Mauaji ya Akwilina: DPP afunga jalada la kesi baada ya Jeshi la Polisi kushindwa kubaini mhusika wa mauaji

CCM wameshapata mbunge kwa dhulma, hawajali tena. Damu ya Akwilina haitakwenda bure
 
Hii ni dharau kubwa kwa Watanzania, si kila taarifa ni habari.
 
Kulikiwa na umati mkibwa hivyo kumtambua aliyepiga risasi ni ngumu sana, kwahiyo ni sawa na wananchi wenye hasira kali wanaorusha mawehovyohovyo na litakapompata mtu ,huwei kujua limerushwa a nani
 
MAREHEMU SIKU ZOTE HANA HAKI, sasa tarehe 26 kaandamaneni muone chamoto. Nyendeni mkafanye kazi mjenge maisha yenu binafsi
 
Hivi mlitegemea nini tafauti sana na hiki nyie watu?. ..muuwaji wa Akwilina ni miongoni mwa wasio julikana. Wasio julikana = serekali.
Wakati mnaendelea kushangaa kumbukeni na haya matukio jinsi jeshi lenu lilivyo ya handle 1) Kupingwa risasi Tundu Antipas Lisu. 2).mabo ma ya soweto arusha. 3)kuuliwa kwa Alphonse Mawazo. 4) kutekwa kwa watu mbalimbali kunakwo shamiri hivi sasa. 5)..............
 
bado ofisi ya DP ina matatizo. yaani polis hata wakiua watu mamia hawawezi kushotakiwa? Huyu DPP ilibidi atenguliwe fasta.
 

DPP Biswalo Mganga amesema amefunga jalada la kesi ya mauaji ya Mwanafunzi, Akwilina Akwilini baada ya kushindwa kubaini aliyehusika na mauaji.

--------------
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini amelifunga rasmi.

Hayo ameyasema leo Aprili 20, 2018; Ikulu jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari huku akionya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari.

Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishtaki jeshi.

”Katika maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote.”

Alipoulizwa kuhusu askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio hilo, Biswalo amesema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao wameachiwa huru hawana hatia.”

Mkurugenzi huyo amesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha amani inakuwapo,”na niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa, si mwanasiasa, kwa hiyo sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo, nitamshughulikia.”

“Na wanaosema wataandamana, waambieni wasifanye hivyo kwani wakiandamana watakwenda kuwasilimulia familia yake,” amesisitiza Biswalo

Pia, amevionya vyombo vya habari ambavyo vinavyoweza kuchangia uvunjifu wa amani, hatua zitachukuliwa hivyo kuvitaka kuwa makini na kutimiza wajibu wao kwa kufuata misingi ya taaluma yao.


Chanzo: Mwananchi

Pia soma
- Maandamano ya CHADEMA: Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika

- Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA

- Kamanda Mambosasa: Tunamtafuta Mbowe, pia tunawashikilia Askari 6 waliotumia silaha za moto kudhibiti waandamanaji
Lakini si kilisababishwa na wakina mbowe i.e viongozi wa chadema !
Sasa limefungwa kivipi ?
 
Haki inapatikana Kwa Mungu na sio kwa mwanadamu, inamaana kwamba uyo mdada alikufa mwenyewe, pia nimeshangaa jinsi kesi ilivyoenda haraka wakati kuna watu walio na kesi Kama hii bado uchunguzi unaendelea.
 
Back
Top Bottom