MAUAJI DAR: Maiti tatu zadaiwa kuokotwa ufukweni Coco Beach

Sikubaliani kwamba maiti hizo ni za wakosoaji wa serikali kwa sab wanaoikosoa serikali kwa kufikia hatua ya serikali kustuka au kukasirika ni wale wenye wafuasi wengi na wenye convincing power ya kutosha lkn wenye access kubwa kwenye media watu wa namna hiyo wote wanajulikana kwa majina vyeo n.k

Kwa muktadha huo hakuna watu wa namna hiyo walioripotiwa kupotea ambao wanaweza kuakisi hata asilimia tano ya maiti zilizopatikana mpk sasa.
Haiwezekani watu wenye calibre niliyoitaja wapotee kimya kimya never.
Mpk sasa anayesemekana amepotea mwenye calibre hiyo ni Ben saa nane tu.

Ninashawishika kuamini maiti zile zinatoka nje ya Tanzania.
kama wanaweza kuwadhuru wanaojulikana like Tundu Lissu nabkuwapoteza akina Ben saa 8 na kuwateka wasanii maarufu kama Roma,hao ambao hawajulikani unashangaa nn kuwakuta kwenye viroba?, ngojeni siku wakutwe ndugu zenu wa familia moja wamekufa ndo mtaelewa
 
Una ushahidi km hao uliowataja serikali imehusika? Lkn hao uliowataja hawajafa zaidi ya Saa nane ambaye haonekani inafanana na idadi ya maiti za kwenye viroba?
 
naona unaamua kujifanya chizi ili Uzi wako uwe na comments nyingi, baki na ujinga wako kataa hadharan ila moyon unakubali kwamba this gvt is weak one na ndo maana haitak watu waseme na itashangiliwa na wapuuzi tu.
 
Tenda ya ku supply body bags ingelipa sana mwaka huu kama ma polisi wa Bongo wanatumia hiyo kitu
 
Aise kuna haja uchunguzi ufanyike wabainike kina nani wanahusika na matukio haya
Si jambo la kawaida
Wazri wa Ndani Bw. Madilu system Nchemba akiulizwa ni nani waanaouawa na kutupwa baharini anasema ni: WATU WASIOJULIKANA AU WAKIMBIZI TOKA NCHI JIRANI..!!!!??
Hapa Kazi Tu!!!!!l
 
naona unaamua kujifanya chizi ili Uzi wako uwe na comments nyingi, baki na ujinga wako kataa hadharan ila moyon unakubali kwamba this gvt is weak one na ndo maana haitak watu waseme na itashangiliwa na wapuuzi tu.
Haitaki kivipi wakati kila siku press conferences zinaongozana km kukamatwa ni baada ya kuongea uchochezi. Serikali inashindwa mini kuzuia kabla hazijafanyika?
 
Maiti za wanaume watatu zimekutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo kati ya hizo moja imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba.

Wafanyabiashara wa mihogo wa eneo hilo wamesema juzi wakiwa kwenye biashara zao asubuhi ghafla waliona maiti moja ikielea karibu na miti aina ya mikoko ikiwa na jiwe lililofungwa kifuani huku mikono yake ikifungwa na kamba.

Mmoja wa wafanyabiashara, Aziza Ally amesema baada ya kuona maiti hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika saa 4 asubuhi na kuichukua kwenye gari lao.

Amesema ilipofika saa 8 mchana waliona maiti mbili kila moja ikiwa kwenye kiroba zikielea ndipo mmoja wao alitoa taarifa polisi baadaye zilichukuliwa.

"Polisi walipokuja kuchukua hizi maiti hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kusogelea na kupiga picha tulishangaa sana kuona jana ulinzi mkali tofauti na siku zote na aliyebainika amepiga alipokonywa simu yake," amesema Ally.

Mfanyabiashara mwingine Issa Isaya amesema cha kushangaza maiti zinazookotwa ni za kiume pekee hivyo wanaishi kwa wasiwasi kwa kuwa kila wiki wanakuta maiti zikiwa zinaelea kwenye maeneo hayo.

Amesema Septemba 20 mwaka huu maeneo hayo iliokotwa maiti ya kiume iliyofungwa kwenye kiroba ambayo ilikuwa imeharibika .

Isaya amesema maiti hiyo iligunduliwa na wavuvi waliokuwa wanavua samaki ambao huwa wanatoa taarifa kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.

Amesema mwanzo alikuwa anapata shida alipokuwa anaona maiti katika eneo hilo hivyo kwa kuwa kila wiki wanaokota maiti amelazimika kuizoea hali hiyo.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne amesema tukio hilo atazungumzia Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Alipotafutwa Kamanda Mambosasa amesema hajapata taarifa ya kuokotwa maiti hizo hivyo anafanyia uchunguzi na atalitolea ufafanuzi leo.

"Sina taarifa na hilo hivyo nalifanyia kazi taarifa nitatoa kesho," alisema Mambosasa.

Chanzo: Mwananchi
Hii hali ya mauaji ya watu wasiojulikana yamerudi tena upya kama ilivyokuwa enzi za Magufuli. Hii ni dhambi kubwa sana na itaendelea kuitafuna nchi hii hadi Yesu atakaporudi.
 
Back
Top Bottom