MAUAJI DAR: Maiti tatu zadaiwa kuokotwa ufukweni Coco Beach

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
maiti.jpg

Maiti za wanaume watatu zimekutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo kati ya hizo moja imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba.

Wafanyabiashara wa mihogo wa eneo hilo wamesema juzi wakiwa kwenye biashara zao asubuhi ghafla waliona maiti moja ikielea karibu na miti aina ya mikoko ikiwa na jiwe lililofungwa kifuani huku mikono yake ikifungwa na kamba.

Mmoja wa wafanyabiashara, Aziza Ally amesema baada ya kuona maiti hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika saa 4 asubuhi na kuichukua kwenye gari lao.

Amesema ilipofika saa 8 mchana waliona maiti mbili kila moja ikiwa kwenye kiroba zikielea ndipo mmoja wao alitoa taarifa polisi baadaye zilichukuliwa.

"Polisi walipokuja kuchukua hizi maiti hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kusogelea na kupiga picha tulishangaa sana kuona jana ulinzi mkali tofauti na siku zote na aliyebainika amepiga alipokonywa simu yake," amesema Ally.

Mfanyabiashara mwingine Issa Isaya amesema cha kushangaza maiti zinazookotwa ni za kiume pekee hivyo wanaishi kwa wasiwasi kwa kuwa kila wiki wanakuta maiti zikiwa zinaelea kwenye maeneo hayo.

Amesema Septemba 20 mwaka huu maeneo hayo iliokotwa maiti ya kiume iliyofungwa kwenye kiroba ambayo ilikuwa imeharibika .

Isaya amesema maiti hiyo iligunduliwa na wavuvi waliokuwa wanavua samaki ambao huwa wanatoa taarifa kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.

Amesema mwanzo alikuwa anapata shida alipokuwa anaona maiti katika eneo hilo hivyo kwa kuwa kila wiki wanaokota maiti amelazimika kuizoea hali hiyo.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne amesema tukio hilo atazungumzia Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Alipotafutwa Kamanda Mambosasa amesema hajapata taarifa ya kuokotwa maiti hizo hivyo anafanyia uchunguzi na atalitolea ufafanuzi leo.

"Sina taarifa na hilo hivyo nalifanyia kazi taarifa nitatoa kesho," alisema Mambosasa.

Chanzo: Mwananchi
 
Sijui imekuaje naanza kukumbuka Znz ya Abeid Karume,
Watu walitoswa baharini wakafungwa na Vyuma wasieleee then wakatafutwa Watu wakaanza Eti kuhojiwa kuhusu Watu Hao Hao waliotoswa baharini halafu wakafunguliwa mashtaka ya Mauaji na wakanyongwa huku anaetuhumu na kuhukumu ndie alieua wale waliokufa awali!

Wako wapi waliokuwa wanataka tupate Rais Kama Kagame maana wamejificha hawajitokezi Tena kutuambia Kama kishapatikana au tueendelee na Maombi
 
Makonda hutomsikia akihangaika na hili na uRC wake na hadi sasa huwez ina serikali ukiwa serious na hili jambo,huenda wamefungua dampo kwa ajili ya maiti zisizo na wenyewe. Kule Bagamoyo Mwigulu alisema ile miili name ni wahamiaji haramu,cha kufurahisha hawa kusema wa nchi gani na kwa nini ubalozi wake hawakugaiwa maiti hizo kwa ajili ya kuwaarifu ndugu zao huko!!!
 
Mmmh! Samaki nao hawataki kula watu wasio na hatia
Yule samaki aliyemmeza Yona alimtapika kwenye shore ya bahari. Hawa wameamua kutowameza kwa sababu Roho wa Mungu anawazuia kujiingiza kwenye dhambi hiyo kubwa bali sisi tuko very happy kuwaua wenzetu. Eeeeh Mungu uturehemu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom