Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, amemuondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Nsimeki kwa kushindwa kudhibiti matukio ya uhalifu likiwamo wimbi la mauaji ya watoto, mkoani humo hivi karibuni.
Uamuzi huo aliutangaza juzi jioni alipozungumza na wananchi mjini Lamadi Wilaya ya Busega.
Alisema amechukua uamuzi huo baada ya kamanda huyo kulalamikiwa na wananchi kushindwa kudhibiti hali hiyo.
Alisema pamoja na hali hiyo ni lazima kila aliyepewa jukumu ndani ya Jeshi la Polisi atimize wajibu wake ikiwamo kulinda raia na mali zao.
“Kutokana na matukio hayo tayari nimemwondoa aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa, Deusdedit Nsimeki na kumleta mwingine (hakumtaja jina),” alisema IGP Sirro.
Alisema mbali na wananchi kumlalamikia kamanda huyo wa polisi, bado alionekana kushindwa kukomesha matukio hayo, kazi ambayo alitakiwa kuifanya.
“Mbali na nyie kumlalamikia RPC hata alipokuja kwangu nilimuuliza swali moja, wewe nilikuteua kwenda huko kunisaidia kukomesha uhalifu, sasa kwa nini bado matukio yanaendelea? Na mimi nikaona kazi imemshinda,” alisema.
Pamoja na kuchukua uamuzi huo aliwataka wananchi kutowalalamikia askari wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao badala yake wawataje baadhi ya askari wahusika na si jeshi lote.
Hadi sasa imeripotiwa watoto watatu na wanawake wawili wameuawa na kunyofolewa baadhi ya viungo vyao tangu Oktoba 10 mwaka jana hadi mwaka huu.
Matukio hayo yanahusishwa na imani za ushirikina na mpaka sasa watu 12 wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kuhusika katika matukio hayo.
Kabla ya kuzungumza na wananchi hao alifanya kikao cha ndani cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kilichodumu kwa saa mbili.
Sirro alisema tayari ameongeza nguvu kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi kuweza kushughulikia matukio ya mauaji Lamadi.
Aliahidi kukomesha mtandao mzima wa wahalifu.
“Kuna watu bado wanaamini kupata samaki wengi mpaka watumie njia za ushirikina, mimi bado naikumbuka Lamadi hii tabia ilikiwapo zamani na wahusika wakuu walikuwa wazazi wa watoto.
“Sasa nimeagiza, watafutwe hata hao ambao walihusika katika matukio kama haya huko zamani, tuone kesi zao zilienda vipi na tujue wapi tunaanzia, lakini elimu inahitajika zaidi kwa wananchi,” alisema IGP Sirro.
Alisema ndani ya siku 10 atahakikisha wahusika wote wanapatikana na kuchukuliwa hatua za sheria.
- Mtanzania