Mauaji ya Albino "inawezekana" ya Mkono wa CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Albino "inawezekana" ya Mkono wa CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Jul 4, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Ndugu wanajamvi, wiki iliyopita mmoja wa wabunge toka chama cha CUF wa jimbo moja la kusini. Katika kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu mbunge huyo alisema inaonekana bila shaka kwamba mauaji ya albino huchochewa na wakubwa na wenye fedha. Alisema kwa sasa albino wanapotea katika mazingira yasiyowazi,hawauliwi tena kwa namna ya awali bali hupotezwa na kuuliwa mafichoni.

  Huko Tukuyu-Mbeya kuna mauaji ya aliyekuwa diwani wa kata ya Kiwira na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, marehemu John Mwankenja. Watu zaidi ya 11 wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo. Mmoja wa watuhumiwa alikamatwa akiwa na silaha na risasi kadha. Inasemwa kuwa aliyekamatwa na silaha ni muaji mzoefu. Kwa maelezo yake ati amekiri kumwua John Mwankenja kwa kuwa marehemu hakumlipa ujira wake ambao mtuhumiwa anadai amewahi tumwa na marehemu Mwankenja na kiongozi mwingine (waziri) katika serikali ya JK kumwua kijana albino aliyekuwa anasoma kidato cha pili huko Rungwe. Baadhi ya viungo vya kijana albino huyo vilikutwa kwa mganga wa kienyeji wilayani Ileje.

  Aidha, mtuhumiwa alishaua watu wengine wawili mmoja alimuuwa huko katika eneo la Makandana katika mji wa Tukuyu na mwingine alimuuwa katika mji mdogo wa Kiwira. Mtuhumiwa anadai Mwankenja hakumlipa haki yake kwa kazi hiyo. Na alipomdai alionesha kama asingemlipa na zaidi yeye Mwankenja angemuuwa huyo mtuhumiwa. Hapo ndipo mtuhumiwa huyo alipoamua kumuwahi marehemu Mwankenja.
  Inasemekana, mtuhumiwa amedai yeye hakutumwa kumuuwa Mwankenja aliyafanya mauaji hayo yeye mwenyewe kwa sababu hizo.
   
Loading...