Simulizi: Mauaji ya Kifo

RIWAYA; MAUAJI YA KIFO.

NA; BAHATI MWAMBA.

SIMU; 0758573660.

SEHEMU YA NNE.

Willy alibaki kukodoa macho bila kujua aseme nini. Moja ya mambo ambayo kamwe hakupenda hata kuyasikia ni; kuwa siku moja ataiacha kambi ya jeshi na kurudi uraiani. Sasa kuyasikia maneno hayo kwa mtu yule asiyeeleweka, ilikuwa ni kama kuchomwa na ncha ya mshale utosini. Jasho la woga na majuto lilimtoka.

“Nakuomba kitu kimoja bwana mdogo” Kifo aliongea na kumtoa mawazoni. Aliinua kichwa chake na kumtazama.
“Chaza hoteli iko Dodoma na kwenye kibao cha kuhifadhia funguo, kuna ufunguo upo na hautumiki. Ufunguo huo ni namba 105. Hakikisha unaupata ufunguo huo, kisha follow the money” Aliongea kwa utulivu mkubwa na alimaanisha. Lakini maneno yake yalimwacha njia panda aliyeambiwa.

Midomo ilimwanguka tena kwa mshangao, maneno aliyoambia hakuyaelewa kabisa na hakujua kwa nini mtu yule alikuwa anamwambia habari zile. Maswali mengi yalipita kichwani mwake na aliamua kuchagua swali moja alilohisi ni sahihi kuliuliza wakati kama ule.
“Kwa hiyo unamaanisha nikiupata huo ufunguo, nitazifikia hizo pesa?” Aliuliza.

“Pesa!? Pesa zipi bwana mdogo!”

“Haah!” Ulikuwa ni mshangao wa karne kwa Willy Kondo. Kichwani mwake alijua tafsiri ya follow the money, ni fuata pesa kwa lugha ya kiswahili sasa vipi tena bwana yule aseme siyo pesa, wakati na ufunguo upo Chaza?

Aalah! Ajabu hii.

****
Wakati wakiwa bado wanaeleweshana kuhusu uwepo wao ndani ya pori, vishindo vya watu vilisikika vikija upande wao.

Wote kwa pamoja walinyamaza huku wakiwa makini kutizama upande wa njia. Dakika moja iliyofuata macho ya Willy yaliona kile ambacho hakukitarajia.
Alipita kijana mmoja aliyekuwa amevaa gwanda huku akiwa na bunduki yake mkononi, alikimbia huku akitizama nyuma mara kwa mara na wasiwasi mkubwa ulionekana usoni mwake.

Willy alitaka kukurupuka na kumfuata kwa nyuma, lakini Kifo aliwahi kumdaka na kumuonya asifanye hivyo.

Wakati wakiwa bado wanabishana, macho yao yalishuhuhudia mtu mwingine akiwa na bunduki mkononi mwake, akijaribu kumkimbiza kuruti yule ambae alikuwa amechoka na mbio pamoja na hofu ya kukimbizwa na mtu yule.

“Kwa nini unanizuia kujitokeza kumsaidia rafiki yangu?” Willy aliuliza kwa hofu.

“Nilikwambia tangu mwanzo huwezi kupambana na hawa watu, wako vizuri kila idara. Huyo uliyemuona anaitwa Cholo, anaua kama anakula karanga; haifai kukutana nae wakati huu.” Kifo alifafanua huku bado akiwa anatizama upande ambao walitokea wale watu waliokimbizana.

“Lakini tukiwa wawili tunaweza kumdhibiti na..”Willy hakumalizia kauli yake na alikatishwa na Kifo.

“Ukiona Cholo yuko nyuma ya adui, ujue Podo kapita upande mwingine kwa nia ya kumtangulia adui wao. Hivyo lazima wawe wawili wote kila umuonapo mmoja”

Machozi ya hofu yalimtoka Willy Kondo. Alilia kwa uchungu huku akijaribu kutafari na kujenga picha namna rafiki yake atakavyouwawa.

“Lakini kwa nini haya yote yanatokea?” Hatimae alimgeukia yule mtu aliyejiita kifo na kumuuliza.

“Unauliza humu porini au nje ya pori?”

“Popote!”
Kifo aliguna huku akitoa kadi aliyokuwa ameitoa kwenye kamera iliyokuwa shingoni mwake.

“Humu porini wanaitafuta hii kadi na hii kamera. Lakini kikubwa wananitafuta mimi.”

“Vina nini vitu hivi!?”

“utafute ufunguo namba 105 kisha, follow the money. Hakikisha follow the money.”

“Why follow the money?”
“Because it’s money”

Willy alimkodolea macho mtu yule, majibu yake hayakuwa wazi kabisa na hakuna aliloelewa na kila alipojaribu kuomba kueleweshwa, aliishia kuambulia fumbo juu ya fumbo.

“Kwa nini unanipa mafumbo kila ninapokuuliza?” Willy aliuliza na Kifo aliishia kutabasamu kisha na yeye aliuliza bila kujibu kile alichoulizwa.

“Kwa nini ulitaka kujiunga na jeshi…” Alinyamza kidogo huku akiirejesha ile kadi kwenye kamera na kuendelea kusema…

“ ulijiunga ili uajiriwe au ulijiunga ili kutumikia nchi yako?” Alimaliza na kusimama.

“Nilijiunga ili niipambanie nchi yangu kwa jasho na damu.” Willy alijibu.

“Basi fanya ninalokwambia. Pata ufunguo na follow the money, mimi nimepambania nchi yangu vya kutosha hadi sasa na ni zamu yako kuendeleza pale nilipoishia. Mimi ni kifo na kifo kipo karibu yangu ila wewe utanuka harufu yangu kila utakapoenda na…” Hakumalizia kauli yake, alibaki na mshangao wa karne.

Willy alichomoka kama risasi ya jangili aliyeona simba mbele yake, bila kutarajia. Alichomoka kama mshale kwenye filamu za kizungu. Willy alimkimbia Kifo.
Alikimbia kwa sababu ya kutomuelewa Kifo na habari zake, pia alitaka kuwahi kumsaidia rafiki yake. Aliamini mafunzo ya kijeshi yangelimsaidia kupambana na huyo mtu aliyeitwa Cholo ambae alikuwa anamkimbiza rafiki yake. Hakujua wengine walipatwa na nini huko walikokuwa, bali alitaka kwanza kumsaidia rafiki yake yule, kisha wajue walipo wenzao.

Kifo alitizama chini pale alipotoka Willy Kondo na alibaki akitisa kichwa kwa masikitiko makubwa, kisha aliamua kumfuata nyuma taratibu huku akiwa anapitia maumivu makali kutokana na jeraha lilokuwa tumboni mwake.

Alikimbia huku kamera ikiwa kifuani mwake na mkono wake wa kulia, ulikuwa umeshika upande ule wa jeraha, ambalo lilikuwa bado linatoa damu japo si kwa kiwango kikubwa kama mwanzo na, hiyo ilikuwa ni dalili mbaya kwake kwa maana damu ilikuwa imeanza kumuishia mwilini mwake.

Roho yake ilikubaliana na akili yake kuhusu mstakabali wa maisha yake, hakuona kama anamuda mrefu wa kuishi na hakujua ni vipi atakufa, lakini aliamini safari yake ingeliishia pale.

Licha ya kukiwaza kifo, lakini hakutaka kifo kimkute wakati ambao hajajua hatima ya Willy Kondo ndani ya pori lile kubwa na la kutisha.

Kukutana kwake na kijana yule aliona kama ni bahati ya mtende kuota jangwani. Lakini kuacha afe mikononi mwa Cholo na Podo ni kosa ambalo hakutaka litokee angali akiwa hai.

Alizidi kufuata njia ambayo aliona Willy akiipita na mbio zake za madenge.

***

Willy Kondo alikimbia kwa kasi akiwa na nia ya kumpoteza mtu yule aliyejiita Kifo. Aliamini atampoteza kwa sababu ya jeraha aliloliona mbavuni mwake na lisingeweza kumpa uwezo wa kukimbia kwa kasi kubwa kama aliyokuwa nayo yeye. Lakini pia alihitaji kuwahi kumuokoa rafiki yake ambae hakujua atakuwa amekutwa na kitu gani wakati huo.

Mbio zake zilimfikisha hadi kwenye sehemu ambayo alikutana na mlalo wa nyasi mbichi.

Alisimama na kuanza kuchunguza lile eneo kwa utulivu. Kitu kimoja alichogundua ni kuwa, eneo lile ulitokea mtifuoano wa mkubwa muda mfupi uliyopita. Alipochunguza aligundua kulikuwa na mburuzo wa kitu chenye kilo kadhaa. Aliamua kuufuata mburuzo huo. Hatua kadhaa mbele yake aliiona bunduki ikiwa imeanguka chini, hapo ndipo alipoikumbuka bunduki yake na alipojaribu kuiweka sawa alibaki akiwa ameachama kama mlevi.

Bega lake lilikuwa tupu hakukuwa na bunduki, aliiacha pale alipokuwa amejificha na yule mtu aliyejiita Kifo.

“Aisee!” Alishangaa huku akijishika kiuno chake, alikuwa amefanya kosa kubwa kuiacha bunduki yake. Si kujilinda tu, hata huko kambini ilikuwa ni kasheshe nyingine. Lilikuwa kosa juu ya kosa. Jasho la woga lilianza kumtoka kila sehemu ya kiungo chake, mikono ilitetemeka.

Macho yake yaliangukia pale ilipokuwa ile bunduki. Alipoitizama vizuri aligundua ilikuwa inafanana na ile aliyokuwa nayo yeye, zilitofautiana namba pekee.

Mapigo ya moyo wake yaliongeza kasi kuliko awali, kuikuta pale bunduki ya aina ile, ilimaanisha rafiki yake yuko matatizoni na ndiye aliyekuwa anaburuzwa.
Alijaribu kupiga hatua kwenda mbele, alijikuta anashindwa na alipojaribu kupiga kurudi nyuma, pia alishindwa.
Kichwani mwake aliwaza sifa za Cholo na Podo, hakika aliogopa.

Hakujua aende mbele au arudi nyuma, hakujua aokote bunduki ile ambayo haikuwa na risasi au afanye kitu gani.

Alibaki njia panda.
437579d25fbe7249e9605fb551675ba9.0.jpg
 
RIWAYA; MAUAJI YA KIFO.

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA TANO

Akili yake ilifanya kazi kwa kasi kubwa, alihitaji kufanya uamuzi sahihi bila kuathiri lolote. Akili yake ilifikiria kurudi nyuma na kuichukua silaha yake, kisha atokomee na kurudi kambini. Lakini alipomfikiria mtu aliyejiita Kifo, aliona si jambo jema kurudi kule na kukutana nae tena.

Alifikiria kuichukua silaha ile iliyokuwa imeachwa na rafiki yake, kisha akimbie na kurejea kambini, lakini alipokumbuka namba za silaha ile na namba za silaha yake havifanani, aliamua kugairi kuichukua na alibaki na uamuzi wa kwenda mbele kuufuatilia mburuzo uliyokuwa mbele yake.
Aliona kurudi nyuma ni kumdhalilisha mkufunzi wake, ambae aliwafundisha kusonga mbele bila kujali ukubwa wa vita inayopiganwa na; kurudi nyuma ni ishara ya kushindwa mapema kabla ya kujaribu kushinda.
Yeye aliamua kushinda na ujasiri ilikuwa ni silaha muhimu kuliko bunduki. Alihitaji kujua kilichomsibu mwenzake na ikibidi amuokoe au kufa wakiwa pamoja. Kurudi nyuma ni uoga ambao mwanajeshi hajawahi kuufikiria kirahisi na akirudi nyuma, kuna mbinu anazipanga.

Ujasiri ukamvaa na taratibu alianza kupiga hatua zake kuelekea mbele, huku akiufuata mburuzo aliyouona.

Alitembea zaidi ya hatua ishirini na, alipoanza kuzihesabu hatua nyingine zaidi; macho yake yaliona kibuyu cha maji kikiwa kimetelekezwa chini. Kibuyu kile kilikuwa sawa na kile kilichokuwa kiunoni mwake na, ilimaanisha kibuyu kile kilikuwa ni cha rafiki yake.
Midomo ilimtetemeka kwa hasira; kuikuta bunduki na kisha kibuyu, ilimaanisha usalama kwa rafiki yake ulikuwa ni asilimia chache kati ya nyingi za kudhurika. Haraka alianza kukimbia kuelekea mbele na kabla hata ya kumaliza mita ishirini, alikutana na kile ambacho alidhania japo hakukitarajia.

Mbele yake kulikuwa na mtu akiwa amelala chini na kuitanua miguu yake. Mtu yule alikuwa amelala kwenye dimbwi la lita zaidi ya tatu za damu,huku akiwa ametenganishwa kichwa na kiwiliwili chake.

Mtu yule alikuwa amechinjwa.

Willy alipiga magoti kwa unyonge huku machozi yakimtoka kwa wingi bila kupenda. Rafiki yake wa karibu alikuwa ameuwawa kikatili kwa kutenganishwa kichwa chake. Kilio cha kwikwi kilimtoka huku kamasi nyepesi zikiunda mifereji kuelekea kwenye papi za midomo yake.

Majuto yalimzonga huku akishindwa kuelewa ni hatua gani achukue kwa haraka ndani ya pori lile lenye mauza mauza ya kutisha.
Alijuta kwa sababu yeye ndiye aliyetoa wazo la wao kuingia porini na kutafuta maji, baada ya maji waliyopewa kuisha na wakizuiwa kunywa maji tena, kwa sababu walifanya mazoezi makali ya kukimbia na mazoezi mengine ya viungo, kabla ya kuingia kwenye uwanja wa ulengaji.

Kama si yeye basi pengine wangelikuwa salama na wakati huo wangelishaingia kambini na kuoga kisha kupumzika.

Kilio kisingeweza kuyapunguza machungu na majuto aliyokuwa nayo .

Alihitaji kutoka ndani ya msitu ule na kwenda kutoa taarifa kambini, huku akiwa tayari kwa adhabu yoyote huko kambini, lakini taarifa itoke na utaratibu mwingine ufanywe. Alikuwa tayari kwa lolote na kikubwa zaidi alitamani kuona msako kwa Podo na Cholo unafanyika, ili watiwe nguvuni kwa kile walichokuwa wamekifanya.

Alisimama kisha akayafuta machozi yake na kugeuka.

Lahaulal!!

Willy hakuwa peke yake, macho yake yalikutana na watu wawili wakiwa wanamtizana kwa macho ya chuki na dhihaka. Watu wale walikuwa na sura za kuogofya; macho makali na uso uliyojaa makovu makubwa. Mmoja alikuwa ni mkubwa wa mwili na kichwa kidogo mithili ya monjo. Mwili wake ulikuwa mkubwa kama mcheza mieleka maarufu kwa jina la Bigshaw. Mwingine alikuwa ni mrefu na mwili uliyojaa kimazoezi kama walinda milango kwenye kasino.
Mbali na ukubwa wa miili yao, mikononi mwao walibeba silaha aina ya Uzi12, silaha ambazo hazikuonekana kutumiwa na jeshi lolote hapa nchini.

Willy Kondo alitetemeka kwa uoga na kuanza kurudi nyuma. Kwa hofu iliyomjaa alisahau kiwiliwili cha rafiki yake kilichokuwa nyuma yake, badala yake alijikuta akijikwaa na kuanguka huku akipiga kelele za hamaniko, kisha alianza kusota chini kwa makalio yake.

Wakati akiendelea kurudi nyuma kwa nia ya kujiweka mbali na watu wale ambao hawakuonekana kuwa na nia njema, jitu lile lenye mwili mkubwa na kichwa kidogo kama monjo, lilianza kumfuata huku likikenua kinywa chake kilichogoma kuota meno. Jitu lile lilikuwa kibogoyo. Sura yake iliyokosa muonekano kamili kwa sababu ya kichwa kidogo, ilizidi kuonekana mbaya kwa sababu ya kinywa kukosa meno.
Jitu lile alilitambua kwa jina la Podo kwa sababu lilikuwa na sifa sawa na zile alizoambiwa na mtu aliyejiita Kifo.

Willy Kondo aliendelea kusota chini huku akijaribu kupapasa kitu chochote, ambacho kingeweza kumsaidia kujitetea mbele ya watu wale ambao, hawakuonekana kuwa na nia njema kwake.
Mkono wake wa kulia uligusa kipande cha mti, alikishika vizuri na kutulia huku akimtizama Podo alivyokuwa akimsogelea kwa hatua zake nzito.
Alimhesabia hatua kwa nia yakutaka kumshambulia, ili apate upenyo wa kutoroka mikononi mwa watu wale wabaya.

Podo alipomkaribia kwa haraka alijinyanyua chini kwa wepesi na kumtandika kichwani na kile kipande cha mti hadi kilivunjika.
Licha ya kipande cha mti kuvunjika, lakini Podo hakuonesha dalili ya kuingiwa na pigo lile la kushitukiza, badala yake alianza kucheka kwa dharau na kumdaka Willy kwa mikono yake yote miwili na kumnyanyua juu kama karatasi. Willy Kondo alijaa vema kwenye mikono imara ya Podo na, kila alipojaribu kufurukuta alishindwa na kubaki akilia kama mtoto mdogo aliyetishiwa na nyoka wa kuchonga.

Willy alizidi kufurukuta kwa kurusha miguu yake huku na huko, lakini mbavu zake zilibanwa nusu ya kuvunjika, kisha alitupwa chini kama jiwe la kuua nyoka. Alianguka chini na kusambaratika kama mlevi wa choya, huku akilia kwa uchungu.
Akiwa bado anajizoazoa chini, macho yake yaliona Cholo akimfuata kwa kasi na kumtandika teke zito usoni na kumpasua midomo yake. Alilia tena kwa uchungu uliyochanganyika na woga wa kuingia kwenye mikono ya wauaji.
Akili yake ilianza kumkumbuka Kifo ambaye alimuonya kuhusu watu wale wabaya. Lakini hakuwa na la kufanya wakati huo ili kuwakimbia, hali ilizidi kuwa tete na tayari walimsogelea na kumweka katikati yao, kisha Cholo akatoa kisu kutoka kwenye soksi za miguu yake na kwenda kukiweka shingoni mwake. Willy alitumbua macho huku akihema kwa shida, mwili ulimtetemeka huku akilini akijenga picha ya kutenganishwa kichwa chake na kiwiliwili.

Mikono ya Cholo iligawana majukumu; mkono wa kushoto ulimziba mdomo Willy huku mkono wa kulia ukitafuta shabaha ya kuinasa shingo ya Willy. Podo nae hakuwa nyuma kuitumia mikono yake kuidhibiti miguu na mikono ya Willy, ambae alikuwa akitapatapa kutaka kuinusuru roho yake.

“Usilie haiumi.” Cholo aliunguruma huku akimtizama kwa macho ya dhihaka.

“Unatekenywa tu hapo shingoni, usilie.” Podo nae alimwambia huku akizisukutua fizi zake kwa ulimi,huku mate yakimtoka kwa raha ya kutaka kuiona damu ya mtu inavyoruka.
Hakika maneno ya Kifo yalikuwa sahihi kuwaita majini watu.

Willy alilowesha suruali yake kwa mkojo, wakati kisu kilipoanza kuipekenyua ngozi ya shingo.

****

KWAKO MSOMAJI......

HITAJI LA RIWAYA HII LIMEKUWA KUBWA, HIVYO BASI, NAOMBA KWA YEYOTE ANAEHITAJI KITABU CHA RIWAYA HII, AWASILIANE NA MIMI KWA 0758573660, 0624155629... AU 0658564341WHATSAPP TU.

KITABU KITAUZWA KWA TSH 12000, LAKINI ATAKAE WAHI KUTOA ODA, ATAPEWA PUNGUZO HADI TSH 8000/= NA WALE WANAOTAKA KUNUNUA KWA SOFT COPY NI TSH 5000.

UNACHOTAKIWA KUFANYA UNAPOKUJA KUTOA ODA TANGULIZA MALIPO YA TSH 5000 ILI KUWE NA UHAKIKA WA ODA YAKO.
WANAOTAKA KUNUNUA SOFT COPY PIA UNATAKIWA KULIPA NA KUSUBIRI HADI MWISHO WA WIKI, AMBAPO NDIYO ITAKUWA MWISHO WA KUPOKEA ODA NA PESA YA SOFT COPY.

NB; KAMA KUNA MTU ANAHITAJI KUDHAMINI KOPI KADHAA UNAKARIBISHWA KWA MAZUNGUMZO.

KARIBUNI.....
a653e8736584abaea153ac18769f4210.0.jpg
 
Asante

KARIBUNI.....View attachment 1323725

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KITABU; MAUAJI YA KIFO.

DONDOO...

Mbio zake hazikuweza kumsidia kuondoa hofu
iliyomkumba, silaha yake mkononi haikufanya
kazi yoyote, zaidi ilimwongezea uzito kwenye
mikono yake.
Akiwa bado ni mwingi hofu na wasiwasi
katikati ya pori nene, ghafla anakutana na mtu
anaevuja damu kwenye ubavu wa kushoto.
Mtu yule alijiita Kifo.
Kifo nae alikuwa ni mwenye hofu kubwa, japo
alijitahidi kutoionesha mbele yake. Kukutana
na yule mtu mwenye kuvuja damu, hakukuwa
na msaada, bali kuliongeza tatizo lingine.
Tatizo ambalo liligarimu maisha ya watu wengi
kwa wakati mmoja, tatizo ambalo lilimfanya
akimbilie kila kona ya nchi, bila kupata
msaada.

Akiwa katikati ya matatizo, mara
anakumbuka neno la mwisho aliloambiwa na
mtu aliyejiita Kifo. Lilikuwa ni neno la mwisho
kabla ya Kifo hajakutwa na umauti.
Alikumbuka aliambiwa.. “FOLLOW THE
MONEY”
Je, Follow the money, ina maana gani
kwenye mkasa huu? Kwa nini mtu ajiite Kifo?
Ni mambo gani yalimkuta Willy Kondo; kabla
na baada ya kukutana na Kifo?

Fuatilia mkasa kwa kununua kitabu kwa bei ya tsh 10000/=, ujibiwe maswali yako yote.

Wasiliana na Mwandishi kwa simu 0758573660.
IMG_20200311_091907.jpg
 
Katika kambi ya Mafunzo ya Chaya, Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Walikuwa katika mafunzo maalum ya ulengaji shabaha. Maeneo ya kanda ya kati yanakabiliwa sana na uhaba wa mito ya maji. Hii inapelekea vijana watatu walio katika mafunzo hayo ya kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa, kufanya mpango wa kutoroka wakiwa mafunzoni ili wakatafute maji ya kunywa baada ya kuishiwa maji. Jua lilikuwa kali. Maji kidogo waliyopewa, yaliisha. Kiu kikali kiliwakamata huku mafunzo magumu yakiendelea. Mpango ulikuwa hivi; wakati mafunzo yanaendelea, watoroke wakatafute maji mtoni na kurudi haraka. Lakini vijana hawa baada ya kuingia katikati ya pori, nje kidogo ya kambi ya mafunzo wakitafuta mto, ndipo wanakutana na balaa wasilolitarajia. Wawili wanauawa kikatili (kwa kuchinjwa) Mmoja anaokolewa kwa bahati nasibu na Mtu wa huko porini anayejitambulisha kwa jina la Kifo. Huyu Kifo anampa siri nzito kijana wa JKT. Siri ambayo anajaribu kuifikisha kwa wakubwa wa Kambi ya Mafunzo. Je, watamwamini ilihali ana kesi ya kujibu ya kutoroka kambini? Mkuu wa mafunzo atachukua uamuzi gani kuthibitisha vijana wawili, walio katika mafunzo wamechinjwa msituni na watu wasiojulikana? Jambo hilo linapelekea mlolongo mrefu wa visa lukiki katika Riwaya hii ya MAUAJI YA KIFO toka kwa bahati Mwamba

Mauaji ya Kifo ni kitabu kilichojaa visa vya kusisimua, hujachelewa bado kinapatikana kwa gharama ya sh 10000 tu.

Kitabu cha MAUAJI YA KIFO, kinapatikana;

1:Kona ya riwaya Bookshop.

2: Come &readbookstore (0717978899). Hii iko Bunju.

3: Tabata (0718975659)

4:Lugarawa Bookshop (DODOMA),,, 0685097713.

Kwa tofauti na mikoa hiyo, mnaweza kuwasiliana na mwandishi kwa namba 0758573660, na kutumiwa kwa njia utakayopendekeza mteja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom