Mauaji ya Evelyn Howells: Je alikuwa ni mama au balaa ya familia………? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Evelyn Howells: Je alikuwa ni mama au balaa ya familia………?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 17, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Ukweli ni kwamba hata Polisi walipofika katika eneo la tukio waliamini kwamba yule mama alikuwa ameuawa na majambazi. Kwani wakati mauaji yale yanafanyika mume wa yule mama alikuwa baa ya jirani na wenzake akicheza Darts, na watoto wake wawili Glenn aliyekuwa na umri wa miaka 15 na John aliyekuwa na umri wa miaka 14 walikuwa wametumwa na mama yao huyo kumtembeza mbwa wao.

  Kwa mujibu wa maelezo yao wakati wakihojiwa na polisi walisema kuwa walimkuta mama yao akiwa sakafuni amefariki huku damu ikivuja kichwani kwani alikuwa amepigwa na kitu kizito kichwani. Akizungumza na wandishi wa habari waliofika kwenye eneo la tukio askari wa upelelezi aliyejulikana kwa jina la Gary Heigh, alisema “Tunaamini kwamba, Bi Eve Howells alikuwa amekaa sebuleni akiwa amejipumzisha na ndipo wezi hao wa kuvizia walipoingia ndani kwa kutumia mlango wa nyuma ambao ulikuwa haujafungwa na kumkabili kwa nyuma na kumtwanga kwa nyundo au kitu kizito kichwani na kumuua kisha kuiba kiasi cha dola 150. Mtu huyo au watu hao waliohusika na mauaji hayo wangeweza kuchukuwa fedha hizo bila hata ya kuuwa, kwani ni kiasi kidogo sana cha fedha ukilinganisha na uhai wa mtu.”

  Naye mume wa marehemu, Injinia David Howells ambaye ameishi na mkewe kwa miaka 23 akiongea kwa majonzi juu ya kifo cha mkewe alisema, “hawa wanyama wameharibu maisha yangu kwani wamedhulumu uhai wa mke wangu kipenzi.” Alisema mume huyo wa marehemu, kisha akaendelea ……. “Naamini ni mtu wa hapa hapa mtaani ambaye analindwa na mtu Fulani au watu fulani. Najua natakiwa niwe jasiri ili kukabiliana na hali hii kwa ustawi wa familia yangu. Eve alikuwa ni mtu muhimu katika familia ambaye alikuwa akishiriki kikamilifu katika malezi ya familia kiasi kwamba itakuwa ni vigumu sana kwangu kuziba pengo aliloliacha.”Kulikuwa na simanzi katika eneo hilo kutokana na msiba huo uliowastua watu wengi, hususan marafiki, majirani zao na waalimu wenzie waliokuwa wakifanya kazi pamoja na Eve katika shule ya Newsome ambapo Eva alikuwa akifundisha historia na elimu ya dini.

  Akimzungumzia Eve mwalimu mkuu wa shule hiyo alisema……… “Nitamkumbuka mwalimu Eve kama mwalimu mahiri kati ya waalimu ninaofanya nao kazi, wanafunzi walikuwa wanajua namna ya kujiheshimu wawapo katika kipindi chake, licha ya hivyo alikuwa ni mahiri wa kuandaa vipindi na pia ufundishaji wake ulikuwa ni wa kuvutia na wenye kuchangamsha darasa. Alikuwa anajua namna ya kuliweka darasa katika kiwango cha juu cha ustaarabu.”Baada ya Polisi kufanya mahojiano na watu kadhaa, wakiwemo waalimu wenzie na marehemu na majirani zake, walikuja kugundua kwamba, pamoja na sifa nzuri alizomiminiwa kuwa ni mwalimu mzuri kwa watoto, hasa katika masomo yake ya Historia na Dini, lakini majirani zake walimwona kama mzazi mkali sana kwa familia yake. Ilielezwa kwamba, nyumba yake haikuwa na amani kwa sababu ukali wake.

  Maelezo yale yaliwafanya Polisi wakiongozwa na mpelelezi Carry Heigh ambaye alisoma shule moja na mume wa marehemu David Howells kuichunguza zaidi familia husika kuhusiana na kifo cha mama yule.

  Ukweli ni kwamba David Howells hakuhusika na mauaji hayo, kwani wakati mauaji yanatokea alikuwa kwenye baa ya jirani. Ukweli huo ulidhibitishwa na marafiki zake aliokuwa akinywa nao katika baa hiyo ambao walithibitisha kwamba hakuwahi kutoa mguu katika baa hiyo kwenda popote. Askari huyo wa upelelezi Detective Superintendent Haigh alijiwa na fikra kwamba kuna uwezekano mkubwa mtoto mmoja au wote wawili wa familia hiyo wamehusika kumpiga mama yao kwa kitu kizito na kumuua.

  Ni tukio lililotokea mnamo Agosti 31, 1995 katika mji mdogo wa Dalton nchini Uingereza ambapo mama mmoja aitwaye Evelyn Howells aliyekuwa na umri wa miaka 48 wakati huo, ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya sekondari ya Newsome, aliuawa kwa kupigwa na nyundo au kitu kizito kichwani.

  Mnamo saa moja za asubuhi ya Septemba 20 1995, watoto wa familia hiyo Glenn na John Howells walikamatwa na Polisi wakiwa nyumbani kwao. Baba yao aliwasindikiza hadi makao makuu ya Polisi ya Huddesfield ambapo walihojiwa wakiwa wametenganishwa. Walishikiliwa hadi siku iliyofuata ambapo walihojiwa tena.

  Maelezo yao yalitofautiana kuhusiana na tukio hilo la kuuawa kwa mama yao, hivyo hadi inafika jioni ya siku hiyo ya pili askari aliyekuwa akiongoza upelelezi wa kesi hiyo alianza kuamini kwamba, mmoja wao au wote watakuwa wamehusika na kumuua mama yao. Hata hivyo kutokana na kubanwa sana waliamua kusema ukweli.

  Glenn huku akitokwa na machozi alikiri kwamba ni yeye aliyemuua mama yake kwa kumpiga na nyundo kichwani kwa mapigo yapatayo kumi, baada ya mama yake kumuita ‘toto vivu na goigoi,’ kwa sababu hakumtembeza mbwa kama alivyomuagiza.

  Aliendelea kusema kwamba, mama yao aliigeuza maisha yake na ya familia kuwa kama jehanam. Baada ya kuelezwa juu ya kaka yake kukiri kuhusika na mauaji hayo, John naye alikiri kwamba, alimsaidia kaka yake kuivuruga nyumba yao ili ionekane kama ilivamiwa na wezi na pia kuficha silaha iliyotmika katika mauaji hayo. Watoto hao walishitakiwa kwa makosa ya mauaji na kuwekwa katika selo tofauti.Askari aliyekuwa akiongoza upelelezi wa kesi hiyo Detective Superintendent Gary Haigh aliridhika kwamba watoto wale walihusika na mauaji yale , lakini alipata wasiwasi kwamba huenda na baba yao atakuwa amehusika kwa njia moja ama nyingine. Kwa jinsi alivyozidi kuchimba zaidi juu ya maisha ya familia ya ndoa ya David Howells na mke wake, haraka sana alibaini sababu ambayo ingemfanya hata Howells atake mkewe afe.

  Kwanza ilikuwa ni marupurupu ya mkewe ambayo angenufaika nayo. Eve Howells alikuwa na akiba na pia aliwekeza kiasi cha dola 200,000, ukijumlisha na jina lake kuwepo katika orodha ya watakaonufaika na mirathi ya familia yao. Lakini pia kulikuwa na taarifa zilizothibitishwa pasi na shaka kwamba Eve alikuwa na uhusiano nje ya ndoa na rafiki wa karibu kabisa na mumewe aitwae Russell Hirst, uhusiano ambao umedumu kwa takriban miaka 12.

  Licha ya hivyo pia katika maelezo yaliyotolewa na mtoto John Howells wakati akihojiwa na Polisi alidai kwamba mama yao alikuwa akiiendesha familia hiyo kwa mkono wa chuma, na kwa miaka mingi mama huyo aligeyageuza maisha yao kuwa kama jehanam. Hivyo David Howells hakutaka kuendelea kuishi na mke wake, lakini hakuwa na namna ya kumuacha.

  Kwa hiyo Askari huyo wa upelelezi Detective Superintendent Gary Haigh alihitimisha fikra zake kwa kuamini kwamba, njia pekee iliyofikiwa na Howells ni kuwashawishi watoto wake wamuue mama yao wakati yeye akiwa ametengeneza mazingira ya kutokuwepo katika eneo la tukio (Alibi) kwa kutoka na kwenda baa kucheza mchezo wa dats na marafiki zake.

  Mnamo Octoba 19, 1995, David Howells alikamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya kula njama na wanae John na Glenn ili wamuue mama yao. Askari wa upelelezi Detective Superintendent Gary Haigh alijua wazi kwamba bila ushirikiano kutoka kwa watoto wake kumhusisha baba yao kuwa alishiriki katika mpango wa mauaji, basi kesi dhidi ya David Howells isingekuwa na ushahidi wa kina kumtia hatiani.Hivyo alipanga kwa ustadi mbinu ya kupata ushahidi wa kumtiani David Howells kwa kumruhusu kukutana na wanae akiwa hapo selo na kumtegea kifaa cha kurekodia mazungumzo yake na wanae pale selo bila yeye kujua.

  Kesi ya David Howells na wanae ilianza kusikilizwa mnamo January 16, 1997 ukiwa ni miezi 18 tangu wakamatwe. Wote walikanusha mashitaka. Mwanasheria Gary Burrell aliyesimama kama wakili wa Glenn Howells aliyekiri kosa la kuhusika na mauaji ya mama yake kwa kisingizio kwamba alitekeleza mauaji hayo kutokana na kushikwa na hasira zilizopitiliza. Alisema kwamba watoto wale waliteswa sana na kwa kipindi kirefu kiasi cha kuathirika kiakili na kisaikolojia.

  Mwanasheria huyo aliendelea kuieleza mahakama jinsi mama huyo alivyokuwa akiwafanyia watoto hao ugaidi kwa miaka mingi na alikwenda mbali zaidi ambapo alifikia hatua ya kufunga jokofu na kufuli ili kuwazuia watoto hao kula kitu chochote kilichohifadhiwa humo bila ridhaa yake. Glenn aliieleza mahakama kwamba alikasirika kupita kiasi sana kutokana na maneno ya kuudhi aliyoambiwa na mama yake.

  Mwendesha mashitaka wa serikali Franz Muller, aliieleza mahakama jinsi mauaji hayo yalivyopangwa kwa makini na ustadi mkubwa na watu hao watatu ili David Howells anufaike na urithi wa mkewe.

  “Baba wa watoto hawa alitengeneza mazingira ya kutowepo katika eneo la tukio wakati mauaji yanatokea (alibi) akijua kwamba iwapo atahusishwa na mauaji hayo itakuwa ni vigumu kwake kunufaika na urithi wa mkewe” Alisema mwendesha mshaitaka huyo pale mahakamani.

  Ili kuthibitisha maneno yake, Mwanasheria huyo alichezesha tepu pale mahakamani ambayo ilikuwa imerekodi mazungumzo ya David Howells na wanae walipokuwa selo….. “Inabidi tushikamane haswa, iwapo ninyi wawili mtatofautiana, na mimi nitingia kwenye mkubo, kinachotakiwa ni kushikamana kwa pamoja…. Tutakuwa na maisha mazuri baada ya hapa wala msiwe na wasiwasi, nitakuwa pamoja nanyi kwa kwa lolote litakalotokea.”

  Glenn alikuwa ndiye wa kwanza kujitetea pale mahakamni. Huku akitokwa na machozi, aliielezea mahakama jinsi alivyomtwanga mama yake kwa nyundo na kumuua na baadaye kuukumbatia mwili wake na kulia…… “Nisamehe, nakupenda sana mama yangu.”

  Glenn aliendelea kusema kwamba, kitendo kumuua mama yake ambaye alikuwa ni katili kwao, ilikuwa ndio njia pekee iliyokuwa imebaki ili kumaliza mateso waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa mama yao kiasi cha kumfanya afikiria hata kujiua. “Nilikuwa nataka mateso yakome, nilikuwa nataka niishi maisha yenye amani na furaha kama marafiki zangu na nilikuwa nataka kuyafurahia maisha wakati wote wa uhai wangu, jambo ambalo lilikuwa halipo. Njia pekee niliyoiona kuwa ingefaa ilikuwa ni kummaliza ili kuondokana na matatizo hayo.”

  Huku akitokwa na machozi, Glenn alielezea jinsi alivyotekeleza mauaji hayo peke yake. Alieleza jinsi alivyochukua nyundo ya kuvunjia mawe iliyokuwa na kutu kutoka katika mvungu wa kitanda chake na kmvizia mama yake kwa nyuma ambaye alikuwa amekaa kwenye sofa sebuleni akiandika anuani kwenye bahasha. “Nilivuta pumzi na nilitulia kimya ili asije akanisikia. Nilisimama nyuma yake na hakujua kwamba nataka kufanya nini. Nikiwa nimesimama pale nyuma yake, lakini sikudhani kama nitaweza kufanya kile nilishokusudia.”

  Lakini nikiwa bado nimesimama pale nilikumbuka matukio yote yakututesa aliyokuwa akitufanyia……. Nilimwangalia na nilianza kupata picha za matukio hayo…… ghafla moyo wangu ulilipuka, lakini kuna kitu kilinijia akilini, wala sikumbuki ni kitu gani, mpaka nilipomsikia mdogo wangu akipiga kelele… ‘Hapana..!’ Nilisema: ‘toka haraka nje!’…………. Sikutaka aone. Nilipojiwa na fahamu, ndipo nilipojua kwamba nimeua. Niliinama pale chini na kuukumbatia mwili wake kisha nikasema………………., ‘nisamehe mama, nakupenda sana mama yangu….”

  John Howells alikuwa ndiye wa pili kujitetea pale mahakamani. Aliiambia mahakama kwamba baba yao ndiye aliyepanga mpango wa kumuua mama yao, na alimsikia kaka yake Glenn alizungumzia kuhusu kutaka kumuua mama yao kwa miaka zaidi ya miwili na walizungunzia jambo hilo na baba yao. “hali ilikuwa ni mbaya.” Alisema John. “Tulipanga kumtupa kutoka kwenye kibaraza cha ghorofani (Balcony) tukiwa tumesafiri kwenda likizo ughaibuni au kumsukumia barabarani ili agongwe na gari tukiwa matembezini.”

  Lakini pia walipanga kumsukumia katika ngema (Cliff) ya bahari watakapokuwa wamekwenda kwenye ufukwe wa Flamborough kwa mapmziko.

  Hatimaye muda mfupi baada ya familia hiyo kurejea kutoka likizo kutoka katika ukanda wa bahari ya Mediterania katika kisiwa cha Ibiza hapo mnamo Agosti 1995, walipanga kwamba Glenn ndiye amuue mama yao kwa kumpiga kwa nyundo kichwani, na tukio hilo walifanye kama alivamiwa na wezi wa kuvizia (Burglary).David Howells alikanusha kuhusika na mpango huo wa kuwatumia watoto ili kumuua mama yao. Alidai kwamba alijua kuhusu Glenn kuhusika na mauaji ya mama yao baada ya kusikia mazungumzo kati yao walipokuwa wakijadili kuhusu jambo hilo.

  Howells alikubali kwamba ni kweli kwa miaka mingi alikuwa akimsihi mkewe kuacha kuwafokea watoto…. “Isingkuwa ni jambo la busara kwangu mimi kujaribu kuingilia.” Alisema Howells. “katu nisingeshinda. Tungeishia tu kubishana. Mke wangu alikuwa ni mahiri wa kusema. Alikuwa ameishika nyumba kisawasawa.”Howells alisema kwamba, baada ya mauaji alizungumza na wanae kwa makini sana. “Niliwauliza kwa nini wamefanya hivyo. Ni jambo gani litawatokea? Lakini baadae nilikubali kubeba jukumu la kuwasaidia.”

  Akihitimisha kesi hiyo iliyosikilizwa kwa siku 19, Mheshimiwa Jaji Elliot alisema kwamba, kitendo cha Bi. Eve Howells kuwa katili kwa watoto wake pamoja na mumewe, si cha kuvumiliwa lakini hiyo haihalalishi yeye kuuawa.

  Jopo la baraza la washauri lililokuwa na wanaume watano na wanawake saba lilikutana kwa masaa matatu kabla ya kuwakuta watuhumiwa wote na hatia ya mauaji. David Howells alihukumiwa kifungo cha maisha na wanae wawili, Jopo la baraza la washauri lilipendekeza Glenn atumikie kifungo cha miaka kumi na John Howells atumikie kifungo cha miaka saba, kwa sababu ushiriki wake katika mauaji hayo haukuwa na uzito. Hata hivyo iliamuliwa wawekwe kizuizini mpaka watakapotimiza miaka 18 ndipo hukumu hiyo itakapoidhinishwa rasmi.

  Hata hivyo David Howells hakuridhika na hukumu hiyo, hivyo alikata rufaa ambayo ilitupiliwa mbali. Akisoma uamuzi wa mahakama juu ya rufaa hiyo mheshimiwa Jaji alisema kwamba itabidi David atumikie kifungo cha miaka 18 jela ndipo ajaribu kuomba huruma ya bodi ya Parole.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haya wadau ni Ijumaa nyingine tena nimewaletea kesi hii iliyowahi kutokea huko nchini Uingereza.
  Kesi hii ya mauaji inahusishwa na malezi mabaya kwa watoto wetu pamoja na mahusiano nje ya ndoa.....
  Ni jambo la kusikitisha kwamba matendo mabaya ya mama yanamsababishia umauti, ambapo anauawa na mwanae mwenyewe wa kumzaa kutoka katika tumbo lake................... Balaa gani hili...........................................................!
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  I will read it first thing in the morning. Asante sana mkuu Mtambuzi kwa elimu yako nzuri.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Me huwa napenda tu wenzetu wanavyofanya investigation halafu hii defence ya alibi naona majambazi wanapenda sana kuitumia.Da wamama wakali noma unatamani hata kukimbia home .Nimewahi kuona mwanaume kasikia mkewe kashtakiwa jambo kuhusu yeye tena la kawaida akabaki kukutetemeka nilishangaa mpaka na leo
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Mkuu Ijumaa Karim. Ahsante kwa kesi nzuri
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  MTAMBUZI

  mwaka 2000 nilikutana na one friend who knew this case in person, naye ni Howells wa midland UK, wakati nasoma postgraduate huko.... hiyo kitu ni balaa chali'angu

  hakupenda kabisa kuitwa hiyo surname,
   
 7. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi malezi na makuzi ya watoto siku zote huwa yana athri sana mwenendo wa watoto hasa katika utu wao wa ndani. Ninaamin kabisa hawa watoto wangelelewa makuzi mazuri na kuonyeshwa nini athar za kulipa kisasi na kwamba wasilipe kisasi basi wangekua hivyo. hta hivyo baba yao aliunderestimate sana uwezo wa wanae na akadhani ni watoto ama wangeweza kuficha siri.

  nimekumbuka miaka ile nakua niko kijijini baba na mama walikuwa wakitaka kujadili jambo sensitive la familia ustawi wa familia walikuwa wanatutoa kwenye uwepo wao wanasema kabisa hebu kachezeni kwanza kuna jambo tunajadili hapa. kumbe ilikuwa ni njia ya kutufanya tusisikie mambo mengine tukashindwa kuwa na usiri tukajikuta tumeropoka, pia ilikuwa ni kuzoezwa kwamba kuna mida wazazi kama wazazi wanahitaj nafasi yao wenyewe. Lakini nilijifunza pia mtoto ananafasi yake na kamwe haiwez kubadilika hasa katika maamuzi ya mambo magumu ya kifamilia ikiwa ni pamoja na uwajibikaji. huyu anaambiwa akachunge mbwa anakuwa mvivu wenzie tunachungishwa mbuzi hadi 30 na ole wako apotee mmoja.

  ni vyema sisi kama wazazi tukawalea watoto katika njia iwapasayo. tusiwaonyeshe ubabe, ila tusiwapandie roho mbaya za visasi na chuki watakua nazo tu milele.
  RIP Eveln howels
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mtambuzi asante sana kwa kisa hiki.
  Kweli malezi yanahitaji busara na umakini wa hali ya juu. Waweza kusema kwa uhakika kuwa unawalea vyema wanao kumbe ndani mwao wana kisasi cha hali ya juu na wanapanga jambo juu yako.
  Mungu atangulie tuu katika kutuonyesha njia salama na ya kufaa katika kuwalea.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mtambuzi hapa tunajifunza kwamba malezi ya mtoto si kitu cha kufanyia ubabaishaji kama wahenga walivyosema, 'mtoto umleavyo ndio akuavyo'. Evelyn bila kujua amewatengeneza wanae wawe makatili km yeye alivowalea kwa 'mkono wa chuma'. Miaka ya nyuma ukimwambia mtanzania haya yanaweza kutokea hata hapa angebisha,lakini kwa kasi ya mmomonyoko wa ' traditional social networks' hatuko mbali sana kwa watoto wetu kufikia maamuzi mazito kama haya. Umetupa somo la maana sana na kuifanya ijumaa timilifu.
   
 10. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  huwa naisubirije ijumaaa!
   
 11. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hapo penye bold, tunahitaji kumuomba Mungu atusaidie tuwe na malezi sahihi kwa watoto wetu, naamini wenyewe kama wenyewe, hatuwezi maana "kila mtu jambo analolifanya ni jema sana machoni pake mwenyewe ..."
  Asante kwa mada nzuri.
   
 12. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kweli wahenga walisema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.asante sana


  sawa Baba Mkwe ujue Mtambuzi leo sina hata senti moja (......................)nimetumiwa hela ya matumizi wamekataaa..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi ahsante kwa hiki kisanga..
  Kwa kweli huwa napenda sana jinsi wenzetu wanavyoendesha chunguzi (investigation) zao!
  Back to ze topic..Ukali kwa watoto sio malezi mema hata kidogo!
  Kuna mambo ukiwafanyia watoto hayabanduki haraka kwenye akili zao!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. majany

  majany JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Niliishi na mama wa kambo........jamani jamani jamani wakina mama......hebu punguzeni ukali...huwa nikiona visa kama hivi machozi hunilenga lenga,kiukweli malezi ya utotoni yana athiri sana.Kwangu mimi,ule uzito ambao watu huchukulia mama zao,mie sina...yaani kukaa mwaka mmoja bila kumuona au hata kumsalimia,hainipi shida.....yaan..mpk huwa najiona kama tofauti...lakini yoote haya husababishwa na malezi.......THANKS MTAMBUZI....
   
 16. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Gustavo asante kama kawaida! Yaani mpaka watoto walifikia kumwua mama yao. Kutokana na ukali wake. Kweli samaki mkunje angali mbichi!!
   
 17. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,735
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mkuu nashukuru kwa hilo desa wengine tumejifunza kitu hapo.
  hiyo kesi ingekuwa bongo watoto na baba yao wanakula bata sasa hivi we sibiri uone ya msofe...
   
 18. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  KAma mmesoma vema , mtoto wa pili alivotoa ushahidi alitamka bayana kuwa mpango huo ulikuwa wa baba yao. NA alipowekewa tepu bila yeye kujua aliwaambia watoto wake tushikamane na baada ya hapa tutaishi maisha mazuri, so mimi kwa mtazamo wangu sidhani kama ni malezi, ila ni baba mtu tamaa alowatia watoto ili wadhani kuwa wataishi maisha ya starehe .

  NA kutaka kuthibitisha hili mtoto wake alivomuua mama yake alimkumbatia na kumwambia nakupenda mama nisamehe ! so haya KATILI NI BABA , NA AOZEE JELA
   
 19. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  N a wewe si ucomment kwa pale chini mpaka ulicomment lote hili
   
 20. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Nashukuru mkuu........!
   
Loading...