Mauaji Tarime: Barrick inapata tabu na kuulizwa nje na sio Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji Tarime: Barrick inapata tabu na kuulizwa nje na sio Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, May 23, 2011.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,164
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Barrick yashangazwa na mauaji
  Kampuni ya African Barrick North Mara imesema inapata tabu kila yanapojitokeza matukio ya ukiukwaji haki za binadamu na mauaji, huku akionyesha kuwalaumu polisi.

  Meneja Mawasiliano wa African Barrick, Teweli Teweli alisema kampuni yake imeingia mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu, hivyo matukio kama hayo yanawapa tabu nje ya nchi.

  "Kampuni iligharamia mafunzo yaliyoshirikisha makamanda mbalimbali na kufanyikia Mwanza na wataalamu kutoka Canada waliwajengea uwezo namna ya kukabiliana na uhalifu kwa kuzingatia haki za binadamu. Yanapotokea mauaji tunaulizwa sana nje, tukiambiwa kuwa tunakiuka haki, maana wanajua sisi ndiyo tunafanya," alisema Teweli.


  Source: Mwananchi 23/05/2011

  My take: Kumbe Serikali yetu huwa haiulizi chochote kuhusiana na mauji ya Wananchi achilia mbali kuwapa taabu. Hakika tumekwisha na tunahitaji ufumbuzi wa haraka wa kulitatua hili.

  CHADEMA nawaunga mkono kwa move mliyoanzisha. Tupo pamoja, kwani Serikali imenyamaza na haiulizi chochote hadi pale Obama na Cameroon waulize.
   
 2. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Serikali huwa haiwaulizi bali anatetea mauaji ya raia wake.
   
 3. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Yale yale ya Pesa za Rada!
  Kwamba viongozi wetu kama mazezeta wanaona mambo yanatukia lakini wamenyaza tu kama vile ni MAJUHA fulani vile!
  Ukitoka mgawo ni wa kwanza kukomaa.

  Wewe unafikiri issue ya Tarime ingelikuwa ni mgawo wa kupewa mapande wa Dhahabu pangelikuwa hapatoshi. Lakini kwasababu ni wananchi ambao wao viongozi wetu majuha wanasema hao waliouawa ni ''majambazi'' ndiyo maana wako kimya huku wakiendesha kampeni za chinichini za kutoa sanda na rambirambi za kuwazika haohao wanaowaita ''majambazi''

  Hakika Nchi hii inaongozwa na MAJUHA!
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,164
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Kwenye hiyo red nadhani pangekuwa hapatoshi Tarime, Kuanzia juu hadi chini, we check tu Samunge kwa babu, hadi barabara.
   
Loading...