Mauaji ya JF Kennedy - rais wa 35 wa USA : Namna yalivyotokea!

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Sehemu ya Kwanza.

John Fitzgerald Kennedy, aliyekuwa maarufu kama JFK au Bobby, alikuwa mwanasiasa wa Marekani aliyehudumu kama rais wa 35 wa USA kutoka mwaka 1961 hadi alipouawa mwishoni mwa mwaka wake wa tatu katika ofisi hiyo.
Aliuawa huko Dallas, Texas, US na kifo hicho kilitangazwa rasmi katika hospitali ya Parkland.
Alizaliwa: May 29,1917, Brookline, Massachusetts, huko Marekani.
Mke wake wa ndoa aliitwa Jacqueline Kennedy Onassis na walioana mwaka 1953 hadi 1963 JFK alipouawa..
Makamu wake wa rais alikuwa Lyndon B. Johnson kutoka mwaka 1961 hadi 1963.

Kuna nadharia nyingi sana za njama za jinsi JFK alivyouawa (conspiracy theories), mtu aliyemuua na sababu ya yeye kuuawa. Lakini ukipitia nadharia zote hizo utaona mapungufu makubwa. Na hata msimamo wa Serikali ya Marekani na vyombo vya usalama mpaka sasa kuwa Lee Harvey Oswald ndiye muuaji wa JFK pia una mapungufu makubwa.

Ni mpaka mwaka 2003 ambapo utata uliondolewa na mahojiano aliyofanya bwana James Files ambae kwa hakika ndiye muuaji wa JFK.
Kwenye mahojiano hayo ambayo yatafuata hapa utajionea mipangilio na matukio hatua kwa hatua jinsi JFK alivyouawa.

Mahojiano haya yalifanyika November 19, 2003 ndani ya magereza ya Stateville huko Joliet, Illinois.

Wahusika katika mahojiano haya ni;
1. James Files - muuaji aliyekiri kumpiga JFK risasi ya kichwa.
2. Pamela Ray - mtunzi wa vitabu na rafiki wa karibu wa James Files tangu mwaka 1999 - alipaswa kuwa katika mahojiano na James Files.
3. Jim Marrs - mtunzi wa vitabu na mtu ambaye Pamela Ray alikubali amuhoji James Files badala yake mwaka 2003.
4. Gary Beebe - mchukua video.
5. Mrs. French - mtu wa utawala katika magereza ya Stateville.
6. Wim Dankbaar - afsa mauzo mwenye asili ya Dutch.

Kuna kipande kidogo cha mwanzo cha mahojiano ambapo sintofahamu ilitokea baada ya timu ya mahojiano kufika kwenye mahojiano bila Pamela Ray.
Pamela Ray alikuwa mtu muhimu sana kwa Files maana kwanza alimwamini na pili yeye asingeweza kukubaliana mkataba wowote kisheria akiwa mfungwa hivyo alimtegemea sana Pamela kwenye mambo ya mikataba.

Ila baada ya Files kueleweshwa na kuona maandishi kutoka kwa Pamela yakimtaka amwamini Jim Marrs basi mahojiano yakaendelea kama ifuatavyo;

Jim Marrs - swali : kumbukumbu zako juu ya jinsi Joe West alivyowasiliana na wewe na ulichofikiria juu yake, zikoje?

James Files - jibu : Mara ya kwanza Joe West aliwasiliana na mimi hapa magereza nikiwa nimetembelewa na mgeni. Mshauri nasaha wa magereza akaja kwenye chumba cha wageni nilipokua na akasema anataka nitoke na nipige simu. Nikamwambia," Haiwezekani, niko hapa siku 365 za mwaka. Siwezi kumuacha mgeni wangu ili nikapige simu. Nikauliza,"nani anapiga simu?" . Akajibu,"Kuna mtu kutoka Texas anaitwa Joe West".
Nikamwambia," simjui huyo mtu. Mwambie, nitampigia kwa muda wangu, sio muda wake. Niko na ugeni. Usinisumbue nikiwa kwenye ugeni".

Siku iliyofuata walikuja wakanitoa kwenye sero yangu, wakaniteremsha chini kwenye ngazi; walikua wamening'iniza simu ikinisubiri. Nikampigia Joe West na kuongea nae. Nikamwambia : una dakika tatu (3) za kunishawishi kwanini niongee na wewe. Joe alipoanza kuongea, nikamwambia : Woo, usiendelee! Umegusa sehemu nyingi nyeti; hizi simu zote zinarekodiwa. Kila simu inayoingia na kutoka inarekodiwa. Kama una nia kiasi hicho ya kuongea na mimi, basi napendekeza uje unitembelee. Joe West akanitaka nimuweke kwenye orodha ya wageni. Na akaja kunitembelea.

Alitumia siku mbili kuongea na mimi. Siku ya kwanza wala sikutaka kuongelea suala la Kennedy. Tuliongelea michezo; hali ya hewa, kwa ujumla kuhusu jela, na vitu vya kawaida mpaka nikawa na amani na yeye.
Siku iliyofuata, baada ya kuwa nimetafakari hilo jambo usiku mzima, Joe alionekana kuwa mtu mzuri tu, nilimpenda Joe. Alikuwa na mvuto fulani juu yake. Siku iliyofuata tulikaa chini na tukawa 'serious' na kisha tukaanza kuongea.

Nikiwa kwenye chumba cha wageni na Joe. Wakanipa penseli na karatasi. Nikaichora Dealey Plaza yote, bila kunakili kwenye ramani, bila picha, bila chochote kuwepo, na nikamuelezea Joe wakati ule, kwasababu Joe alitaka kujua nilikuwa sehemu gani katika huo mchoro. Na nikasema: Nitaweka alama ya 'X' katika karatasi, kunitambulisha mimi, ila hii 'X' haitakuwa sehemu sahihi. Nikasema: muda sahihi ukifika, hapo nitaiweka 'X' pale inapopaswa kuwa

Itaendelea....
 
Tuendelee...

MAUAJI YA JF KENNEDY - RAIS WA 35 WA USA : NAMNA YALIVYOTOKEA

Sehemu ya Pili

Jim Marrs - swali: Ni nini ulichomwambia ambacho kilimfanya Joe ajue ulikuwa Dealey Plaza siku hiyo?

James Files - jibu: Oh, hata mimi nilimuuliza. Alisema kuwa kuna mtu alimtaarifu yeye kuwa nilikuwepo. Alisema ana chanzo kinachoaminika. Na sikuwa najua kwa muda mrefu hicho chanzo kilikuwa nani. Ilinichukua muda kidogo baadae kabla ya kugundua kuwa FBI walikuwa na taarifa za uwepo wangu kuanzia mwaka 1964. Kwasababu sikuwahi kujua kama kuna mtu yeyote aliyefahamu kuhusu mimi.

Ila Zack Shelton ( jasusi mstaafu wa FBI), kwa ninavyofahamu, na haya nayasema kutoka kwenye minon'gono ya hapa na pale, kwamba Zack ndiye ndiye aliyesema na kumpatia Joe West taarifa kuhusu mimi : kwamba nilikuwa Dealey Plaza.

Jim Marrs - swali: Hata mimi naelewa hivyo. Uliwahi kukiri kwa Joe West kuwa wewe ndio uliempiga risasi JFK?

Files - jibu: Hapana, sikuwahi kufanya hivyo

Jim Marrs - Toa tamko
Files - Sawa, suala lote ni kwamba, kama ilivyokua kwa Joe West ... Joe West alikufa. Alikufa bila kujua kua nilikua moja kati ya wapiga risasi pale Dealey Plaza siku hiyo. Joe West hakuwahi kujua kama nilikuwepo kwenye kile kilima chenye nyasi.

Swali : Una fikra zozote juu ya kifo chake? Unadhani kilikuwa cha kawaida?
Jibu: Joe West alienda kufanya upasuaji wa moyo. Na kufuatia niliyoambiwa na nilivyofahamu, kwamba upasuaji ulienda vizuri sana na alikuwa njiani kupona. Ila nikaambiwa kulitokea tatizo kwenye dawa zake, alipata 'allergy - mzio' iliyosababishwa na dawa au kitu kinachofanana na hicho. Ila kilimuua, dawa zilimuua. Miaka kadhaa iliyopita, labda mwaka na nusu, nilisikia kupitia chanzo kisicho rasmi, na sitataja huo upande ulioniletea hizo taarifa, walisema kwamba kuna mtu 'alicheza' na dawa za Joe na akapewa dawa zisizo sahihi. Kwasababu walitaka kumnyamazisha. Hayo pia ni mawazo ya mke wake.

Swali: Na kwanini walitaka kumnyamazisha?
Jibu: Tulikuwa.... sipaswi kusema hivyo, Joe West alifungua kesi mahakamani; alitaka kufukua mwili wa John F. Kennedy. Na hicho ndicho alikuwa akipambania. Na wakati huu nilipoongea na Joe West, nilimuelewesha kwamba John F. Kennedy alipigwa kichwani na risasi zenye zebaki - 'mercury', risasi ya kipekee. Na wakati huu nikamwelewesha kuwa anaweza kutumia hii kuishawishi mahakama imruhusu afukue huo mwili kwasababu bado kungekuwa na matone ya zebaki kwakuwa zebaki huwa haitoweki kabisa. Hiyo daima itakuwepo. Kwahivyo hicho ndicho Joe West alitaka kurudi nacho, ushahidi zaidi, na kuutumia huo kufukua mwili wa Kennedy. Kuangalia matone ya zebaki.

Swali: Na mahakama ilikubali kesi yake?Jibu: Mahakama ilikubali kesi yake. Ila alipokufa na kesi ikafa.

Swali: Unadhani kumbukumbu zako ni nzuri kama zilivyokuwa miaka kumi iliyopita?
Jibu : Hapana, sidhani hivyo, sio nzuri kiivyo. Kumbukumbu zangu kwa miaka kumi iliyopita zilikuwa makini zaidi kuliko zilivyo sasa. Na sio kwasababu nazeeka na kuwa dhaifu, ila ni hali ya magereza, hali tunamoishi. Maji yetu hapa, wakati watu wanapokuja hapa na nna hakika mmeshauriwa kutokunywa maji ya humu ndani na mnunue maji ya chupa.

Nimekuwa nikinywa haya maji kwa miaka kumi na mbili iliyopita yakiwa na radiamu (madini ya chuma yenye mionzi) ndani yake, na vivyo hivyo kwa kila mfungwa hapa. Hatukujua hali ya haya maji mpaka Oliver Stone alipokuja kutengeneza filamu hapa. Na wakati akitengeneza filamu hapa, tukaona wale watu wote kutoka kampuni ya filamu wakipitapita huku wamebeba chupa za maji. Hata maafisa waliokua wakifanya kazi hapa wakaingia wasiwasi na hapo ndipo tulipoanza kutafiti : haya maji sio mazuri kwa afya.

Jim Marrs : Kwa kuchomekea tu, unajua: Sodium fluoride ndiyo kemikali inayowekwa kwenye mfumo wa maji wa baadhi ya majiji. Hiyo ndiyo wa - Nazi walikua wanaweka kwenye mfumo wa maji wa zile kambi za mateso kutuliza hasira za kila mmoja.

James Files: Ndio, sawa, wanatulisha kemikali hizo hapa ili kututuliza na kweli wametutuliza tokea tumeingia kwenye 'lockdown' kwa miezi kumi na wakalichukua gereza na kuliendesha kwa taratibu zao kwa sasa. Na nina maanisha nikisema hapa mahali pana uthibiti wa hali ya juu hasa kwa sasa. Hakuna harakati yeyote hapa kwa sasa.

Itaendelea...
 
Tuendelee...

MAUAJI YA JF KENNEDY - RAIS WA 35 WA USA : NAMNA YALIVYOTOKEA

Sehemu ya Pili

Jim Marrs - swali: Ni nini ulichomwambia ambacho kilimfanya Joe ajue ulikuwa Dealey Plaza siku hiyo?

James Files - jibu: Oh, hata mimi nilimuuliza. Alisema kuwa kuna mtu alimtaarifu yeye kuwa nilikuwepo. Alisema ana chanzo kinachoaminika. Na sikuwa najua kwa muda mrefu hicho chanzo kilikuwa nani. Ilinichukua muda kidogo baadae kabla ya kugundua kuwa FBI walikuwa na taarifa za uwepo wangu kuanzia mwaka 1964. Kwasababu sikuwahi kujua kama kuna mtu yeyote aliyefahamu kuhusu mimi.

Ila Zack Shelton ( jasusi mstaafu wa FBI), kwa ninavyofahamu, na haya nayasema kutoka kwenye minon'gono ya hapa na pale, kwamba Zack ndiye ndiye aliyesema na kumpatia Joe West taarifa kuhusu mimi : kwamba nilikuwa Dealey Plaza.

Jim Marrs - swali: Hata mimi naelewa hivyo. Uliwahi kukiri kwa Joe West kuwa wewe ndio uliempiga risasi JFK?

Files - jibu: Hapana, sikuwahi kufanya hivyo

Jim Marrs - Toa tamko
Files - Sawa, suala lote ni kwamba, kama ilivyokua kwa Joe West ... Joe West alikufa. Alikufa bila kujua kua nilikua moja kati ya wapiga risasi pale Dealey Plaza siku hiyo. Joe West hakuwahi kujua kama nilikuwepo kwenye kile kilima chenye nyasi.

Swali : Una fikra zozote juu ya kifo chake? Unadhani kilikuwa cha kawaida?
Jibu: Joe West alienda kufanya upasuaji wa moyo. Na kufuatia niliyoambiwa na nilivyofahamu, kwamba upasuaji ulienda vizuri sana na alikuwa njiani kupona. Ila nikaambiwa kulitokea tatizo kwenye dawa zake, alipata 'allergy - mzio' iliyosababishwa na dawa au kitu kinachofanana na hicho. Ila kilimuua, dawa zilimuua. Miaka kadhaa iliyopita, labda mwaka na nusu, nilisikia kupitia chanzo kisicho rasmi, na sitataja huo upande ulioniletea hizo taarifa, walisema kwamba kuna mtu 'alicheza' na dawa za Joe na akapewa dawa zisizo sahihi. Kwasababu walitaka kumnyamazisha.

.... nitaendeleza sehemu hii muda mfupi ujao....
Nakufatilia mkuu, dondosha vitu
 
kwa mujibu wa aliyekuwa CIA chief huko congo miaka ya 1960, Kennedy ndiye alitoa ruhusa ya mauaji ya Lumumba
 
Sehemu ya Kwanza.

John Fitzgerald Kennedy, aliyekuwa maarufu kama JFK au Bobby, alikuwa mwanasiasa wa Marekani aliyehudumu kama rais wa 35 wa USA kutoka mwaka 1961 hadi alipouawa mwishoni mwa mwaka wake wa tatu katika ofisi hiyo.
Aliuawa huko Dallas, Texas, US na kifo hicho kilitangazwa rasmi katika hospitali ya Parkland.
Alizaliwa: May 29,1917, Brookline, Massachusetts, huko Marekani.
Mke wake wa ndoa aliitwa Jacqueline Kennedy Onassis na walioana mwaka 1953 hadi 1963 JFK alipouawa..
Makamu wake wa rais alikuwa Lyndon B. Johnson kutoka mwaka 1961 hadi 1963.

Kuna nadharia nyingi sana za njama za jinsi JFK alivyouawa (conspiracy theories), mtu aliyemuua na sababu ya yeye kuuawa. Lakini ukipitia nadharia zote hizo utaona mapungufu makubwa. Na hata msimamo wa Serikali ya Marekani na vyombo vya usalama mpaka sasa kuwa Lee Harvey Oswald ndiye muuaji wa JFK pia una mapungufu makubwa.

Ni mpaka mwaka 2003 ambapo utata uliondolewa na mahojiano aliyofanya bwana James Files ambae kwa hakika ndiye muuaji wa JFK.
Kwenye mahojiano hayo ambayo yatafuata hapa utajionea mipangilio na matukio hatua kwa hatua jinsi JFK alivyouawa.

Mahojiano haya yalifanyika November 19, 2003 ndani ya magereza ya Stateville huko Joliet, Illinois.

Wahusika katika mahojiano haya ni;
1. James Files - muuaji aliyekiri kumpiga JFK risasi ya kichwa.
2. Pamela Ray - mtunzi wa vitabu na rafiki wa karibu wa James Files tangu mwaka 1999 - alipaswa kuwa katika mahojiano na James Files.
3. Jim Marrs - mtunzi wa vitabu na mtu ambaye Pamela Ray alikubali amuhoji James Files badala yake mwaka 2003.
4. Gary Beebe - mchukua video.
5. Mrs. French - mtu wa utawala katika magereza ya Stateville.
6. Wim Dankbaar - afsa mauzo mwenye asili ya Dutch.

Kuna kipande kidogo cha mwanzo cha mahojiano ambapo sintofahamu ilitokea baada ya timu ya mahojiano kufika kwenye mahojiano bila Pamela Ray.
Pamela Ray alikuwa mtu muhimu sana kwa Files maana kwanza alimwamini na pili yeye asingeweza kukubaliana mkataba wowote kisheria akiwa mfungwa hivyo alimtegemea sana Pamela kwenye mambo ya mikataba.

Ila baada ya Files kueleweshwa na kuona maandishi kutoka kwa Pamela yakimtaka amwamini Jim Marrs basi mahojiano yakaendelea kama ifuatavyo;

Jim Marrs - swali : kumbukumbu zako juu ya jinsi Joe West alivyowasiliana na wewe na ulichofikiria juu yake, zikoje?

James Files - jibu : Mara ya kwanza Joe West aliwasiliana na mimi hapa magereza nikiwa nimetembelewa na mgeni. Mshauri nasaha wa magereza akaja kwenye chumba cha wageni nilipokua na akasema anataka nitoke na nipige simu. Nikamwambia," Haiwezekani, niko hapa siku 365 za mwaka. Siwezi kumuacha mgeni wangu ili nikapige simu. Nikauliza,"nani anapiga simu?" . Akajibu,"Kuna mtu kutoka Texas anaitwa Joe West".
Nikamwambia," simjui huyo mtu. Mwambie, nitampigia kwa muda wangu, sio muda wake. Niko na ugeni. Usinisumbue nikiwa kwenye ugeni".

Siku iliyofuata walikuja wakanitoa kwenye sero yangu, wakaniteremsha chini kwenye ngazi; walikua wamening'iniza simu ikinisubiri. Nikampigia Joe West na kuongea nae. Nikamwambia : una dakika tatu (3) za kunishawishi kwanini niongee na wewe. Joe alipoanza kuongea, nikamwambia : Woo, usiendelee! Umegusa sehemu nyingi nyeti; hizi simu zote zinarekodiwa. Kila simu inayoingia na kutoka inarekodiwa. Kama una nia kiasi hicho ya kuongea na mimi, basi napendekeza uje unitembelee. Joe West akanitaka nimuweke kwenye orodha ya wageni. Na akaja kunitembelea.

Alitumia siku mbili kuongea na mimi. Siku ya kwanza wala sikutaka kuongelea suala la Kennedy. Tuliongelea michezo; hali ya hewa, kwa ujumla kuhusu jela, na vitu vya kawaida mpaka nikawa na amani na yeye.
Siku iliyofuata, baada ya kuwa nimetafakari hilo jambo usiku mzima, Joe alionekana kuwa mtu mzuri tu, nilimpenda Joe. Alikuwa na mvuto fulani juu yake. Siku iliyofuata tulikaa chini na tukawa 'serious' na kisha tukaanza kuongea.

Nikiwa kwenye chumba cha wageni na Joe. Wakanipa penseli na karatasi. Nikaichora Dealey Plaza yote, bila kunakili kwenye ramani, bila picha, bila chochote kuwepo, na nikamuelezea Joe wakati ule, kwasababu Joe alitaka kujua nilikuwa sehemu gani katika huo mchoro. Na nikasema: Nitaweka alama ya 'X' katika karatasi, kunitambulisha mimi, ila hii 'X' haitakuwa sehemu sahihi. Nikasema: muda sahihi ukifika, hapo nitaiweka 'X' pale inapopaswa kuwa

Itaendelea....
Haya ni maamuzi ya Roman Catholic na Je suits.
 
Tuendelee...

MAUAJI YA JF KENNEDY - RAIS WA 35 WA USA: JINSI YALIVYOTOKEA

Sehemu ya tatu.

Jim Marrs - swali: Uliwahi kukutana na Oliver Stone moja kwa moja?
James Files - Jibu: Nimekutana na Oliver Stone mara tatu. Na kwa ushahidi nina karatasi ambayo Joe West, hapana -samahani, sio Joe West ila Bob Vernon alimsainisha Oliver Stone.

Sasa Bob Vernon alikuja baada ya dili la Joe West. Bob Vernon aliendelea pale Joe West alipoachia. Bob Vernon alikutana na Oliver Stone na akamsainisha mkataba ambapo walinitaka nishiriki kwenye filamu, ila nilikataa kufanya hivyo. Nilikutana na Oliver Stone mara tatu.

Swali: Na hukuwahi kumwambia simulizi yako?
Jibu: Hapana, sikuwahi kumwambia Oliver Stone simulizi yangu. Nilikataa kujadiliana hii simulizi na yeye na kama nilivyosema, nina nakala yenye sahihi ya Oliver Stone. Sahihi ya Bob Vernon ndiyo pekee inayoonyesha huo mkataba unahusu nini, kitu pekee kinachokosekana ni sahihi yangu, kwasababu kamwe nisingeweza kuweka sahihi hiyo karatasi kuwa mkataba.

Swali: Kwanini ilikuwa hivyo?
Jibu : Sikumpenda huyo jamaa.

Swali: Kesi ikawa imefungwa?
Jibu: Kesi ikafungwa! Na kama ukipenda, nitakuwa na furaha zaidi kukutumia nakala ya hiyo nyaraka. Na ina sahihi halisi ya Oliver Stone na sahihi ya Bob Vernon juu yake.

Jim Marrs: Vizuri, nina maswali kibao, unaelewa tunachokifanya hapa, tunafanya mahojiano haya mapya kukusaidia wewe na Pamela.
James Files: Sahihi.

Jim Marrs: Sasa turudi nyuma ili twende hatua moja baada ya nyingine, niambie simulizi yako tena. Rudi mpaka wakati ulipogundua kwa mara ya kwanza kulikuwa na njama za kumuua Kennedy na utupeleke mbele jinsi ilivyotokea.

James Files : Poa, mara ya kwanza nilipojua kuwa kuna chochote kinapangiliwa juu ya Kennedy. Oh, nilisikia minong'ono mingi sana, hakuna mtu alimpenda Kennedy, walitaka kumuua Kennedy, walitaka mauaji ya kisiasa. Walitaka kufanya kila kitu kwa huyo jamaa.

Swali: Wewe binafsi ulikuwa na hasira nae kiaina?
Jibu: Nilikuwa na hasira nae juu ya 'Bay of Pigs', ila sikulitilia hili mkazo sana mwanzoni, kwasababu unajua, kila mtu anaongea, mtu fulani akiudhiwa na mtu fulani na mara moja utasikia : Nitaenda kumuua huyu jamaa, nitaenda kumuua yule jamaa, woo, woo, woo, woo! Unajua, kubweka kwingi sana, kubweka kama mbwa wa jalalani.

Ila jioni hiyo nilikuwa nimekaa 'Harlo Grill', Nachezea mashine ya 'pinball'. Sio ile ya kuzungusha, ile yenye namba unayoweza kuchezea kamari, unaweka kama dola kumi halafu unacheza.

Na Charles Nicoletti akaingia. Mtu ambaye nilifanya nae kazi nyingi, mtu niliyemheshimu. Na akaingia chumba cha nyuma nilikokuweko, akasema : Jimmy tuondoke! Nikasema: Nitakuwa na wewe baada ya dakika moja! Akaizima mashine kisha akasema: Twende sasa! Jibu langu likawa: Ndio mkuu, Mr. Nicoletti!

Nilijua hakuwa kwenye hali ya kusubiri na kukaa pale. Akasema: Nataka kuongea na wewe. Nikatoka nje na tukaingia kwenye gari lake na tukaanza kutembea, na tulikuwa na tabia ya msingi ya kuto kukaa mahali kama restaurant, na kuongea, kujadili vitu kama hivi na watu wengi wakisikia.

Na tulipokua tukitembea na gari akaniambia: Tunaenda 'kumfanyizia' rafiki yako! Na nikasema: Yesu, amefanya ujinga gani tena? Kwasababu nilifikiri anamuongelea rafiki yangu mmoja mjini, alikuwa anaiba kwenye mashine za 'pinball' na mashine za kuuzia sigara; alikuwa na tabia ya kutumia heroin kila uchao. Alikuwa ni teja kabisa, unajua.

Walishampiga mara kadhaa na kumfanyia vitu vingine na kumtishia, ila hawakuwahi kufikiria kumuua. Chuck akanicheka na kusema," Hapana, sio huyo, Namuongelea Rais Kennedy, JFK". Nikamuangalia na kusema, "Nini?" Akasema, "JFK, mshkaji wako!"

Nikafikiri ananirusha roho... unajua, ananipa wakati mgumu. Alimjua JFK na alijua ni kiasi gani nilimchukia huyu mtu. Hivyo nikamuangalia na nikacheka. Nikasema: Sawa, ni vyema! Kwangu ni sawa! Sina pingamizi hapo! Na mpaka hapa nikawa ninawaza, unajua, alikuwa akinitania. Ila akawa 'serious' kuhusu hilo jambo. Na tukaanza kuongea na akasema,"
Nakutaka wewe upepese macho mjini, utafiti baadhi ya maeneo mjini" akasema," Unajua kila kitu vizuri. Uangalia hapo tutakapofanyia tukio, aina ya silaha tutakazohitaji na vitu vingine kama hivyo.

Na akasema: angemhusisha pia Johnny Roselli kwenye hili jambo. Nikasema kwangu ni poa, napenda kufanya kazi na Johnny; sina tatizo lolote na yeye. Na mwanzoni tulipangilia kufanyia tukio Chicago, ila watu fulani hawakupenda hilo wazo, hivyo tukaachana na huo mpango kama miezi sita kabla ya mauaji yenyewe kufanyika.

Itaendelea...
 
Tuendelee...

MAUAJI YA JF KENNEDY - RAIS WA 35 WA USA :NAMNA YALIVYOTOKEA

Sehemu ya nne.

Jim Marrs - swali: Ila wewe hukupaswa kuwa mpigaji wa risasi?
James Files - Jibu : Oh hapana, kamwe, sikuwa mpigaji wa risasi, nilikuwa.... acha tuseme hivi : Nilikuwa wa kufuata hiki, kufuata kile, kuokota hiki, kuokota kile, kuzunguka mitaani, kuendesha gari mitaani. Wakati Chuck alipoenda mahali fulani, nilikuwa nae kila wakati.

Swali : Uliwahi kuhisi kwa namna yeyote ile kwamba taasisi za kijasusi za USA zingeweza kuwa zimefahamu mpango wa Chicago?
Jibu : Hapana, sikuwahi kupata hisia kama hizo hata kidogo. Nilikuwa najua tu kwamba watu fulani wa ngazi za juu ndani ya mafia, hawakufurahia sana hilo wazo la kuwa na kitu kama hicho cha ukubwa huo kitokee kwenye ukumbi nyuma ya nyumba zao.

Kwasababu waligundua Bobby kweli angeteremka Chicago na wao tayari walikua na vita zao ndogo za wao kwa wao zikiendelea. Hivyo ikabidi tuamue sehemu nyingine ya kufanyia tukio, Sikua na wazo kwamba ingekuwa Texas, kwa wakati huo. Hili nilikuja kulitambua baadae.

Swali: Ni wakati gani ulikuja kutambua hilo?
Jibu : Vizuri, nataka kusema... nakadiria miezi miwili na nusu, miezi mitatu, labda minne, kabla ya mimi kufanya safari kwenda Texas ambapo walikua wakiongelea kuhusu sehemu hiyo. Kwasababu hawakujua ni wapi angeenda. Walikua wakitafuta maeneo ambayo angeenda. Ila wakati huo wakasikia kwamba kuna uwezekano kuwa angeenda Texas, ila hakukua na uhakika. Na sikwenda Texas mpaka hilo lilipohakikishwa.

Na...walikuwa wanadhania maeneo kadhaa, kulikua na New Orleans na sijui, kulikuwa na maeneo mengine aliyokuwa akitembelea. Ila ilipokuja kwenye maamuzi ya sehemu ya tukio, niliambiwa kulikua na maeneo waliyopangilia kufanya, watu wengine walikua wameruhusiwa na vitu kama hivyo, unajua, ni minong'ono tofauti tofauti unasikia. Ina uhakika kiasi gani, siwezi kusema.

Ila muda ulipowadia na tukajua itakuwa 'serious' na Chuck akanituma kwenda Texas, hapo ilikua ni wakati nilipoteremka kwenda Belmont Avenue, sehemu ya zamani walipokua wakitengeneza mashine za pinball. Nilikuwa na mahali pa kujificha pale, sehemu, chumba cha nyuma, na pote palikua pakimilikiwa na mafia, hata hizo mashine za pinball.

Nilikua nimeweka akiba ya silaha pale; tulikua tukizifanyia kazi nyingi pale. Ninaposema 'tulikuwa', namuongelea mtu anayeitwa Wolfman, ambaye kwa sasa amefariki, ila kwa wakati huo alikuwa yuko vizuri sana, kurekebisha na kuboresha silaha, kutengeneza risasi, chochote kilichohusu bastola na bunduki. Huyu jamaa alikuwa mtaalamu hasa. Aliweza kutengeneza vitu kwenye chumba chake cha ardhini, ambavyo hungeweza kuamini, kuanzia vipunguza sauti - silencers na vyote vinavyohusiana na silaha, alikuwa akifanya vyote kwaajili ya mafia.

Hivyo nikateremka hapo chini, nikachukua vitu tulivyohitaji. Na tulikuwa na gari moja ambayo Chuck alikua amenunua siku za karibuni, tayari nilishaweka kila kitu ndani ya gari, tulikuwa na sehemu za siri ndani ya gari. Na kila gari tulitokuwa nayo, hata kabla ya Chevy ya mwaka 1963, hata kwenye Ford ya mwaka 1961 ambayo tulikuwa nayo kabla ya hiyo mwaka 1962, tulikuwa na sehemu kwenye 'dash' ambazo ungeweza kufungua kwa chini na kuweka mabomu ya kurusha kwa mkono, bastola, chochote tulichohitaji. Nyuma ya viti vya nyuma tulikuwa na stendi za kuwekea bunduki. Tulikuwa na vitasa vya mlango ambavyo unaweza kuchomoa na kurudishia, tuliweka bastola na vitu vingine humo ndani. Chochote unachohitaji, ila kila wakati tulikuwa na gari ya kazi ikiwa tayari.

Swali : Hivyo, Wolfman alikusaidia kufanya nini?
Jibu : Wolfman, wakati nilipowasiliana naye baada ya yote haya kutokea, na hii ni miaka kadhaa baadae, hapa ni wakati nilikutana na Joe West na Joe West akawa amekuja kunitembelea, tuliongea na akaniomba : Unafikiri huyu mtu anayeitwa Wolfman anaweza kuongea na mimi? Na Joe akaniuliza kuwa jina lake la ukweli ni nani na nikamwambia : hilo sitaongelea ila nitampigia simu na nitaongea nae.

Hivyo nikampigia simu na nikamwambia nilikua kwenye mazungumzo na Joe West kutoka Texas, na akataka kujua Joe ni nani na nikamuelewesha kila kitu na nikamwambia : Joe anatamaani sana kufanya mahojiano na wewe. Sijampatia Joe West jina lako ila nimemwambia kwamba wewe ndiye uliyetengeneza zile risasi za kipekee. Alinitengezea risasi sita ambazo nilienda nazo Texas, zote zikiwa na zebaki - mercury ndani.
Nikasema : Anataka sana kuongea na wewe. Je utaongea nae? Na akasema: Atanirudia! Nitakujulisha. Akasema : Nataka kuangalia vitu vichache. Wiki iliyofuata Wolfman alikua amekufa.

Itaendelea...
 
Tuendelee...

MAUAJI YA JF KENNEDY - RAIS WA 35 WA USA : NAMNA YALIVYOTOKEA

Sehemu ya tano.

Jim Marrs - swali: Alikufaje?
James Files - jibu: Naamini alipata shambulio la moyo. Sijawahi kuwasiliana na mtu yeyote aliyekuwa karibu na Wolfman kutokea siku hiyo.

Swali: Nielezee kuhusu hizi risasi zenye zebaki- mercury. Unaweza kuzielezea?
Jibu : Vizuri, zilikuwa ni risasi za 22mm na alitoa vichwa vya risasi, akavitoboa kwa juu na 'drill' na na akatumia chupa ya dawa ya macho kunyunyuzia matone ya zebaki na akavirudishia kwa kutumia gundi. Hivi ni kivifanya vilipuke vikishapiga kwenye shabaha.

Swali : Sawa, sasa silaha zako ziko tayari, sasa elezea gari uliyotumia.
Jibu: Gari lilikuwa Chevy ya mwaka 1963 yenye milango ya mbele na ya nyuma -Burgundy. Chevy Impala.

Swali : Ilikuwa na sehemu za siri za kubebea silaha?
Jibu : Ee, ndiyo, tulikuwa na sehemu ya siri kwenye 'dash', tulikuwa na kiti cha nyuma ambacho unaweza kukitoa, na kufungua ka-mlango kwa chini, ukanyanyua hiyo sehemu ya nyuma. Tulitoa 'spring' nyuma ya viti vya nyuma na tukachomea box ngumu za chuma zenye stendi za kuwekea silaha.

Swali : Sawa, sasa una silaha zako, una risasi zako na una gari ya kazi tayari. Ilikuwaje baada ya hapo?
Jibu : Kidogo kabla sijaondoka, maelekezo ya mwisho Chuck aliniambia: Natala uondoke asubuhi sana. Alisema : Sitaki uendeshe gari usiku. Nakutaka uwe barabara kuu kukiwa na foleni kubwa ya magari mchana ambapo hamna mtu atakutilia shaka.

Swali : Rudi nyuma na unipe tarehe au hata makadirio.
Jibu : Sikumbuki tarehe ila niliteremka kule kama wiki moja kabla ya mauaji. Naweza kusema nilikuwa eneo la dallas siku tano kabla ya mauaji kufanyika.

Swali : Na nini ilikuwa sababu ya wewe kuwahi?
Jibu : Sababu ya kuwahi ilikuwa mimi kwenda Dallas, kuangalia kwa umakini eneo, kujua mitaa ambayo barabara zake haziendelei, vivukio vya reli, muda treni inapovuka. Tayari walishajua barabara msafara utakapopita, na walishahakikisha hilo na walitaka kujua kama kuna sehemu nyingine tamu zaidi.

Watu wengi walishaamua sehemu ya tukio, sio mimi niliyechagua Dealey Plaza, ila niliambiwa nihakiki eneo kwa karibu zaidi na nione kama nafikiri kuna eneo jingine tamu kuliko hilo. Na nilihakiki eneo lote ambalo msafara ungepita. Na wakati wote nilikuwa na Lee Harvey Oswald.

Swali: Sawa, hebu rudi nyuma kidogo, kama wiki moja kabla, nadhani ilikuwa jumatatu kwa kumbukumbu zangu?
Jibu : Sina hakika.

Jim Marrs : Sawa, ila ulitoka Chicago. Tuanzie hapo. Ulitoka Chicago na ukaenda...
James Files : Hapana, sikuondoka jumatatu. Niliondoka au Alhamisi au Ijumaa asubuhi, sijui ni siku ipi kati ya hizo ila nilikuwa Mesquite, Texas jumamosi asubuhi. Kwasababu wakati huo ndio Lee Harvey Oswald alikuja pale Motel ambapo nilikuwa. Nilifika pale Ijumaa. Sasa nina uhakika ilikuwa ijumaa nilipofika pale.

Swali : Ulimpigia mtu yeyote simu ulipofika Dallas?
Jibu : Nilipiga simu mbili nilipofika pale. Nilimpigia Charles Nicoletti; nikamwambia niko eneo la tukio na nikamwambia nilipofikia ili kama akitaka kunitafuta. Nikageuka na kupiga simu nyingine, nikampigia David Atlee Philips. Nilikuwa na namba ya kumpata, simu ikaunganishwa kwa David Philips na akajulishwa nilipo. Kwasababu sikumwambia kabla kwamba ninaenda Dallas, Texas.

Swali : Kwanini ulimpigia David Atlee Phillips?
Jibu : Kwasababu kila wakati alipaswa kujua mahali nilipo kwakuwa alikuwa mthibiti wangu?

Swali : Wa kazi gani?
Jibu : Shughuli za CIA , operesheni maalum au chochote ambacho kingepaswa kufanyika.

Swali : Ulilazimika kuwa unawasiliana nae?
Jibu : Wakati wote tulikuwa tukiwasiliana. Tulikuwa na namba za kupiga.

Swali : Nini kilifuata baada ya hapo?
Jibu : Alisema "asante", na hiyo inatosha. Hatukuwa na mazungumzo marefu kwenye simu ; Nilimwambia sehemu niliyokuwa. Na kupitia kwa David Atlee Phillips ndio njia pekee ambayo Lee Harvey Oswald angeweza kujua nilipokuwa. Kwasababu sikumpigia mtu mwingine. Nilipiga simu mbili tu.

Swali : Ulikuwa unakaa wapi?
Jibu : Nilifikia Lamplighter Inn, palepale Mesquite, Texas.

Itaendelea....
 
Back
Top Bottom