Mauaji Mkuranga: Dereva wa bodaboda akatwa mapanga na kufariki

shaks001

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
1,246
1,070
Jioni hii ya saa moja kijana mmoja dereva wa bodaboda ameuwawa kwa kukatwa-katwa mapanga na kutolewa utumbo nje baada ya kukodiwa na mwanamke ampeleke sehemu.

Chanzo cha habari cha kuaminika kinasema mauaji hayo yametokana na wivu wa mapenzi baada ya mume wa huyo dada aliyekodi bodaboda hiyo kuhisi kuwa dereva huyo ana mahusiano ya kimapenzi na mke wake huyo.

Ilipofika mida ya jioni hii saa 1,inavyosemekana dada huyo alikwenda mpaka kijiwe cha bodaboda(mgundini)ambacho jamaa huyo anapaki na kumkodi(Haijulikani ilikuwaje dada huyu akaamua ampeleke "bwana ake"huyo kwa mumewe) na kumpeleka maeneo ya pori lenye utulivu na kumkuta mume huyo kando ya barabara na ndipo mume huyo akatekeleza mauaji hayo kwa kumkata-kata mapanga dereva huyo kuanzia mikononi na hatimaye kumtoboa tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumwaga utumbo nje.

Baada ya tukio mwanamke alianza kukimbia kama kachanganyikiwa na baadae alikamatwa na wananchi kijiji kinachofuata,na kwa maelezo ya awali mtuhumiwa anadai walikuwa wawili(yeye na mumewe)tu,katika tukio hilo na mumewe ndie aliyemtoa uhai dereva huyo.Mwanamke yupo chini ya ulinzi kituo cha polisi Mkuranga.

Nili-Google nikaandika "most dangerous animals in the world,nikakuta binadamu yupo kwenye top ten.Nilijiuliza sana kwa nini binadamu kawekwa kwenye kundi la wanyama wakali duniani,sasa nimeanza kujua.Ni bora ukutane na chui porini anaweza akakuonea huruma na si baadhi ya binadamu.
 
Kuna watu wengine huwa hawawezi kuwa na option ya kuoa mke mwingine, wao huwa wanabakiwa na option moja tu ya kufa yeye au kumuua mwenzake
 
Sasa kama mke ndio anayechepuka,mwenye kosa sio jamaa wa bodaboda bali ni uyo mwanamke
 
Back
Top Bottom