Mauaji / Ukatili wa Jeshi la Polisi kwa Raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji / Ukatili wa Jeshi la Polisi kwa Raia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mizambwa, Mar 6, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Jeshi la Polisi linaendelea na utaratibu wake wa kufanya mauaji / Ukatili kwa raia wasio na hatia, tena mauaji kwa raia asiye na silaha yoyote.


  Wana jamvi naomba tukumbushane mauaji yaliyofanywa na Askari Polisi katika kipindi cha kuanzia mwaka 2005 hadi hapa tulipo. Na kama kuna picha ya tukio au source ni vyema ikaambatanishwa katika mchango wako, Pia na hukumu gani ilitolewa kwa wahusika.  NATOA HOJA


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 2. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  unatukumbusha machungu tuliyokwisha sahau!!!:rant:
   
 3. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Yaani kweli ni uchungu, lakini mbona ajabu bado yanaendelea. Tukumbushane kwani huenda humu ndani wapo au wahusika watapitia thread hii ili wajirekebishe. LABDA ITAWAUMA KIDOGO!!!


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Ile kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini wilayani Mahenge mkoani Morogoro na dereva, inayowakabili maofisa 13 wa Polisi akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abdallah Zombe.

  Mbali na mashahidi pia kuna vielelezo vingi zikiwemo ripoti za daktari, ramani ya tukio, maganda ya risasi na vingine.

  Walidaiwa kuwa Januari 14, mwaka 2006i wakiwa katika msitu wa Pande Luisi ulioko Mbezi, Dar es Salaam walimuua kwa makusudi Bw. Ephraim Chigumbi.

  Katika mashitaka mengine walidaiwa kuwa siku hiyo na wakiwa katika msitu huo waliwaua kwa makusudi, Bw. Sabinusi Chigumbi, Bw. Juma Ndugu na Bw. Mathias Lukombe ambapo walikana kutenda makosa hayo.

  Kwa mujibu wa maelezo ya kesi hiyo ambayo yalisomwa mahakamani yalisema kuwa marehemu wote walikamatwa katika eneo la Sinza, Dar es Salaam bila ya kuwa na kurupushani ambapo askari walidai kuwa ni majambazi.

  Washitakiwa hao ni Bw. Zombe, Bw. Bageni, Bw. Makele, F5912 Noel, YP4513 Jane, D6440 Nyangerella, D1406 Mabula, E6712 Felix, D8289 Michael, D2300 Abeneth, B1321 Rashid, D4656 Rajab na D1367 Philipo.


  UAMUZI WA MAHAKAMA: Washitakiwa waliachiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 17 / 08 / 2009.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 5. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LATUHUMIWA KUFANYA MAUAJI YA MWANAFUNZI.

  http://1.bp.blogspot.com/-rWUD4oOly_A/T1MF1W53S2I/AAAAAAAAEKc/b5xqUgcbkqU/s1600/DSC00506.JPG


  Jeshi la polisi mkoani Mbeya limeendelea kujisiriba matope kwa kuendesha mauaji ya kiholela kwa raia ambapo jana askari wa jeshi hilo wamemuua mwanafunzi Said Msabaha wa shule ya Sekondari Lupa iliyopo wilayani Chunya mkoani hapa.

  Mwenyekiti wa Kijiji cha Lupa wilayani humo William Patrick Mbawala, ameuambia mtandao wa huu kuwa mwanafunzi huyo kabla ya kifo chake alikamatwa na askari hao akiwa na wenzake watatu kwa tuhuma za wizi wa simu Februari 29, 2012 na baadaye waliachiwa kwa dhamana.

  Amesema baada ya kutolewa katika kituo kidogo cha Lupa, Marehemu alionekana kuwa hali yake imedhoofika na alipoulizwa alieleza kuwa alipokuwa kituoni hapo alipigwa na askari polisi jambo ambalo liliwalazimu kumpeleka katika zahanati ya kijiji hicho chini ya Mganga aliyemtaja kwa jina la Dr. Solomon.

  Naye Baba mzazi wa marehemu, Msabaha Hussein, amesema kuwa baada ya kufariki mtoto wake akachukua jukumu la kupeleka maiti kituo cha polisi ili wahusike katika kuuzika mwili wa marehemu kwa kile aichodai kuwa kifo cha mwanae ni matokeo ya kipigo walichokitoa alipokuwa mikononi mwao.

  Wamesema kuwa baada ya kuwakosa katika makazi yao, waliamua kuzichoma moto nyumba za askari hao ambao ni Copl. Maxmillian, PC Mjuni na PC Hery ambapo hawakuishia hapo walimtafuta PC Fadhil bila mafanikio na kuharibu samani zake za ndani huku wakishinikiza Jeshi la polisi kuuzika mwili wa marehemu huyo.

  Afisa upepelezi wa Jeshi hilo mkoani Mbeya (RCO) Elias Mwita alipotakiwa kuzungumzia sakata hilo alisema kuwa ni mapema mno.

  Awali askari hao walidaiwa kutorokea Jijini Mbeya lakini taarifa kutoka ndani ya vyanzo vya kikosi kazi cha mtandao huu jeshi la Polisi mkoani Mbeya vimesema kuwa askari hao walikuwa bado hawajakamatwa wala kuonekana katika viunga vya Jiji la Mbeya.

  Tukio hilo la kinyama limetokea siku chache baada ya askari wa jeshi hilo PC Maduhu kuhusika kumuua aliyekuwa Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya Daniel Godluck Mwakyusa (31) February 14, mwaka huu.
  :::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::

  MWISHO WA kUNUKUU
   
 6. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LAWAMANI KUHUSIKA NA KIFO CHA MWANACHUO ALIYE FARIKI SIKU YA WAPENDANAO YANI VALENTINE DAY


  Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya marehemu Daniel Godluck Mwakyusa (31) ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho aliuawa na Askari wa Jeshi la Polisi PC Maduhu tarehe 14/02/2012 katika sikukuu ya wapendanao {valentine day].

  Marehemu akiwa na wenzake wanne walikuwa katika matembezi ambapo polisi walikuwa doria walikuta vijana hao wakipata vinywaji ndipo waliwatuhumu kuwa ni majambazi ambapo PC Maduhu alimpiga marehemu risasi mbili kwa kutumia bunduki aina ya [SMG].

  Pia marehemu aliporwa shilingi laki tatu pamoja na simu ya mkononi .

  Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu huyo Bwana Pastory Mwakyusa amesema kuwa anasikitishwa sana na kitendo hicho kilichotokea kwani mwanawe hakuwa na tabia ya wizi au ujambazi hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kueleza sababu ya kumuua mtoto wake.

  Hata hivyo Jeshi la Polisi lilitoa usafiri wa gari lenye nambari za usajili T 138 AFK aina ya Coster kwa ajili ya kusafirisha Mwili wa marehemu kwenda katika wilaya ya Kyela kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa daktari kuthibitisha kuwa marehemu ameuwawa kwa risasi.

  ::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
  MWISHO WA KUNUKUU  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA
   
 7. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  By Waandishi wetu
  20th March 2012:  Watu watano wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kuzuka tafrani baina ya wananchi na wanajeshi waliokuwa wakishirikiana na mgambo kuendesha operesheni maalum ya kuwaondoa waliovamia eneo la hifadhi katika kijiji cha Maguba, kata ya Igawa, tarafa ya Malinyi wilayani Ulanga.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo saa Jumamosi iliyopita saa 8:00 mchana.

  Waliouawa ni Sanyiwa Ndaya (34), Lutaya Ndala (48), Nchambi Bujiku (28), Kulwa Luhende (48) na Shija Msheshiwa (35), ambaye alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Ulanga. Wote wakazi wa Kijiji cha Mguba, kata ya Igawa.

  Waliojeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Wilaya ya Ulanga ni Nkama Jisonge (35), Zina Msheshiwa (30), Msheshiwa Taiya (60) na MT 70328 Koplo Paulo Lawrent ambao hali zao zimeelezwa kuendelea vizuri.

  Akifafanua kuhusiana na tukio hilo, Kamanda Chialo alisema kuwa siku ya tukio askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Job Edward (54) Ofisa Mteule wa daraja la pili, ambaye ni mshauri wa mgambo wilaya ya Mahenge akiongoza timu ya watu 15 akiwemo askari mwingine wa jeshi hilo, MT 70328 Koplo Paulo Lawrent na mgambo, walikwenda katika eneo hilo kwa ajili ya operesheni maalum ya kuwaondoa watu waliovamia hifadhi hiyo.

  Kwa mujibu wa Kamanda Chialo, watu hao baada ya kufika walivamiwa na wananchi waliokuwa na silaha za kijadi na walipojaribu kujitetea, Koplo Lawrent aliyekuwa na bunduki aina ya SMG alifyatua risasi hewani ili kuwatawanya wananchi hao ambao waliendelea kupambana nao.

  “Na yeye huenda katika kunusuru silaha ile isiporwe na wananchi, alirusha risasi hewani zilizopoteza maisha ya wananchi wanne pale pale katika eneo la tukio, huku mwananchi mmoja akifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mahenge,” alisema Kamanda Chialo.

  Kufuatia tukio hilo, Chialo alisema watu wanane wamekamatwa na wanahojiwa na polisi ili hatua zaidi za kisheria dhidi yao zikuchukuliwe na kuongeza kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

  Awali, ilidaiwa kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro ilikwenda katika eneo hilo na kuwazuia wananchi kuendelea na shughuli za kilimo na uharibifu wa mazingira katika eneo hilo la hifadhi, lakini walikataa kwa madai kuwa hawafahamu mipaka kati ya eneo lao na eneo la hifadhi.

  Inadaiwa kuwa mipaka hiyo iliwekwa na Serikali na wananchi hao kutakiwa kutii mamlaka ya Serikali kwa kuacha kufanya uharibifu ndani ya hifadhi bila mafanikio, hadi ilipofanyika operesheni hiyo katika eneo hilo ambalo ni hifadhi ya wanyamapori linalomilikiwa na wizara ya Maliasili na Utalii.


  KAULI ZA DIWANI, MAJERUHI

  Diwani wa Kata ya Malinyi (Chadema), Said Tila, alisema mauaji hayo yalifanyika katika hifadhi ya Magumba ambayo kabla ya kutangazwa kuwa hifadhi, zilikuwa zinafanyika shughuli za kilimo cha mpunga na ufugaji.

  Alisema eneo hilo ambalo lilitangazwa rasmi na Serikali kupitia mikutano na wananchi uliofanyika katika tarafa ya Malinyi uliowahusisha Waziri wa Malisili na Utalii, Ezekiel Maige; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa na Mbunge wa Ulanga Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda.

  Alisema kuwa siku ya tukio, kikosi cha hifadhi hiyo kikiongozwa na wanajeshi wawili wakiwa na silaha na mgambo sita walifika eneo la kitalu kufanya doria ya kawaida, baada ya Serikali kuwataka wananchi na wafugaji kutofanya shughuli zozote.

  Kwa mujibu wa diwani huyo, walipofika katika eneo hilo, waliwakuta wakulima wa jamii ya Wasukuma zaidi ya 100 wakiwa na silaha za jadi.

  Alisema mmoja wa askari aliwaamuru kutoka haraka, lakini Wasukuma hao walikahidi na kuendelea kuwaita askari na mgambo kufika katika eneo hilo na kuanza kuwazingira.

  Alisema kutokana na hali hiyo, askari walifyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanya, lakini Wasukuma hao waliendelea kukahidi na kwamba mmoja wao, alimfata askari mmoja na kumpiga bakora kichwani na kuanguka chini huku wenzake wakitaka kuipora bunduki aliyokuwa nayo.

  Diwani huyo alisema baada ya kuona hivyo, askari huyo kwa kujihami alianza kuwapiga risasi Wasukuma hao na kuwaua watano huku wengine wakijeruhiwa, hatua iliyowalazimisha wengine kukimbia.

  Tila alisema kuwa tayari ndugu wa marehemu hao wameshafanya taratibu za mazishi baada ya miili hiyo kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Lugala.

  Hata hivyo, diwani huyo alisema askari hao walitumia nguvu kubwa kwani walikuwa na uwezo wa kuwapiga risasi marehemu sehemu ambazo zisingeweza kuwasababishia maafa na kuongeza kuwa kutendo hicho kinaweza kuongeza uhasama kati yao, wafugaji na wakulima katika tarafa ya Malinyi.

  Tila alikiri kuwa wafugaji hao wameingiza mifugo yao katika kitalu cha Magumba karibu na eneo la wafugaji hao na kwamba lingine linatumiwa na wakulima kwa shughuli za kilimo, lakini makundi yote yaliamriwa kuondoka katika eneo hilo.

  Akizungumza huku akiwa amelazwa hospitalini, mmoja wa majeruhi Shina Msheshiwa, alisema kuwa waliamua kupigana na askari hao baada ya kuwatesa kila wanapowakamata na kuchukua fedha zao huku wale wasiotoa fedha kuteswa na askari hao.

  Msheshiwa alisema kuwa baada ya kuona askari hao wanaendeleza vitendo hivyo, waliamua kupambana nao, lakini alikana kukahidi amri ya kuwataka waondoke baada ya kupigwa risasi hewani.


  KAULI YA RC


  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, aliliambia NIPASHE kwa simu kutoka wilayani Kilombero kuwa hadi jana jioni hali ya usalama ilikuwa shwari katika eneo hilo.

  Bendera aliongeza kuwa hakuna uvunjifu wa amani na kwamba wananchi wamerudi katika maeneo yao.

  Hata hivyo, alisema kuwa kwa wakati huo asingeweza kuzungumzia zaidi suala hilo kwa kuwa tayari ameshamuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Francis Miti na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamis Seleman, kwenda katika eneo la tukio na baadaye kumpa taarifa.


  Imeandikwa na Idda Mushi, Fitina Haule na Ashton Balaigwa, Morogoro.


  SOURCE: NIPASHE
   
Loading...