Mauaji Igunga: Watuhumiwa ni ccm - Mbona wako kimya ?

RMA

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
409
87
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinahusika na kifo cha wakala wake aliyepotea tangu Oktoba 2, mwaka huu na mwili wake kuokotwa Agosti 9, mjini Igunga mkoani Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi wa CHADEMA, Benson Kigaila, alisema mazingira ya kifo cha kada huyo, Mbwana Masoud Mbwana, yanaonyesha dhahiri kuwa CCM kimehusika na kifo hicho.
Alisema mwili wa marehemu haukuwa umeharibika, hali inayoonesha kuwa marehemu alitekwa usiku wa kuamkia Agosti 2, na kushikiliwa mahali fulani ambako aliteswa kwa kumpiga vibaya, na kwamba aliuawa siku chache kabla ya mwili wake haujatupwa katika msitu wa Magereza, ambao hauko mbali na mjini.
“Kama kweli Msoud angeuawa siku aliyopotea, mwili wake ungeharibika sana,” alisema na kuongeza kuwa waliukuta mwili ukiwa na majeraha makubwa kichwani na macho yake yakiwa yametobolewa.
“CCM wamehusika na kifo hicho kwani sote tunajua waliandaa makambi ya vijana waliokuwa wakivamia wanachama wa CHADEMA na kuwajeruhi huku wakiwawinda mawakala wetu,” alisema.
Alisema pamoja na kutoa taarifa za vurugu zinazofanywa na vijana wa CCM kwa polisi, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za kupotea kwa kada wao.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Anthony Rutashuburugukwa, alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu.alipigwa na vitu vyenye ncha kali kichwani na shingo yake kunyongwa.
Kamanda huyo alisema hadi sasa jeshi lake halijapokea rasmi taarifa ya daktari lakini, wanaamini kuwa marehemu aliuawa, na kwamba hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusika na kifo hicho.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA, Jimbo la Ubungo, Ali Makwillo, ambaye aliongozana na ndugu wawili wa marehemu Masoud kwenda Igunga kwa ajili ya kutambua mwili, alisema ni kweli (marehemu) alikuwa ameumizwa vibaya kichwani huku shingo yake ikionekana wazi alinyongwa.
“Baada ya kufika Igunga juzi, wote tulioishuhudia maiti ile tuliona namna marehemu alivyojeruhiwa vibaya huku shingo yake ikionekana kulegea sana,” alisema Makwillo.
Makwillo alisema baada ya kuona vile, waliomba ripoti ya uchunguzi kwa daktari ambaye aliwanyima na kuwaeleza kuwa si yao bali wataikadhi polisi. “Lakini alivyoona tunang’ang’ania sana kudai ripoti alitueleza kuwa jamaa yenu kauawa kwa kupingwa na vitu vyenye ncha kali na kunyongwa ...nendeni mkaendelee na taratibu zingine,” alisema.
Katibu mwenezi huyo alisema baada ya kupata taarifa hiyo, kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu, viongozi wa dini, viongozi wa chama wilayani, mkoani pamoja na wananchi waliamua kwenda kuuzika mwili wa marehemu uliokuwa umeharibika.
“Tulizika siku hiyo hiyo (juzi Oktoba 10) baada ya kuona mwili wa marehemu Masoud umeharibika... kwa sasa tupo Dodoma tunarudi Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya hitima, ” alisema Makwillo.
Juzi taarifa ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, iliwalaani waliohusika na vitendo hivyo na kuvitaka vyombo vya dola kufanya uchunguzi haraka na kuwakamata wote waliohusika na unyama huo, pia alitoa wito kwa mwananchi yeyote anayetambua chochote kuhusu kifo hicho atoe taarifa kwa vyombo vya usalama na chama chao kwa ufuatiliaji zaidi.
Marehemu Masoud alikuwa ni mmoja wa wanachama waliojitolea kusafiri kwenda Igunga kuwa mawakala kwenye uchaguzi Oktoba 2, 2011 na alitoweka katika mazingira ya kutatanisha wilayani Igunga Septemba 30, walitoa taarifa polisi Oktoba 3, mwaka huu na kufungua jalada RB/748/2011.
 
Lazima watakuwa ni CCM kwani tulishuhudia kati yao wakining'iniza bastola viounoni waziwazi!
 
Magwanda wameanza kuuana wenyewe kwa wenyewe ili waichafue ccm.
 
Damu ya Masoud iliyomwagwa na CCM ndiyo chachu ya mapinduzi halisi ya nchi hii.

Wao wamemua ili wao wastarehe lakini itawatafuna mmoja mmoja mpaka yule gamba kuu na nawahakikishia ya kwamba HAKI ITASIMAMA KAMA HAKI TU HATA IKIPINDISHWA KAMA ILIVYO WAZI PALE IGUNGA HAKIKA MAOVU YA HAWA sisiem MUNGU ATAJIBU KTK KIPINDI KIFUPI SANA.
 
Tunako elekea ni kubaya .Hakuna media wala matamko ya bakwata wala polisi na CCM wenyewe. Haya wacha wakae kimya ila wanaya anza haya huwa yanakuwa mazito baadaye .RIP Mbwana .
 
Back
Top Bottom