TUNTEMEKE
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 4,587
- 579
Tunapaswa kujifunza demokrasia upya, najiuliza nini maana ya Freedom of expresion?
Tukiwazuia watu kuongea what we call siri katika media ni sawa? Maana kama chama kinarumika na CCM wasiseme? Ukiona Mbatia anafanya jambo ujue wakubwa zake wa kazi wamekwishampa go ahead, katika kesi ya kawe Mh. Mdee na mawakili wake walifanya juhudi hadi muda wa kesi ukaisha bila kesi kusikilizwa, lakini Kombani kawaongezea muda kusikiliza kesi hiyo kwani lazima lirudi CCM kwa kutumia kesi ya Kijana wao Mbatia.
Katika sakata la Kafulila, wajumbe walibadilishwa na nakala ikapelekwa kwa Msajili wa Vyama siku mbili kabla ya NEC ya dharura, Rungwe alipoenda kupinga akakuta Tendwa ana updated list ya Wajumbe na wengine wamefutwa na kuweka wapya ili wapige kura kwa adhma ya kuwafukuza waliompinga Mwenyekiti.
Hiyo haikutosha bali watu walilazimishwa kupiga kura kwa kunyanyua mikono, kwa ile fukuza wajumbe wengi wanakiri kuwa waliogopa na kwa kuangalia maslahi yao waliamua kunyoosha mikono kwa lazima.
Je madai ya Rungwe kuwa Mbatia alimzuia kuisema CCM katika uchaguzi wa mwaka jana ndio yameisha? Rungwe alikiandikia chama barua kulalamikia hatua hiyo, je majibu ya maswali hayo ndiyo hayo?
Kafulila alikataa kwenda kumuona Rais, masaa machache baada ya kufukuzwa chama kimepata mwaliko wa ikulu, je kuna shinikizo toka juu?
Tendwa na Nape wamezungumzia gharama za Uchaguzi mdogo kuwa utakuwa na gharama kubwa, tumeshuhudia katika uchaguzi wa Igunga mauaji na watu kujeruhiwa kutokana na mchakato ule wa uchaguzi, je hatuangalii gharama ya damu za watanzania wenzetu inayoweza kumwagika kigoma kusini kwenye uchaguzi huo mdogo kama ukitokea?
Mauaji hayo nani alaumiwe? Je, damu ya watu watakaopoteza maisha katika uchaguzi wa kigoma kusini kama ukitokea uwe juu ya kichwa cha Mbatia na genge lake?
Je, kuwa na uvumilivu wa kisiasa na kuwajibika katika changamoto zinazokukabili haina faida kubwa kuliko kuweka maisha ya watu katika hatari na kupoteza muda katika chaguzi?
Bilioni 19 zitakazotumika katika uchaguzi zingetumika kulipa madeni ya waalimu, je tatizo s lingepungua?
Tafakari chukua hatua!