Mauaji ya Daudi Mwangosi: Jaji Mstaafu Ihema Kuongoza Tume Huru ya Uchunguzi!

Kupoteza kodi za wananchi kwa tume ya jambo lililo wazi? Hebu tubadilishe mtindo wa kudanganya Watanganyika. Sasa hivi wanaelewa si wadanganyika na mbumbu tena.
 
Waziri Nchimbi kwanini asichukuwe maamuzi magumu kama waliyofanya wenzake, Mwakyembe na yule wa maliasili? Wao wamewasimamisha kazi watendaji kupisha uchunguzi. Sasa huu uchunguzi ambao utafanywa na Kamuhanda bado yupo ofisini utaleta tija kweli! Kwanza alishaua huko Songea, ikaundwa Tume na Chagonja lakini majibu ya Tume mpaka Masiha arudi tena kwa mara ya pili! Tume hii itamchunguza huyo huyo tena, kazi ipo!
 
Tulishapoteza naye imani kwenye kifo cha marehemu Ally Zona Morogoro baada ya kutoa majibu ya hovyo kabla ya TUME na kisha TUME ikaleta majibu ya hovyo hayohayo. Vilevile tunamshangaa kwa kuwashirikisha POLISI wa hapa nchini kwenye TUME hizi ambazo na wao ni walalamikiwa/wahalifu. Hatutegemei jipya, na kama mwendo ndiyo huu basi ni dhahiri SERIKALI yetu imeshindwa. Kwa ushauri wa harakaharaka ni bora yeye na wakuu wenzie wa Wizara ya Mambo ya ndani akiwemo IGP Mwema wajiuzuru haraka ili kurejesha imani kidooogo na jeshi letu la polisi pamoja na serikali.

Nadhani hata kifo cha Mh.Amina Chifupa wenye ccm yao walisema
 
  1. Judge...........Mwenyekiti
  2. Theophile Makunga-Tanzania Editors Forum (TEF)
  3. Pili Mtambalike-MCT
  4. Jeshi la Polisi
  5. Mtaalamu wa Mabomu
ameipa mwezi mmoja ilete taarifa, anasema kuna maswali mengi yamegubika kifo cha Mwangosi mojawapo ikiwa ni mahusiano kati ya mwandishi na jeshi la polisi na amesema hivi karibuni atachukua hatua kali dhili ya polisi wazembe

I smell something fishy here
 
Kwani huyo askari alieelekeza bunduki kwenye tumbo la marehemu hajulikani? watu wa iringa tupeni taarifa za askari huyu ndiye alieua.
 
Tulisema tangu 'breaking news' ya tukio kuwa tutasikia upuuzi wa kuunda tume.
Jana ilundwa tume na IGP kuongoza kama sitakosea.
Leo Nchimbi anaunda tume nyingine.
Wamechanganyikiwa kwasababu ukweli upo wazi na wanajua lazima WAONDOKE ili nchi itulie

Nchimbi anaunda tume ili kulinda kibarua chake na si kutafuta ukweli.
Huu ni upuuzi na tusiendelee kuukubali.

NCHIMBI NA MWEMA wanapaswa kuondoka kwanza ili kupisha uchunguzi halali.
Hawana mamlaka ya kiroho kusimamia tukio hili.

Hajawahi kuchukua hatua kali, hawezi kuchukua hatua kali.
Anachokifanya ni kijificha nyuma ya tume ili hali yeye ni mhusika katika mazingira ya tukio na anatakiwa akae pembeni.

NCHIMBI RESIGN FIRST! Stop bla bla bla.
 
Hiyo tume inaenda kuchunguza nch gani mpaka iwe mwezi?? siku 7 zinatosha na kuzidi kwani kilakitu kikowazi. kama kashindwa asepe na tume yake. Je tume ya morogoro inasemaje? na dr. ulimboka inasemaje? zote siziko chin yake? kwenda zako mzushi...
 
  1. Judge...........Mwenyekiti
  2. Theophile Makunga-Tanzania Editors Forum (TEF)
  3. Pili Mtambalike-MCT
  4. Jeshi la Polisi
  5. Mtaalamu wa Mabomu
ameipa mwezi mmoja ilete taarifa, anasema kuna maswali mengi yamegubika kifo cha Mwangosi mojawapo ikiwa ni mahusiano kati ya mwandishi na jeshi la polisi na amesema hivi karibuni atachukua hatua kali dhili ya polisi wazembe

Mtu anayeteua tume ni sehemu ya watuhumiwa..polisi inafanya kazi chini ya mamlaka ya waziri nchimbi.lolote baya au zuri linalofonywa na polisi linapimwa kama sehemu ya utendaji wa waziri. huu ni upuuzi wa kiwango cha juu kuwahi kuushuhudia ktk dunia tunayoishi...hatuwezi kutuhumiwa sisi alafutukajiundia tume ya kutuchunguza sisi wenyewe.. hiki si chombo huru cha uchunguzi...

Chombo hiki hakiwezi kufanya kazi kwa uhuru wakati watu wanaotuhumiwa wakiwa bado wako ofisini na wanaendelea na kazi...watatumia nafasi na mamlaka walionayo ku-frastrate uchunguzi...mhm kuliko yote kwa kuanzia ni kujiuzulu kwa wale wote wanaotuhumiwa moja kwa moja na wale ambao makosa na unyama huu umefanyika chini ya dhamana yao..

Waziri wa mambo yandani ya nchi, IGP, mkuu wa operesheni na mafunzo, RPC Iringa, RCO Iringa, kikosi kilichoendesha operesheni ya mauaji, mkuu wa mkoa wa Iringa kama mwenyekiti wa Kamati yau ulinzi.na usalama ya mkoa, mkuu wa wilaya kama kiongozi wa ulinzi na usalama wa wilaya, Mtend.aji wa kata ambamo mauaji yamefanyika kama mwenyekiti wa kamati ya ulizi na usalama ya kata, mwenyekiti wa kijiji husika na mtendaji wake, hata mwenyekiti wa kitongoji ktk eneo hilo...

Hatuwezi kuwa na taasisi amabazo zimekabidhiwa dhamana ya kutulinda alafu kinyume chake taasisi hizo zikageuka kuwa muuaji mkubwa wa raia bila kuchukuliwa hatua..huku mamlaka zinazohusika zikiendelea kukaa kimya nwa kuwakingia kifua wauaji...kwa maneno mepesi kabisa ni kwamba sasa hivi kama nchi hatuna dola..

Hatuna dola kwa sababu "mamlaka iliyopo imeshindwa kukidhi vigezo vya kuitwa dola...dola inayoshindwa kufany kazi ya msingi ya kuhakikisha usalama na uhai wa raia hiyo ni dola mfu...Dola inayoua wananchi wake badala ya kuwalinda si dola bali ni kichaka cha wauaji

We have abandoned our ideals. this is the worst stage of irresponsibility.

Kwa waandishi wa habari huu ndo wakati wenu wa kuonyesha kwamba you are a Forth PillAr of thd state..mkishindwakutumia nafasi yetu vizuri katika kipindi hiki, mtakuwa mmejisaliti wenyewe..na historia yataifahili itawaandika ktk upande msostahili kuwepo....

Twafahamu kati yenu wapo wachumia tumbo na wataendelea kuwasaliliti lakini kumbukeni mabadiliko yoyote ya kweli huwa hayaletwi na watu 100 bali wachache wenye dhamira ya dhati na utashi wa kweli kutimiza azma ya ukombozi...mkisubiri wanaochumia tumbo na waoga wawaunge mkono haki yenu mtakuta imeshavuka mto na kwa hiyo hamtaipata tena.

Hata siku moja kumbikeni Hakuna mtu aliewahi kusifiwa kwa kushindwa, praise alwayz go to the victor/winner.. no right has everbeen given on a golden plate.msipodai nakuitaka haki yetu hakuna atawaletea mkiwa mmetulia..

Tuko pamoja nanyi.
 
Nchi ina udhalimu wa hali ya juu, kwa ali hii nimeamini serikali ya tanzania ni katili na isiyo na huruma kwa watu, wapo kwa maslahi yao na watoto wao, la IRINGA lipo wazi haliitaji tume wala uchunguzi, hatua za kuwanyonga hapo zifate
 
Toka siku nyingi namchukia sana Emmanuel Nchimbi, tangu akiwa UVCCM. Huwa nikisikia tu akitajwa au kaandikwa kwenye gazeti hasira inanipanga. Mungu anisamehe? Mtu mwingine ni Januari Makamba. Sijui ni kwa nini watu hawa ninawachukia? Mungu anisamehe lakini.

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Makubaliano yaliyofikiwa jana baina ya Dr Slaa na IGP Mwema ni pamoja na kuundwa tume ya kupokea malalamiko dhidi ya vitendo vya polisi kuua raia wasio na hatia. Tumaini Makene ameteuliwa kuingia katika tume hiyi akishirikiana na Robert manumba na tayari wameanza kazi Jana.

Hii ni tofauti na ile tume ya Nchimbi
 
Tumaini Makene huyu huyu anaekuja JF? mbona kachoka hata michango yake humu haina mshiko?

Sasa nayakubali maneno ya Sitta.
 
Polisi watatugeuka muda si mrefu. Mkuu Tumaini Makene, hayo makubaliano ya kufanya uchunguzi wa pamoja mliandikishana au??
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna tume ngapi?

mwisho zitatuchanganya. Kuna uchunguzi wa UTPC unafanywa na Simbeye, Uchunguzi wa MCT unaongozwa na John Mirenyi, Haura Shamte na Berege simoni, upo wa Polisi unafanywa na polisi wenyewe, upo wa kamati ya nchimbi na huenda wanaharakati wakateua ya kwao.
 
Back
Top Bottom