Mauaji ya Januari 26/27 , 2001 na Madai ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
*MAUAJI YA JANUARI 26/27 NA MADAI YA KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI

CUF- Chama Cha Wananchi
kinaendelea na Maandalizi ya Maadhimisho ya Mashujaa wa Chama waliouawa kinyama Januari 26 na 27 mwaka 2001. Kama tunavyokumbuka Mauaji makubwa na ya Kinyama yalifanywa na Utawala wa CCM tarehe hizo kutokana na Maandamano ya Amani ambayo ni zao la kubakwa kwa Demokrasia kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2000, hususan Zanzibar ambapo CUF- Chama Cha Wananchi kinaamini kilishinda Uchaguzi kwa nafasi ya Urais na kupata Viti vingi vya Uwakilishi. Chama kiliitisha Maandamano ambayo pamoja na malengo mengine, yalilenga kusisitiza Kupatikana kwa Tume Huru za Uchaguzi (kwa Jamhuri ya Muungano na kwa Zanzibar) na Katiba Mpya.

Maadhimisho haya mwaka huu yanabeba Uzito wa Kipekee kwa kuwa Chama kimetangaza Mapambano ya Kudai Katiba Mpya yenye Tume Huru ya Uchaguzi, jambo linaloonekana kuungwa mkono na Wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanasiasa na Viongozi wa Dini.

Kama Chama tumepanga kufanya Mambo Makubwa Januari 26 na 27 katika Kumbukizi ya Mauaji hayo ya Kinyama na Maandalizi yanaendelea Chama Taifa kwa kushirikiana na Viongozi wa Wilaya. Tutaadhimisha nchi nzima kwa Utaratibu tutakaotangaziana baadae.Kila mmoja wetu ajipange kushiriki kwa namna moja au nyingine.

Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi NI LAZIMA KWA SASA na Jukumu la kila Mtanzania mwenye Mapenzi* na *nchi yake kushiriki kwenye Mapambano haya .

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!

Eng . ** Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi
wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF
- Chama Cha Wananchi
Januari 20, 2021*
 
Nawaombeni mjitahidi kwanza kurekebisha mifumo na sera zenu, siku hizi tunawaona kama ccm b,hamna lolote.
 
CUF chama dola kimeshawatumia na sasa mpo kama toilet paper iliyotumika,huwezi kuitumia tena ila unaitupa pamoja na uchafu wake na ku flash.
 
CUF hamna mvuto, labda muongee na ccm wanaowatumia kueneza matarajio yenu. Tunaoamini upinzani tunawaona ni vibaraka tu.
 
Unakumbuka shuka kumekucha,mlijitia najisi wenyewe Kwa kujipendekeza Kwa maccm huko ikulu
 
Back
Top Bottom