MAUAJI YA DEREVA TAKSI:Msemaji wa familia ahojiwa saa tatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAUAJI YA DEREVA TAKSI:Msemaji wa familia ahojiwa saa tatu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Geofrey Nyang'oro

  FAMILIA ya Musa Juma anayedaiwa kuuawa na polisi wa kituo cha Changombe jijini Dar es Salaam jana alishindwa kupata majibu ya awali ya uchunguzi wa kifo hicho baada ya msemaji wa familia hiyo, Mwijuma Mzee kushikiliwa na Jeshi la polisi kwa mahojiano kwa muda wa saa tatu.

  Tukio hilo, lilitokea jana siku ambayo daktari alitarajiwa kutoa majibu ya awali kama alivyoahidi baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo, uliofanywa juzi.

  Daktari huyo kutoka hosptali ya Taifa ya Muhimbili, aliyeteuliwa na familia kwa ajili ya kushiriki kufanya uchunguzi wa kifo cha Musa Juma.

  Mzee ambaye pia ni mjomba wa marehemu, aliyetakiwa kwenda kuchukua majibu hayo jana aliliambia Mwananchi kuwa kabla ya kwenda hospitalini aliitika wito uliotolewa na polisi juzi ukimtaka aende kituoni hapo na mwanafamilia mwingine, lakini hakuambiwa sababu ya wito huo.
  Baada ya uchunguzi wa mwili wa marehemu kukamilika polisi walinitaka mimi na Dk Zuberi Kipingu ambao kwa pamoja tulishuhudia uchunguzi huo, wakitutaka kuripoti kituoni leo (jana) asubuhi, hata hivyo polisi hao hawakutueleza sababu za wito huo, lakini tulipofika walituhoji kwa muda wa saa tatu jambo lililonifanya nishindwe kwenda kufuatilia majibu ya uchunguzi huo kutoka kwa Daktari wetu,alisema Mzee.

  Mzee alisema kazi ya kumhohoji ilianza saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 asubuhi na wakati wote polisi hao,walitaka kujua kazi aliyokuwa aikiifanya marehemu, historia yake na namna yeye anavyomfahamu kijana huyo ambaye ni mtoto wa dada yake.

  Katika hatu nyingine familia hiyo, imesema imenyimwa fursa ya kushiriki kupeleka vipimo kwa mkemia mkuu wa serikali ambaye ndiye atakayetoa majibu ya mwisho ya uchunguzi huo.

  Alisema pamoja na wao kuomba daktari wao kushirikishiwa, jeshi hilo liligoma na kusisitiza kuwa kazi hiyo, itafanywa na daktari aliyetoka polisi na kwamba familia hiyo, itatakiwa kusubiri majibu ya vipimo hivyo.


  Sisi kama familia hatutakuwa na mashaka na majibu ya Mkemia huyo kwa kuwa hatua zote za uchunguzi tumeshiriki vizuri, wakati wa uchunguzi familia iliingiza watu watatu akiwemo Mwanasheria wa familia kapteni Ibrahim Bendera na Dk Kipingu na mimi mwenyewe, mwili tuliuona kwa macho na tulishuhudia kila kitu," alisema Mzee.

  Katika hatua nyingine vilio na simanzi vilitawala eneo lililo karibu na chumba cha kuhifadhia maiti baada ya ndugu wa marehemu Juma kushindwa kujizuia na kuanza kulia pindi walipoona jeneza la kijana huyo, likitolewa kwenye chumba hicho, na kupelekwa msikitini.

  Mwili wa marehemu Juma jana ulisafirishwa kuanzia saa 7:00 mchana kutoka hospitalini na kupelekwa Bagamoyo ambako ulizikwa baadaye saa 10:00 jioni.

  Kifo cha Juma kilizuia uatata mkubwa baada ya kijana huyo kukamatwa na polisi Machi 8, mwaka huu na polisi wa Changombe na kukushirikiwa na Jeshi hilo taarifa za kifo chake zilipojulikana Machi 10, mwaka huu.


  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18557
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280
  Ukisikia polisi jamii ndio hii.
  Kwanini wamemkataa daktari wa familia kushiriki uchunguzi?
   
 3. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapa Polisi walikuwa wanakwepa liability. Sasa kama mtindo huu wa kulindana kwa mapolisi , madaktari na ma-nurse wa mwananyamala kwa mauaji ya watu wasio na hatia yataendelea tutafika wapi? Nina imani wahusika IGP Mwema na Prof. Mwaikyusa wasiposhikia bango mambo haya itafika wakati watu watalipuka ama kupasuka kama jipu lililokaa kwa muda mrefu makalioni na likapasukia sokoni, msikitini au kanisani mbele za watu. Waelewe watanzania sio kondoo kama alivyokwisha kusema Mchungaji Mtikila siku za nyuma. Uvumulivu utakapotwashinda watajua kuwa watanzania ini simba na siyo kondoo.
   
Loading...