Mauaji Pwani: Ikwiriri, Kibiti, Njopeka kutembea mwisho saa 3 usiku

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,988
1,209
Wana jamvi habari ya jioni awali ya yote niwape pole kwa kazi za kila siku za kulijenga taifa na pia kuzijenga familia zetu.

Ndugu zangu maeneo hayo niliyoyataja ambayo yapo mkoa wa Pwani hali ni tete baada ya viongozi wa serikali za vijiji kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambao mpaka ninapo andika taarifa hakuna aliyekamatwa.

Kuna viongozi takribani watatu serikali za vijiji wamepoteza maisha yao na wahusika hawajakamatwa bado.

Nadhani huu ni muendelezo wa majambazi ambayo yalikamatwa vikindu na moja lilitoroka baada ya kumuua kiongozi wa msafara katika shambulio hilo.
Kwa mjibu wa baadhi ya jamaa waliotembea maeneo hayo wanadai kuwa askari wamemwaga sana katika eneo hilo lakini ajabu ni kwamba bado mauaji yanaendelea.
Inasemekana usiku wa kuamkia juzi majambazi hayo yalipanga magogo katika kona ya kuelekea Hospital ya Songa na kupora wasafiri vitu mbalimbali ikiwa pamoja na fedha wakitumia mapanga na kuwajeruhi wasafiri takribani 8 ambao wamelazwa Hospital ya Songa.

USHAURI KWA SERIKALI.

Tanzania imekuwa ni nchi ambayo ulinzi wa mipakani ni dhaifu sana kiasi ambacho wageni wanaweza kuingia na kutoka kadri wanavyoweza bila ya shida yeyote hivyo nashauri serikali iimarishe ulinzi wa mipakani.

USHUHUDA.

Nimewahi kisafiri kutoka Nairobi kupitia Namanga na kutoka Mombasa kupitia Holili unapokuwa Kenya au Uganda wenzetu wako makini basi linaposamishwa basi katika vizuizi wanakagua kila mtu kitambulisho lakini ukiingia huku kwetu wanakagua kwa kutazama sura.

SIYO INCHI YA AMANI TENA.

Tanzania siyo ichi ya amani tena kama majambazi yaliweza kuvamia vitu vya polisi Ikwiriri Kimanzichana na baadaye Sitaki shari katikati ya jiji bila kukamatwa tunatarajia nini ni kweli tuko salama hapana.

Serikali imechukua hatua gani kukabiliana na uhalifu huu jibu ni kwamba hakuna bado tumebweteka tuu Tanzania sasa hivi unaweza kuizunguka yote kwa kutumia gari dogo kutoka na miundombinu ilivyoboreshwa.

WAKIMBIZI.

Nchi hii sasa hivi imejaa wakimbizi kila kona lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na wakimbizi hawa wanatoka katika nchi ambazo haziko salama kabisa asilimia kubwa ya wanaofanya biashara ya matunda ni wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda na hata wale ambao wanauza kahawa pia asilimia kubwa ni wakimbizi.

Magereji ya magari hasa ya watanzania wenye asili ya kisomali yanahifadhi wakimbizi wa kisomali magodown yote yamejaa wahindi maafisa uhamiaji wakienda kazi yao kubwa ni kuchukua rushwa na kurudi.

Tumeshuhudia juzi hapa watanzania waliokuwa wakiishi nchini msumbiji bila ya utaratibu wakirejeshwa sisi tunangoja nini ujambazi utaishaje?

Viongozi pangeni mkakati wakuifanya Tanzania endelee kuwa na amani hali iliyopo sasa inatisha kuna kipindi ujambazi ulikuwa unatisha lakini IGP Mwema alifanya kazi kubwa kuutokomeza IGP Mangu kaza buti vinginevyo kazi inakushinda.

img-20170329-wa0038-jpg.488589
 
Mkuu hao wanaoteka magari ni majambazi. Wale wanaoua viongozi sio majambazi ni Waislamu wenye msimamo mkali dhidi ya serikali za vijiji na viyongoji. Ni kweli wako connected na organized kiasi kuwa polisi hawajaweza kuwakamata. Niliwahi kuishi vijiji vya huko nimeona nankuyasikia haya mauaji sana tu tangu mwaka jana.

Hata leo kwenye taarifa ya Habari ITV nimeona mauaji yametokea ya kiongozi wa CCM.

Polisi wanahitaji kutumia mafunzo yao vyema na sio kukaa vituoni huku wamejazana mamia na mauaji yanatokea ni aibu kwa jeshi letu.

Kwa sasa siko huko tena hivyo naomba Polisi msinitafute maana kule kijijini mmekamata watu wengi wasiohusika huku wahusika wakiwazidi ujanja. Ni hayo tu
 
Sasa mkuu shida yangu ni kwanini muda wote huu bado jeshi linashindwa kuwadhibiti tatizo tunafanya kazi ya zimamoto utakumbuka hata wale wa mwanzo ndiyo walikujajulikana kwamba ndiyo waliyoiba benk ya nmb Mkulanga na walikutwa na pesa nyingi
 
Waharabu kutafuta chanzo cha kuuwawa hao viongozi
Tatizo letu badala ya kutafuta chanzo cha tatizo tunakimbilia matamko?!nadhani haya yanayoendelea mkoa wa pwani sio ujambazi ni kama ugaidi fulani hivi! Sasa leo eti unakuja na tamko kuwa kuanzia sasa boda boda mkoa wa pwani mwisho saa 12 jioni!! Kweli ndio suruhisho hili?? Tafuteni mzizi wa tatizo ni nini?
 
Hao watu wakamatwe Mara moja!! Wananchi toeni taarifa vituoni ili hao wapuuzi wakamatwe Mara moja
Inasemekana kuna kiongozi mmja amelazwa Mchukwi anawaelewa na kwa sasa analindwa na Polisi ila polisi wachunguze chanzo chake ni nini kwa nini wauwawe viongozi tu kitu gani kilichojificha nyuma ya mauaji haya?
 
Wana jamvi habari ya jioni awali ya yote niwape pole kwa kazi za kila siku za kulijenga taifa na pia kuzijenga familia zetu.

Ndugu zangu maeneo hayo niliyoyataja ambayo yapo mkoa wa Pwani hali ni tete baada ya viongozi wa serikali za vijiji kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambao mpaka ninapo andika taarifa hakuna aliyekamatwa.

Kuna viongozi takribani watatu serikali za vijiji wamepoteza maisha yao na wahusika hawajakamatwa bado.

Nadhani huu ni muendelezo wa majambazi ambayo yalikamatwa vikindu na moja lilitoroka baada ya kumuua kiongozi wa msafara katika shambulio hilo.
Kwa mjibu wa baadhi ya jamaa waliotembea maeneo hayo wanadai kuwa askari wamemwaga sana katika eneo hilo lakini ajabu ni kwamba bado mauaji yanaendelea.
Inasemekana usiku wa kuamkia juzi majambazi hayo yalipanga magogo katika kona ya kuelekea Hospital ya Songa na kupora wasafiri vitu mbalimbali ikiwa pamoja na fedha wakitumia mapanga na kuwajeruhi wasafiri takribani 8 ambao wamelazwa Hospital ya Songa.

USHAURI KWA SERIKALI.

Tanzania imekuwa ni nchi ambayo ulinzi wa mipakani ni dhaifu sana kiasi ambacho wageni wanaweza kuingia na kutoka kadri wanavyoweza bila ya shida yeyote hivyo nashauri serikali iimarishe ulinzi wa mipakani.

USHUHUDA.

Nimewahi kisafiri kutoka Nairobi kupitia Namanga na kutoka Mombasa kupitia Holili unapokuwa Kenya au Uganda wenzetu wako makini basi linaposamishwa basi katika vizuizi wanakagua kila mtu kitambulisho lakini ukiingia huku kwetu wanakagua kwa kutazama sura.

SIYO INCHI YA AMANI TENA.

Tanzania siyo ichi ya amani tena kama majambazi yaliweza kuvamia vitu vya polisi Ikwiriri Kimanzichana na baadaye Sitaki shari katikati ya jiji bila kukamatwa tunatarajia nini ni kweli tuko salama hapana.

Serikali imechukua hatua gani kukabiliana na uhalifu huu jibu ni kwamba hakuna bado tumebweteka tuu Tanzania sasa hivi unaweza kuizunguka yote kwa kutumia gari dogo kutoka na miundombinu ilivyoboreshwa.

WAKIMBIZI.

Nchi hii sasa hivi imejaa wakimbizi kila kona lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na wakimbizi hawa wanatoka katika nchi ambazo haziko salama kabisa asilimia kubwa ya wanaofanya biashara ya matunda ni wakimbizi kutoka Burundi na Rwanda na hata wale ambao wanauza kahawa pia asilimia kubwa ni wakimbizi.

Magereji ya magari hasa ya watanzania wenye asili ya kisomali yanahifadhi wakimbizi wa kisomali magodown yote yamejaa wahindi maafisa uhamiaji wakienda kazi yao kubwa ni kuchukua rushwa na kurudi.

Tumeshuhudia juzi hapa watanzania waliokuwa wakiishi nchini msumbiji bila ya utaratibu wakirejeshwa sisi tunangoja nini ujambazi utaishaje?

Viongozi pangeni mkakati wakuifanya Tanzania endelee kuwa na amani hali iliyopo sasa inatisha kuna kipindi ujambazi ulikuwa unatisha lakini IGP Mwema alifanya kazi kubwa kuutokomeza IGP Mangu kaza buti vinginevyo kazi inakushinda.
IMG-20170329-WA0038.jpg
 
Mkuu hao wanaoteka magari ni majambazi. Wale wanaoua viongozi sio majambazi ni Waislamu wenye msimamo mkali dhidi ya serikali za vijiji na viyongoji. Ni kweli wako connected na organized kiasi kuwa polisi hawajaweza kuwakamata. Niliwahi kuishi vijiji vya huko nimeona nankuyasikia haya mauaji sana tu tangu mwaka jana.

Hata leo kwenye taarifa ya Habari ITV nimeona mauaji yametokea ya kiongozi wa CCM.

Polisi wanahitaji kutumia mafunzo yao vyema na sio kukaa vituoni huku wamejazana mamia na mauaji yanatokea ni aibu kwa jeshi letu.

Kwa sasa siko huko tena hivyo naomba Polisi msinitafute maana kule kijijini mmekamata watu wengi wasiohusika huku wahusika wakiwazidi ujanja. Ni hayo tu
Huku kuhitimisha kuwa waislam ndio wamefanya ndio kupoteza ushahidi kwenyewe. Wewe mwenyewe unahisi umetema bonge la pwenti
 
Wajitambulish ebasi tuwajue kama niIslamic state au al kaeda ama al shababi
 
Mkuu hao wanaoteka magari ni majambazi. Wale wanaoua viongozi sio majambazi ni Waislamu wenye msimamo mkali dhidi ya serikali za vijiji na viyongoji. Ni kweli wako connected na organized kiasi kuwa polisi hawajaweza kuwakamata. Niliwahi kuishi vijiji vya huko nimeona nankuyasikia haya mauaji sana tu tangu mwaka jana.

Hata leo kwenye taarifa ya Habari ITV nimeona mauaji yametokea ya kiongozi wa CCM.

Polisi wanahitaji kutumia mafunzo yao vyema na sio kukaa vituoni huku wamejazana mamia na mauaji yanatokea ni aibu kwa jeshi letu.

Kwa sasa siko huko tena hivyo naomba Polisi msinitafute maana kule kijijini mmekamata watu wengi wasiohusika huku wahusika wakiwazidi ujanja. Ni hayo tu
Thibitisha kuwa ni Waislam wenye msimamo mkali, au tupe maelezo yenye rejea kuhusu misimamo ya waislam kwa uoni wa Waislamu. La sivyo futa kauli yako yenye harufu ya udini.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu hao wanaoteka magari ni majambazi. Wale wanaoua viongozi sio majambazi ni Waislamu wenye msimamo mkali dhidi ya serikali za vijiji na viyongoji. Ni kweli wako connected na organized kiasi kuwa polisi hawajaweza kuwakamata. Niliwahi kuishi vijiji vya huko nimeona nankuyasikia haya mauaji sana tu tangu mwaka jana.

Hata leo kwenye taarifa ya Habari ITV nimeona mauaji yametokea ya kiongozi wa CCM.

Polisi wanahitaji kutumia mafunzo yao vyema na sio kukaa vituoni huku wamejazana mamia na mauaji yanatokea ni aibu kwa jeshi letu.

Kwa sasa siko huko tena hivyo naomba Polisi msinitafute maana kule kijijini mmekamata watu wengi wasiohusika huku wahusika wakiwazidi ujanja. Ni hayo tu
we bhn waislam na mauwaji ya viongoz wa kichama wap na wap..acha kupandikiza chuki..ukishaona mauaji ya kichama ujue ni wao wenyewe ktk vyama vyao..unaongea km umelewa ..pointless kbsa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Askari watu wanahitaji kuwezeshwa kizana, kitaaluma na kimwili ili kutimiza lengo la kulinda raia na mali zao.
Poleni ndugu zetu.
Hao mabandidu wasipodhibitiwa haraka hii mambo inaweza kukopiwa ma kupestiwa mikoa na wilaya zingine ulipizaji visasi wa jinsi hii ukawa oder of the conflict.

Nashauri yule aliyemtolea na kumyooshea bastola Nape Nnauye apelekwe huko!!!
 
Huyu anachanganya mada.Tueleze wanaofanya ujambazi ni wahamiaji haramu?Na kwanini husitoe taarifa ktk chombo husika?Na unauhakika gani kama ukaguzi ni lege lege ktk maeneo ya mipaka yetu?Mfano ukitokea namanga gari zinakaguliwa na maafsa wa uhamiaji,ukifika longido kuna ukaguzi ukikaribia Arusha ipo beria hao unaowaona wanapitia wapi?Hebu tueleze ili kazi ifanyike vyema.Vile vile ukitokea horohoro duga maforoni ni lazima ukaguzi ufanyike na sehemu nyinginezo.Mimi ninaona swala la pwani ni swala la majambazi sugu wanaojificha ktk sehemu hizo.Halafu hivi huyo mgeni gani ataingia hadi vijijini na kuwauwa wenyeviti tu?jiulize mwenyewe.
 
Back
Top Bottom