MAUAJI YA ELIMU TANZANIA

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
621
Haya mauaji ya kielimu hayana tofauti na mauaji ya vikongwe kule Mwanza na Shinyanga yaliyomuondoa waziri yule wizara ya mambo ya ndani...!!.
Tofauti ni moja tu kuwa haya ya elimu hasa huko shule za msingi wanakohitimu bila kujua kusoma ni mauaji yauayo akili ya kuweza kufikiri vyema ila haya ya vikongwe yanaua mwili na roho.

Mauaji ya kielimu hayana tofauti na mauaji yaliyofanyika kwenye operation tokomeza na kuwaondoa akina Kagasheki na Nchimbi...!!
Mbaya zaidi huwageuza watu kuwa bookish badala ya kuwa watu wa kuhoji .

Tena haya ya kielimu ni mabaya na makubwa zaidi kuliko yaliyotangulia...!!.
Yanaua akili za watu na kubaki kuwa mtaji wa kisiasa .

Haya yanawaloga watanzania wawe na fikra dumavu wafikiri ccm ndiyo mungu wao hadi wengine hudiriki kusema chama ni baba au mama yako .

Hatariiiii

Justin Mwanshinga
 
Elimu ni suala pana kidogo!

Ipo Formal, Informal na Non Formal Education.Unapokosa mojawapo kati ya haya basi Elimu yako inakuwa na walakini kwa namna moja au nyingine.

Kuanzia Malezi katika Familia zetu, Jamii na hadi ngazi za kitaifa suala la Elimu (Kwa umoja wa hizi aina tatu) inabidi kusukwe kweli-kweli ili kuondokana na ujinga wa kihalaiki, Ushabiki, Umaamuna, Unazi nk.From there, ndipo mtu anaitwa ana Elimu (Si vyeti).

Bado nafanya tafiti kugundua kuwa ni Taifa gani limewahi kuwa na maendeleo endelevu kwa kucheza ama kutokuwekeza katika Elimu ya raia wake ila jitihada zangu zimeshindwa kufua dafu hadi hivi sasa.

Hizi ni hesabu, Ipo haja ya kukaa chini na kutafuta majawabu.
 
Back
Top Bottom