MAUAJI YA DEREVA TEKSI: Familia yaichachamalia polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAUAJI YA DEREVA TEKSI: Familia yaichachamalia polisi

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Mar 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  WAKATI polisi ikihaha kujikwamua na tuhuma za mauaji ya dereva wa teksi kwa mgongo wa majibu ya daktari, familia ya marehemu imekataa uchunguzi wa maiti ya ndugu yao kufanywa bila ya kushirikishwa kwa daktari huru.

  Inadaiwa kuwa dereva huyo wa teksi, Mussa Juma, 27, aliuawa akiwa kituo cha polisi cha Cang'ombe kutokana na kupata kipigo kikali wakati akihojiwa kuhusu tukio la ujambazi.

  Msemaji wa familia hiyo, Mwijuma Mzee aliliambia gazeti hili jana kuwa familia itaweka daktari wake katika kila hatua ya kuchunguzi wa maiti hiyo kabla ya kukubali kuupokea kwa ajili ya mazishi.

  "Lengo ni kuhakikisha hakuna udanganyifu unaofanyika na pia ni kupata majibu yaliyo sahihi kuhusu kifo hicho," alisema.
  Alisema kazi ya kufuatilia suala hilo itaongozwa na Kapteni Ibrahim Bendera, wakili ambaye ameteuliwa na familia hiyo kufuatilia hatua zote za kisheria katika tukio hilo.

  Mzee pia alisema familia ya marehemu haikubaliani na tume iliyoundwa na polisi kuchunguza suala hilo kwa kuwa tume hiyo sio huru.

  "Haiwezekani polisi ambao ni watuhumiwa wachunguze tukio hilo pekee yao bila kuhusishwa watu wengine. Lazima uwepo ushirikishwaji wa wanafamilia," alisema.

  Jana kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa ukweli wa kifo hicho utajulikana baada ya daktari kuufanyia uchunguzi mwili wa kijana huyo ambaye alitarajiwa kufunga ndoa jana.

  Alisema Musa alifarikia hospitali muda mfupi baada ya kukamatwa na askari kwa ajili ya mahojiano.

  "Aliwaambia askari hao kuwa anajisikia vibaya ndipo alipochukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Temeke na kufariki dunia," alisema.

  Baada ya kutokea kifo cha dereva huyo, tulifungua faili la uchunguzi wa kutaka kubaini kama kifo hicho kimetokea katika mazingira gani... polisi waliohusika wanahojiwa, alisema Kova na kufafanua kuwa wanaoshikiliwa ni askari wanne wa kituo cha Changombe.

  Alisema uchunguzi huo wa kina utakashirikisha madaktari kadhaa.
  Akielezea tukio hilo, Kova alisema Mussa alikamatwa baada ya kuhusishwa na tukio la ujambazi lililotokea eneo la Mbozi Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

  Alieleza kuwa alikamatwa Machi 10 majira ya saa 10:15 jioni baada ya gari lake namba T.227 AFF kutambuliwa kuwa lilihusika katika tukio hilo la ujambazi.

  Kwa mujibu wa Kamanda Kova hata kama ndugu wa marehemu wasingelalamikia kifo hicho, polisi kwa utaratibu wake wa kawaida ingefanya uchunguzi wa tukio hilo kujua ukweli.
  "Huwa tunafungua jalada na kuwashikilia polisi waliohusika kwa uchunguzi," alisema Kamanda Kova.

  "Mtu wa muhimu hapa ni daktari ndiye anayeweza kusema ukweli wa tukio zima la kifo cha marehemu na kama kuna mtu atakayebainika kuhusika katika tukio hilo, atachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu tutatumia wanasheria wetu ili haki itendeke."

  Baba mdogo wa dereva huyo, Mohamed Segumba juzi aliiambia Mwananchi kuwa Mussa alikamatwa Machi 8 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku akiwa eneo la Mivinjeni wakati akielekea nyumbani kwake Mtoni Mtongani baada ya muda wa kazi kumalizika.

  Segumba alisema baada ya kukamatwa na polisi kati ya saa 2:00 na saa 3:00 usiku alimpigia simu na kumweleza baba yake mdogo kuwa amekamatwa na alikuwa anapelekwa kituo cha polisi cha Changombe.

  "Nilipopatiwa taarifa hizi niliwasiliana na msimamzi wa gari za tajiri wa kijana wetu, Ramadhani Yahaya, lakini alikuwa tayari ana taarifa juu ya tukio hilo kwani kijana wetu alikuwa ameshamweleza kila kitu," alisema Segumba.

  Segumba aliongeza kuwa walikubaliana wakutane kwenye kituo hicho cha Changombe kwa nia ya kufuatilia na kujua sababu za kukamatwa kwa kijana wao, lakini pia walitaka kumwekea dhamana kama ingewezekana.

  Segumba alisema tofauti na matarajio yao, walipofika kituoni hapo waliwekwa chini ya ulinzi na kuanza kuhojiwa kama watuhumiwa kwenye chumba ambacho walimkuta kijana wao ameketi kwenye kiti akihojiwa na polisi.

  Alisema kuwa wakati wakihojiwa na kupigwa, walisikia sauti zinazoonyesha kuwa kijana wao alikuwa akilazimishwa kukiri kuhusika kwenyeb ujambazi kabla ya askari mwingine kuingia na kumchukua kijana wao na kuondoka naye kwenda sehemu ambayo hawakuijua.

  Baadaye walitakiwa kurejea kituoni baada ya siku mbili na walipoenda siku hiyo hawakuruhusiwa kumuona. Lakini baadaye askari walimchukua mchumba wa dereva huyo, Rehemu Kipanda, na kumhoji kwa muda wakiuliza maswali yaliyohusu afya ya mtarajiwa wake.

  Baada ya mahojiano hayo ndipo walipoeleza kuwa kijana huyo amefariki.

  Habari hii imeandaliwa na Geofrey Nyang'oro, Mahija Mpera na Tumsifu Sanga
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18494
   
Loading...