Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,359
Tusiingize siasa kwenye kila jambo waachieni wenye fani zao waseme kitaeleweka tu.
Elewa kuwa kila kitukatika maisha yako ni siasa. Ndio maana unakaa Masaki na sisi tunakaa kwa mfuga mbwa, ndio maana unaenda kazini na gari wakati wenzio tunatembea kwa mguu kwenda kazini. Ndio maana unaelimu bora kunizidi mimi, ndio maana ukiugua unaenda Ulaya kutibiwa wakati mimi nikiumwa naenda kwa babu loliondo.
Ndio maana nyumba yako inalindwa na security group, ina fensi ya umeme, ina mbwa wanaokula zaidi yangu na bado unalala na bastola wakati mimi mlango wangu umefunikwa na gunia, na wala siogopi wezi, wataiba nini marapurapu na mitumba?
Ndio maana wewe unafanya mikutano ya kampeni Zanzibar na mwema hasemi kitu, unaenda kulinda kwenye fiesta mwema anakenua lakini mimi nikifanya mikutano unaniua.