Matuta yote barabara kuu za mikoa yaondolewe; vivuko viwekwe vya chini ya barabara watu wakimbize magari wawezavyo bila vikwazo. Itapunguza rushwa pia

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,889
India ina watu wengi mno duniani lakini barabara za mikoa ukiwasha gari unatimua mbio bila shida huoni tuta popote. Vijijini hata kuwe na wafugaji vipi barabara huwa na kivuko chini kipana tu cha kupitisha hadi mifugo kwa hiyo juu yanakuwa yanapita magari tu kwa spidi bila hofu ya kugonga kiumbe aitwaye binadamu au mfugo.

Hii itasaidia pia kupunguza rushwa za barabarani za "ohhh ume overspidi!"

Na wale askari wa tochi si vibaya wakatafutiwa majukumu mengine. Miendo ya taratibu inaharibu magari na kuchelewesha uchumi. Gari imetengezwa na spidi ili zifikiwe, sio urembo.
 
Heee! kwanini usiongee na Magufuli moja kwa moja? Kumbe hauna hata namba yake?

Mbona huwa unabwata sana humu?

Nilijua ni bonge la mtu high profile figure kumbe ngumbaru tu —underdog?

Hivi magufuli analijua hata jina lako wewe?
 
Serikal itapoteza mapato tukiondoa tochi barabaran.

Atasikika mmoja wao akisema hvyo
 
Waziri wa miondombinu wa zamani na sasa ange bahatika kufanya ziara India ingewezekana. Japo jaribu kumtumia video clip fupi mfano kivuko miguu Ujiji anaweza kutoa maelekezo.
 
... nakuunga mkono kwenye hili. Tatizo ni kwamba fine za barabarani ni sehemu muhimu ya mapato ya serikali.
 
... nakuunga mkono kwenye hili. Tatizo ni kwamba fine za barabarani ni sehemu muhimu ya mapato ya serikali.
Kama ndivyo mbona kamanda wa polisi aligoma kwamba hawakupewa limit ya makusanyo kutoka barabarani na akasema kwamba faini za barabara hazitumikki kama chanzo Cha mapato hii wewe umetoa wapi
 
Kama ndivyo mbona kamanda wa polisi aligoma kwamba hawakupewa limit ya makusanyo kutoka barabarani na akasema kwamba faini za barabara hazitumikki kama chanzo Cha mapato hii wewe umetoa wapi
... basi ziondelewe kuwe na adhabu mbadala.
 
Waziri wa miondombinu wa zamani na sasa ange bahatika kufanya ziara India ingewezekana. Japo jaribu kumtumia video clip fupi mfano kivuko miguu Ujiji anaweza kutoa maelekezo.
zinakuwa hivi kama kwenye hii video zinaitwa pedesterian underpass barabara inakuwa juu watu na mifugo wanapita chini kutoka upande mmoja kwenda mwingine

Kama ndivyo mbona kamanda wa polisi aligoma kwamba hawakupewa limit ya makusanyo kutoka barabarani na akasema kwamba faini za barabara hazitumikki kama chanzo Cha mapato hii wewe umetoa wapi
Kwan unapolipa fain ya traffic hiyo fain inaingia wapi? Polisi au hazina?
 
Kwa nchi za wenzetu kuna barabara unaweza kimbiza unavyotaka na kuna zingine zina speed limit....ila kwa upande wa matuta sijaona
Swala la matuta naunga mkono
Ila wenzetu watembea kwa mguu wana heshimu sana vivuko na vivuko vyao vingi ni underground
Tehran tu hapo vivuko vingi ni vya chini

Ova
 
zinakuwa hivi kama kwenye hii video zinaitwa pedesterian underpass barabara inakuwa juu watu na mifugo wanapita chini kutoka upande mmoja kwenda mwingine

Wala usiende mbali kote huko, Iringa ipo moja pale kwenye mlima wa Kisima cha bibi na imeindoa usumbufu wa kundi la watu toka Ipogoro kuvuka barabara!!

Wahehe wameitii, eneo lile huoni mtu barabarani kabisa.
 
Hakuna kitu kizuri kama exposure
Exposure ni zaidi ya mtu mwenye degree bongo
Alafu hajawahi kutoka nje ya nchi

Ova
 
Sawa mkuu kwa upande mmoja wazo lako ni zuri, lakini kiuhalisia matuta yaliwekwa barabarani kwa sababu za kiusalama! Kuna watu usipowawekea vithibiti mwendo wanaweza kuwarukia hata hao wanaovuka chini ya barabara!
 
Hayo matuta ndio yanarusha magari mtu akiwa mwendo kasi kama hajaliona akiligusa gari inaruka na kupaa .Yasipokuwepo ajali zitapungua kwenye barabara za mikoani
 
Heee! kwanini usiongee na Magufuli moja kwa moja? Kumbe hauna hata namba yake?

Mbona huwa unabwata sana humu?

Nilijua ni bonge la mtu high profile figure kumbe ngumbaru tu —underdog?

Hivi magufuli analijua hata jina lako wewe?
Acha dharau ,
Usimfokee,
Heshima maoni ya mtu.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom