombo vya sheria vichukue mkondo wake.
   
 2. s

  smp143 Member

  #2
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ehh bwana....kuna kazi hapo.....
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hakika nakifahamu kisiwa cha IJINGA. hakika nilipokuwa Mkurugenzi wa mipango wa mkoa huo miaka ya mwishoni 80's vilikuwa mapori matupu kukiwa na watu wachache sana pale IJINGA na Igomwa.

  Niulizie kuna mzee mmoja maarufu sana IJINGA alikuwa anaitwa Mzee Kilala, ukibahatika kumuona mwambie rafikio Mwarabu aliekuwa mkurugenzi
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hicho kisiwa (kilichomilikiwa) kinaitwaje? Na huyo "jamaa" anaitwa nani (au hata kutaja jina lake ni siri)? Unaweza kupitia hapo Mwanza Central Police ukatoa hiyo taarifa au ukatafuta nambari ya kamanda wetu wa kinondoni (wa zamani) ukampigia moja kwa moja.

  Au wapatie hao watu wa IJINGA nambari hizi za police

  +255741328999 au +255741323999 au +255222194401 watoe taarifa na pia uwaambia siku hizi kuna kitu kinaitwa "Polisi Jamii"
   
 5. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Suala hapa ni namna ya kuanika haya mauaji sio kujitangazia umaarufu, any way, ebu tueleze utasaidiaje kuondoa haya mauaji au wewe ndiye uliyeyaanzisha
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kaitaba,
  kama umaarufu basi sasa mimi ni maarufu sana na nina ujiko sana sana ila
  Hakika amenikumbusha mbaaaaaaaaaali sana. naikumbuka sana Mwanza, nimei miss sana Mwanza.

  Haya Wabeja kulumba
   
 7. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #7
  Jul 9, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Muhimu ni jinsi ya kuwasaidia wenzetu kama we barubaru ulikuwaga konoka ijinga kipindi kile basi wape logic ya kule ili wajue pa kuanzia, msaada kwanza ujiko baadae.
   
Loading...