Mauaji ya Daudi Mwangosi: Ushuhuda wa kilichotokea hadi kifo chake

Duh, sasa wamwache marehemu apumzike,kila siku anaibuka mwingine na stori ile ile. Hizi topic zinajaza server tu sasa.
Hili halitaacha kujadiliwa milele katika nchi hii ni tukio la kuhuzunisha na kufedhehesha na pia ni moja ya sababu ya kupigilia msumali wa mwisho katika jeneza la CCM
 
hii ni murder case kwa wahusika wote. haki itatendeka tu siku moja. RIP Mwangosi. hutoenda bure for sure!
 
Tunahitaji huruma ya mungu kama polisi wetu ndio hawa. Kwani kama wanaamua kuua tu bila kuangalia madhara yake kwa jamii, THIS IS ONLY IN TZ.....!
 
Huyu RPC wa Iringa ni muuaji namba 1.


Ni zaidi ya shetani huyu!

RIP Daudi Mwangosi!
 
Hii inasikitisha sana, Sikuamini mwanzoni kuwa Daudi Mwangosi ndiye aliyeuawa kinyama vile, japo niliona picha toka siku ya tukio, lakini akili yangu ilikuwa ngumu kukubaliana na hali halisi, sijui familia yake itakuwaje! ni kama namuona Marehemu Mwangosi, sikuwa namfahamu sana kabla, lakini kupitia mafunzo ya picha ambayo tuliyaendesha mwaka juzi pale Iringa ndipo nilipata bahati ya kufahamiana naye kwa karibu zaidi, kwani tulikuwa wote muda wa majuma mawili, tulifahamiana vizuri.

Tuli-share interest, hasa kujisomea na kujiendeleza, maana alikuwa ni mtu anayependa sana kusoma vitabu, hivyo tulikuwa na mengi ya kibadirishana, ukweli ni kuwa sote tutakufa siku moja lakini kifo chake kitabaki katika kumbukumbu za wengi wetu ambao tuliwai kumfahamu japo kwa muda tu, inasikitisha sana ikiwa kuna binadamu anaweza kumtendea unyama kiasi kile binadamu mwenzie kana kwamba yeye amehaidiwa kuishi milele chini ya jua, akumbuke kuwa malipo ni hapahapa duniani.

Mungu awape moyo wa subira mjane na watoto.
Buriani Daudi Mwangosi.
 
Michael Kamuhanda aliua vijana wa chadema songea akahamishiwa iringa, na mwangosi alihukumiwa kifo toka alipomsumbua kwa maswali magumu rpc kamuhanda na ile signal ya kunyoosha bastola juu ilikuwa ni amri ya kumlipua mwangosi ambayo ilitekelezwa, ila wafanye wafanyavyo damu ya mwangosi inawalilia wote waliohusika hata kama wataloga usiku kucha hawaponi ng'oo mkono wa mungu uko juu yao.

Kama hawaamini wamuulize sani abacha alivyomuuwa keni sarowiwa alidumu miaka mingapi chezea mungu nyie, haya bwana tuuweni tu majibu mtayapata.
 
RPC Michael Kamuhanda kabla ya kuhamishiwa Iringa alifanya mauaji Songea alikokuwa kama RPC, Kwa bahati mbaya sana Michael Kamuhanda alimhukumu kifo Mwangosi bila yeye Mwangosi kujua alipokuwa akimbana kwa maswali magumu na ndiyo maana hata alipofuatwa kutoa msaada kumwokoa Mwangosi hakutoa kwakuwa kilichokuwa kinafanyika ndicho alichoagiza kifanyike, na ile ishara ya mkono juu na kisha bastola juu ilikuwa ni amri ya kumlipua Mwangosi ambayo ilitekelezwa na yule askari PC wa FFU alichofanya ni kutekeleza amri ya kumuuwa Mwangosi,

Hata hivyo ni kweli wamemuuwa Daud lakini damu yake inawalilia na hakika wataangamia hata wakikesha kwa kalimanzila hawaponi ng'ooo, Mkono wa Mungu uko juu yao kama hawaamini waulize kilichompata General SANI ABACHA WA NIGERIA baada ya kumuuwa KENI SAROWIWA JE ALIISHI?

Kabla ya kifo chake alishuhudia kifo cha mwanaye wa kwanza wa kiume kisha AKAFUATA YEYE, SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU ngoja tusubiri RIP MWANGOSI.
 
askari wa tanzania ni watu katili kuliko unavyo weza kudhani,ni kama wako juu ya sheria.wanaua,wanashiriki kwenye ujambazi,wanabambikiza watu kesi za mauaji hakuna wanacho fanywa!!!!kwa hili la MWANGOSI naomba laana ya MUNGU iwakute na ipo siku MUNGU atafanya maajabu wasio yatarajia.KAMHANDA INAONEKANA alipanga na kumuandaa askari wa kumuua mwangosi.
 
halafu hawa mapolisi wetu elimu yao ni FINYU sana.............kuanzia alipoongea RPC Kamuhanda mpaka kwa Bosi wake Mwema..........Safu yote ya uongozi ya Polisi iwajibishwe..........
 
Haya yanayotokea ni matokeo ya kuliacha Jeshi la Polisi kufanya vitu vya hovyo hovyo bila kudhibitiwa,ni kipindi kirefu sasa Watanzania tumekuwa tukilalamikia uonevu, kupigwa, kubambikiwa kesi na uonevu mwingine mwingi kutoka katika Jeshi hili tulilolirithi kutoka kwa Wakoloni. Ninaimani madhumuni yaliyokusudiwa kuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya usalama wa watu na mali zao hayapo tena!

Watanzania wote shime tuungane tupinge kadhia hii ya Polisi, matukio mengi ya mauaji tumeyashuhudia tena yakitekelezwa na Jeshi hili na wahusika wakiachwa huru bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria tunashindwa kuelewa waha maRPC wanapata wapi nguvu na maamuzi ya kutekeleza mauaji kama siyo maagizo toka ngazi za juu?
 
Dah hivi hapa tuna jeshi la polisi au tuna majangili dhidi ya wanainchi!! Imeniuma sana tena sana, niliumia sana na niliteseka moyo sana wakati ule Dr Ulimboka alipotekwa na kuteswa na hili limetuongezea machungu sana watanzania ....hii nchi ina Raisi kweli???

Why!!! Ni nini tafsiri ya haya?? Kumbe sasa inaonyesha wazi ni jinsi gani tasnia ya habari nchini inavyochukiwa na watawala wetu, n that's why hata gazeti la mwanahalisi likafungiwa, demokrasia inayohubiriwa na amani inayohubiriwa nchini iko wapi ??

Sasa ifike mahali tuseme imetosha!!! RIP Mwangosi
 
ni lazima nichukie na nawachukia hawa CHADEMA kwa kuwa ninaipenda kazi yangu na pia ninakaribia kustaafu na sitaki kustaafu vibaya.”Tunaomba mtuwekee na picha yake huyu mtu ambaye anaona tumbo lake bora kuliko uhai wa mtu
 
Kwa kweli hivi kwani m4c ina nini kwa ccm?wao si wanajiamini kwamba wana hati miliki ya kuongoza sasa wanaua2 ovyo2 kwa nini?
 
Back
Top Bottom