Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,888
Nina wasalimu wote kutokea Eldorest na ndiyo nimetokea eneo ambalo leo watu wameua kinyama na kuleta majonzi zaidi kisa na mkasa ukiwa ni Kibaki kurudi madarakani kwa mabavu.
Ni siku ya 3 sasa tangia matokeo yatangazwe na baadhi ya watu ama viongozi wamekuwa na kauli za haraka za kupongeza na kuondoa kauli kutokana na kitu wazungu wanaita revealation baada ya kura kutangazwa na Kibaki kutamkwa kwamba ni Rais na kukimia kula kiapo akiwa gizani .
Nimeshangaa hadi sasa si Tanzania wala Uganda majirani ambao wamesema neno lolote ama la kupongeza ama la kulaani yaliyo jiri Nchini Kenya . Wala si hata AU ila watu wa mabara mengine kama kawaida wanawasemea ama wanatusemea sisi weusi .
Najua mnataka kujua zaidi ni kitu nimekiona huko Eldoret nami sitasema kwa sasa ila nitasema baadaye kwa sasa nina haya moyoni mwangu kusema nanyi halafu nikimbilie kitandani maana hapa unalala unasikilizia .
Nimekuwa na hamu sana kusikia Rais wangu ndugu JK atasema nini lakini kama kawaida yake na kawaida ya Serikali yake yeye mambo makubwa na magumu huwa wanaamua kuwa bubu hii ndiyo kasi yao . Lakini pia nimejiuliza kama anaamua kutoa tamko atasemaje ? Maana hawezi kusema watu ama polisi waache kuua watu Kenya kwa kuwa Tanzania pia polisi walisha ua watu na hata wakakimbilia Kenya nia afadhali wao Wakenya hawajakimbilia kwetu .
Akisema mzozo juu ya kura Wakenya watawakumbusha ambush yao huko Visiwani na kuwaacha Watanzania wamekufa na wengine hadi leo ni vilema . Maana hata picha ziko online za ukatili wa askari wetu walio ufanya kwa rais kisa wamesimama na kudai haki zao baada ya kupiga kura na kuporwa .
Sana sana JK na CCM wanaweza kuwa wanafurahia kuona watu wanavyo kufa kwa ku resist maana naamini kwamba soon or later CCM watalazimika kutumia njia hii hii kwa kuwa kila mara huwa wanakataa kidogo tu FFU wanamwagwa .
Nimeshangaa kabisa kwamba watu wanaotaka shirikisho wanalitaka liwe la aina gani.Maana kama hawawezi kuelezana ukweli kama sasa kuitana haraka na kusema hapana acheni watu wasife kubalini kufuta utaratibu kweli sisi ni wamoja wa kitu gani ? Umoja huu unanifanya sasa nihitimishe wasi wasi wangu kwamba ulikuwa ni na bado ni umoja wa kujikita madarakani zaidi kuliko umoja wa watu wa Afrika Mashariki na maendeleo yao .
Nasema tena JK unangoja nini kusema kitu ? Au ni kwa vile unajua kwamba aliyo yafanya Kibaki ndiyo CCM wamekuwa wakiyafanyika huko Zenji na hata bara kuiba kura ili kupata wabunge wengi Bungeni? Maana kuna ushahidi wa wazi kuanzia Bukoba hadi Musoma, Arumeru na hata Dar kwamba kura zilitangazwa kwa nguvu baada ya CCM kuwa imepigwa chini .Lakini kwa Tanzania haya yalisha pita na sasa nakuuliza JK utasema lolote na utasema nini ? Kwa usafi upi na nguvu ipi ?
Museveni kusema lolote na nadhani anafurahia kuona watu wanakufa maana yeye hata matembezi ya kawaida Kampala anatumia kifaru. Yeye sawa na CCM wamefanya watu wa Nchi hizi mbili kuwa ni mali yao binafsi na matokeo kama ya Kenya yanatishia usalama wao kesho .
Au mpo .Mpo wapi ? Mnangoja nini ? Mbona juzi Mbeki kapigwa chini na bado mambo yanaendelea kwa nini Kibaki na wengine ya ANC ?
Bado nauliza watu wa Afrika Mashariki viongozi wetu wako wapi ama hadi wazungu waseme ndipo nanyi muweze kusema ?
Naishia hapa nimechoka na majonzi mengi . Niliyo yaona nitayasema kesho lakini naomba msaada wa majibu yangu kama kweli manadhani JK anaweza kusema lolote na atasema nini na kw ausafi upi wa CCM yake .