Mauaji Tarime: Mwenyekiti Halmashauri Tarime Vijijini adaiwa kuua na kufadhili msiba kukwepa mkono wa Sheria

nokwenumuya

Senior Member
Jun 29, 2019
165
500
MWENYEKITI HALMASHAURI TARIME VIJIJINI ADAIWA KUUA, KUKWEPA MKONO WA SHERIA NA KUMALIZANA NA FAMILIA NA KUFADHIRI MAZISHI.

Tarime, 16 May 2021

Mnamo tarehe 15 May 2021, majira ya saa 12 asubuhi katika mtaa wa starehe, kuliko na ofisi za Serikali ya Mtaa wa Starehe, jengo ambalo ni mali ya Edward Empire, ambapo pia amepangisha wapangaji wengine akiwepo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime Vijijini, ambaye amepanga vyumba na kuweka stoo za vinywaji baridi anavyouza katika maduka yake, alipatikana kijana mmoja kwa jina Steven, mwenyeji wa Mkoa wa Kigoma anayeishi kwa kaka yake ambaye ni Mwalimu katika shule ya Secondari Rebu, kwa jina Nelson Makoro 0767646777 Kijana huyo alikutwa na Mwenyekiti wa Mtaa akiwa amefungua Stoo za Mwenyekiti huyo na kuanza kuhamishia vinywaji katika jiko tayari kwa ajili ya kuviiba.

Baada ya Mwenyekiti wa Mtaa kumkuta na kwa kuwa hamfahamu ikabidi ampigie simu mmiliki wa Jengo, simu yake haikupaikana, akampigia Meneja wa mmiliki wa Jengo akampata na kumsimulia juu ya kijana huyo. Naye meneja akampigia Mwenyekiti wa Halmashauri, Mh. Simion Kiles, ambaye ni maarufu kwa jina la K. K akafika pale na mhasibu wake na kumkuta kijana ambaye alikuwa na kopi ya funguo za stoo zake, ambaye inasemekana amekuwa na tabia ya kudamka mara kadhaa mapema asubuhi baada ya mlinzi kuondoka, na kufungua stoo na kuchukua katoni kadhaa za vinywaji.

MWENYEKITI AKABIDHIWA MTUHUMIWA STEVEN ILI AMPELEKE POLISI

Baada ya mazungumzo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Starehe akamuagiza mjumbe aitwaye Boazi, amuandikie barua mhasibu wa Mh. Simion Kiles barua ya kumtambulisha Polisi ili aweze kwenda na mtuhumiwa huyo kwa ajili ya mahojiano juu ya matukio ambayo amekuwa akifanya ya kumuibia katika stoo zake na jinsi alivyopata nakala ya funguo zake za stoo. Akaandikiwa barua na Mh. Simion Kiles, mhasibu wake na mtuhumiwa Steven wakaondoka majira ya saa moja asubuhi na Bajaj ya Mh. Simon kuwa wanaelekea Polisi. Hii ilikuwa tarehe 15 May 2021

STEVEN AOKOTWA AKIWA HOI, APELEKWA HOSPITAL NA KUFARIKI

Siku hiyo hiyo majira ya saa 9 mchana, Polisi wanasema walipigiwa simu na kutaarifiwa kuna mtu yuko hoi, amepigwa na amejeruhiwa. Polisi wakafika eneo la tukio, wakamchukua Steven akiwa Hoi, wakampeleka Hospital ya Wilaya ya Tarime na muda mfupi akafariki.

NDUGU YAKE AMTAFUTA, BAADAE AFANYA MAKUBALIANO NA MH, SIMON KILES

Ndugu yake ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Rebu Sekondari 0767646777 alipopata taarifa kuwa mdogo wake amekamatwa alienda Polisi, Wakamtaarifu kuwa mdogo wake alikuwa mwizi na inaonekana kapigwa na sasa kafariki.

Mwalimu huyo akaja juu kuwa kwa mujibu wa taarifa mdogo wake alikabidhiwa kwa Mh. Kiles akiwa hai na kuwa ampeleke Polisi, je kwa nini hakumpeleka Polisi na baadae akutwe amepigwa hadi mauti?

MH. KILES NA NDUGU WA MAREHEMU WAKUBALI KUYAMALIZA NJE YA MKONO WA SHERIA

Baada ya mazungumzo, ambayo watu wengi hawayajui kiundani Mwalimu ambaye ni Ndugu wa Marehemu Steven alikubali wayamalize, Mh. Kiles akampatia pesa awatumie wazazi wa Steven ambao wanaishi Kigoma waje Bunda mkoani Mara ili waweze kumzika huko ambako kaka yake Steven anaishi.

MH. KILES AFADHIRI MSIBA, ANUNUA JENEZA, CHAKULA CHA MSIBA NA KUKODI COSTA, MAZISHI KUFANYIKA WILAYANI BUNDA KESHO, TAREHE 17 MEI 2021.

Baada ya kutoa nauli wazazi waje Bunda, Mh. Kiles amenunua jeneza, kakodi gari aina ya Costa kwa gharama ya 300,000/- ya kupeleka msiba Bunda kesho Jumatatu, Mei 17, 2021 kwa ajili ya mazishi. Pia ametoa pesa ya chakula na mahitaji mengine kwa ajili ya kuendesha msiba huo.

OMBI KWA SERIKALI NA VIONGOZI

Huyu Mh. Simon Kiles amekuwa mtu wa kuonea watu, katika kituo chake cha mafuta kiitwacho Magere Filling Station, ana chumba ambacho anakitumia kama sero, na pindi akiwa na mgogoro na wafanyakazi wake huweza kuwapiga, kuwaweka sero kwa siku hadi nne ndipo huwaachia na kuwafukuza kazi.

Jambo hili la yeye kujichukulia sheria mkononi na kuua mtu kwa sababu ana pesa za kuweza kuhonga baadhi wa watendaji wa serikali na kuitisha au kuisababisha familia ikubali kuyamaliza nje ya Mahakama inafaa kukomeshwa.

Na kwa kuwa mwili unachukuliwa kesho 17 Mei 2021 saa 3 asubuhi, katika miochwari ya Sirari Tarime ambako mwili umehifadhiwa baada ya majokofu ya Tarime Mjini kuharibika, ili kupelekwa Bunda, tunaomba serikali iingilie kati na mwili huo ufanyiwe Postmortem, Kiles na Mhasibu wake wakamatwe na Uchunguzi ufanyike. La sivyo vifo vya kuua watu na kujichukulia sheria mkononi havitaisha Tarime.

UPDATES
Usiku huu Bwana K na washirika wake wanapanga mipango kuiba mwili mochwari na kwenda kuutupa mto Mara au sehemu yoyote ili kuficha ushahidi.


UPDATES

Haki imetendeka Tarime. Hatimaye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Tarime Vijijini amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua kijana Steven, ambaye alikuwa mtuhumiwa wa kuiba mali katika stoo zake.
 

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,493
2,000
Hili suala la mdogo wako kuuliwa kisha ufanye mazungumzo siyo rahisi, najua hata wewe mleta mada huwezi, yawezekana kuna siasa mnataka kuzipitishia katika hili.
Kama dogo alidakwa ready handed akikwiba,na ushahidi upo wa kutosha,huyo aliyeibiwa na kumuadhibu hadi kupelekea kifo chake alikosea kiasi fulani,ila pia yawezekana kuwa huyo kaka yake na mwizi labda alishachoshwa na tabia ya wizi ya mdogo wake,ndiyo maana akakubali tu kuchukua mpunga kutoka kwa mwenyekiti muuaji,angeweza kuchomwa moto na raia wenye hasira kali na kaka wala wazazi wake wasiambulie chochote,the bottom line ni kwamba marehemu kafa kwa upuuzi wake mwenyewe,kwa nini aibe?
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
12,665
2,000
Japokua Ni kinyume na sheria,
ila Naungana na mwenyekiti wa halmashauri!

Wezi dawa yao wauawe TU, Haina namna

Unapelekea mwizi polisi mwezi Mei,

Mwezi Juni anahukumiwa jela.

Kisha novemba (miezi 5 baadae) siku ya Uhuru anapata msamaha wa raisi.

Anarudi Tena mtaani kanenepa kutuibia zaidi,

Huu upuuzi haukubaliki hata kidogo
 

nokwenumuya

Senior Member
Jun 29, 2019
165
500
Japokua Ni kinyume na sheria,
ila Naungana na mwenyekiti wa halmashauri!

Wezi dawa yao wauawe TU, Haina namna

Unapelekea mwizi polisi mwezi Mei,

Mwezi Juni anahukumiwa jela.

Kisha novemba (miezi 5 baadae) siku ya Uhuru anapata msamaha wa raisi.

Anarudi Tena mtaani kanenepa kutuibia zaidi,

Huu upuuzi haukubaliki hata kidogo
Utawala wa sheria mkuu. Ni kweli dogo kakosea na ndio maana Polisi na Mahakama zipo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom