Matuta barabarani: Wakazi watumiao Morogoro road walia

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,529
8,614
Wiki kadhaa baada ya TANROADS kutekeleza amri ya rais aliyoitoa alipokuwa akizindua barabara huko shinyanga ..ya kutaka barabara kama ya morogoro road kuanzia chalinze kuwekewa matuta,kutokana na ajali kwenye highway hiyo..wananchi wanaotumia barabara hiyo wamekubwa na kadhia kubwa..

kwa sasa matuta yanaanzia ubungo na yapo kila baada ya hatua chache,kiasi cha kusababisha FOLENI KUONGEZEKA MARA DUFU.......kwa kweli foleni ni kubwa sana wakati wa asubuhi.....ambapo mtu anayetoka kibamba inamchukua hadi masaa 2 ..kuvuka mataa ya ubungo....kwani matuta huamzia sehemu wanayoita mbezi mwisho ..ambapo pia watu wa TRA wameweka kituo chao kisichokuwa na parking na kusababisha msongamano wa malori.....

wakati wa jioni hali ni mbaya na msururu wa foleni usiokuwa na mwisho HUANZIA UBUNGO BILA KUKATIKA HADI KITUO CHA TRA MBEZI..hapo unaambiwa mwendo wa gari lazima uwe 10km/hr........watu waanatumia masaa 2.30...huku wengi wakiwa wamechoka....na kusababisha ONGEZEKO LA AJALI KUTOKANA NA BREKI AU MADEREVA KUSINZIA......pia magari mengine hukatikiwa mafuta yakiwa kwenye foleni au kuharibika na kuzidisha taharuki.....

zaidi ya ajali kuongezeka pia wenye magari madogo kwa makubwa wanalalamikia UHARIBIFU kutokana na bump kuwa triple na karibu karibu mno.......magari yanakata spring...

siku hizi magari kukuta yamepinduka asubuhi ni kawaida kwani hizo bump hazina SIGNS zinazoonekana mchana sembuse zinazoreflect usiku..na kusababisha madereva wanaopita usiku wa manane wakupwa nje ya barabara KILA SIKU...

kwa kifupi tuiangalie uamuzi huu kinyume na ushauri wa wataalamu wa barabara kuwa BUMP ..KWENYE HIGHWAY HAZIFAI.....na huu uamuzi wa kisiasa wa kuingilia utaalamu.......nadhani PIA TUFIKIKIRIE KUWEKA VIVUKO VYA MIGUU VYA FLYOVER AU BRIDGE AU UNGERGROUND..ROAD CROSS AMBAZO NI CHEAP kwenye vijiiji au maeneo yenye wakazi ..ili watembea miguu na waenda magari wote wawe salama kwenye highways...
 
JK alisema Nchi iende kisayansi, kwanini hao maengineer wa TANROAD hawakutumia upenyo huu kubuni njia nyingine zaidi ya hayo matuta...?
 
Asante sana mwenzetu Phillemon Mikael kwa kuanzisha mada hii. Maoni yako kwamba ni vibaya wanasiasa kupuuza ushauri wa wataalamu ni ya muhimu sana. Bumps kwenye highway ni kosa kiafya na hata kiuchumi. Lazima hizo bumps za Morogoro Road zitaleta hasara ya mabilioni ya shilingi katika uchumi wa Dar na wa Tanzania kwa ujumla, kila wiki!

Tufanyeje tuondokane na haya maamuzi ya kisiasa kwenye mambo yanayohitaji maamuzi ya kitaalamu?

It is abuse of power for the Head of State to set aside expert opinion and issue ill-considered decrees. He ought to be impeached!

Ayatollah JK usituelemee mno! Utatuharibia nchi yetu !

Naona watu wanaoumia kwenye hayo matuta waende mahakamani wadai fidia toka serikalini. Ukiumia kutokana na uzembe wa Rais au serikali una haki ya kulipwa fidia.
 
Phil.

Unachosema ni kweli kabisa. Naona kila mtu amechukua madaraka ya kuweka matuta barabarani ovyo ovyo tu. Si serikali si watu binafsi, Utakuta tuta kubwa limeweka kiasi kwamba gari ndogo ikipitisha tairi la mbele tu, gari inakaa juu ya tuta na kuwa kama mizani vile. Mfano ni matuta ya pale Chalinze. Siku za nyuma, nilienda Morogoro na kwa kweli ilibidi nisimame pale na kupiga picha. Nitajaribu kuziweka hapa. Hii ni kero kubwa mno kwa wenye magari. Tatizo la wanasiana wetu ni kukurupuka na maamuzi ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kujua faida na hasara zitokanazo na maamuzi hayo.
 
Kwanza matuta yanasababisha uharibifu wa barabara.Pale gari linapo piga break kabla ya tuta linazidisha load maradufu,na baada matumizi ya namna hio ya muda mrefu barabara inaanza kuharibika,pia vilevile gari likisha vuka tuta,maana litaanza na low gear,ivo kuongeza load tena.
Kuna kipindi zamani JK aliwaambia TRA waongeze makusanyo ya mapato wakati hata hana idea wataongezea wapi,hata washauri wake walimwambia kwa wakati huo haikuwa possible,yeye wala hakujali!
 
Wana JF msiangalie upande mmoja wa shilingi,sisi wakazi wa Morogoro road tunajua ni watu wangapi tulikuwa tunawapoteza kila siku kwa kugongwa kuanzia Ubungo hadi Kibamba.Kwa mfano pale Kimara stop over tulikuwa tunapoteza at least mtu mmoja kila baada ya siku mbili au tatu.
Mbona pale mikumi mbugani kuna matuta miaka mingi tu kama kilomita hamsini lakini hakuna anaeongea naile pia ni highway. Au kwakuwa pale kuna "wanyama ambao wanatuingizia fedha za kigeni"?
Tuangalie solution tunazozitoa maana maisha ya watu yanapotea ambayo ni muhimu kuliko hao wanyama wa mikumi.Mnaouzungumza mnataka kuwahi lakini pia maisha ya watu wanaoishi hapa katikati ni muhimu sana kama safari zenu zilivyo za muhimu.
Naomba kuwasilisha kuwasilisha,haya ni mawazo tu niko tayari kupokea mawazo mengine kutoka kwenu maana Tanzania yetu sote na tuna haki ya kikatiba ya kutoa maoni.
 
Soma hapa nchini mapendekezo ya mbadala wa matuta..

.... TUFIKIKIRIE KUWEKA VIVUKO VYA MIGUU VYA FLYOVER AU BRIDGE AU UNGERGROUND..ROAD CROSS AMBAZO NI CHEAP kwenye vijiiji au maeneo yenye wakazi ..ili watembea miguu na waenda magari wote wawe salama kwenye highways...
 
Last edited:
Wana JF msiangalie upande mmoja wa shilingi,sisi wakazi wa Morogoro road tunajua ni watu wangapi tulikuwa tunawapoteza kila siku kwa kugongwa kuanzia Ubungo hadi Kibamba.Kwa mfano pale Kimara stop over tulikuwa tunapoteza at least mtu mmoja kila baada ya siku mbili au tatu.
Mbona pale mikumi mbugani kuna matuta miaka mingi tu kama kilomita hamsini lakini hakuna anaeongea naile pia ni highway. Au kwakuwa pale kuna "wanyama ambao wanatuingizia fedha za kigeni"?
Tuangalie solution tunazozitoa maana maisha ya watu yanapotea ambayo ni muhimu kuliko hao wanyama wa mikumi.Mnaouzungumza mnataka kuwahi lakini pia maisha ya watu wanaoishi hapa katikati ni muhimu sana kama safari zenu zilivyo za muhimu.
Naomba kuwasilisha kuwasilisha,haya ni mawazo tu niko tayari kupokea mawazo mengine kutoka kwenu maana Tanzania yetu sote na tuna haki ya kikatiba ya kutoa maoni.

Hivi matuta ni ufumbuzi pekee wa watu kugongwa? Kwa nini JK aliamuru uwekwaji wa matuta?
 
huu ni upuuzi wa hali ya juu. nimepita hiyo barabara this w'end nimeshangaa. waende nchi kama swaziland wakaone highway zinakuwaje na wapita kwa miguu inakuwaje. nchi ndogo kama swaz inatushinda?
 
Kwanza matuta yanasababisha uharibifu wa barabara.Pale gari linapo piga break kabla ya tuta linazidisha load maradufu,na baada matumizi ya namna hio ya muda mrefu barabara inaanza kuharibika,pia vilevile gari likisha vuka tuta,maana litaanza na low gear,ivo kuongeza load tena.

Hapo hapo Chalinze, kuna semi trailer moja kutokana na tuta kuwa kubwa ilipiga breki na kusababisha container kwenda mbele na kuigonga cabin ya dereva karibu kuitoa kabisa.
 
Nchi yangu Tanzania umekosa nini hadi kuchezewa kiasi hiki? Tangu lini kukawa na speed bumps kwenye Highways? Kwani kuna shida gani kwa Serikali kutengeneza flyovers kila baada ya kilometer moja kuwezesha watu kuvuka barabara? Au kuweka vivuko chini ya barabara? Hata siku moja huwezi kuniconvince kuwa speed bumps ni suluhisho la ajali. Barabara ziwekewe fense na ziwe pedestrian friendly. Hivi kweli katika karne hii unatengenza barabara ya highway ambayo magari yanatoka kila upande unategemea nini? Kupanga ni kuchagua, ni bora tukawa na barabara chache nzuri kuliko kuwa na barabara nyingi ambazo ni makaburi ya wananchi. Sioni ni kwanini kusiwe na two way road toka Dar hadi Mwanza/Arusha/Tunduma/mtwara na hata Sumbawang, na barabara hizi ziwe highway on its true sense. Tulete makandarasi wanaojenga barabara za kuhimili magari ya aina yoyote na kwa muda mrefu. Kuweka matuta barabarani ni kurahisisha tatizo gumu na kunasababisha hasara kubwa kwa serikali , wananchi na pia husababisha madereva kupita pemebeni na kuwagonga hao uliotaka kuwasaidia.
 
Asante sana mwenzetu Phillemon Mikael kwa kuanzisha mada hii. Maoni yako kwamba ni vibaya wanasiasa kupuuza ushauri wa wataalamu ni ya muhimu sana. Bumps kwenye highway ni kosa kiafya na hata kiuchumi. Lazima hizo bumps za Morogoro Road zitaleta hasara ya mabilioni ya shilingi katika uchumi wa Dar na wa Tanzania kwa ujumla, kila wiki!

Tufanyeje tuondokane na haya maamuzi ya kisiasa kwenye mambo yanayohitaji maamuzi ya kitaalamu?

It is abuse of power for the Head of State to set aside expert opinion and issue ill-considered decrees. He ought to be impeached!

Ayatollah JK usituelemee mno! Utatuharibia nchi yetu !

Naona watu wanaoumia kwenye hayo matuta waende mahakamani wadai fidia toka serikalini. Ukiumia kutokana na uzembe wa Rais au serikali una haki ya kulipwa fidia.

Hoja ya msingi ni kwamba matuta yaliyowekwa yanasabaisha foleni na usumbufu mkubwa kwa watu.Rais alipotoa agizo la kujengwa kwa matuta nia yake ni kukoa maisha ya raia wake.

Kabla yake kuna maraisi waliotangulia ambao hawakuwa na wazo kama lake.

Kwa kauli nyingine Rais alitaka nchi yetu iendeshwe kisayansi.Kwa suala hili ni kwamba Rais anapotoa amri bila shaka watendaji wanawajibika kuchunguza na kuandaa mpango madhubuti wa ili kile kitakachojengwa kiweze kukidhi ile haja ya msingi ya kuokoa maisha ya watu.

Sasa kumshambulia Rais na kumwita majina ya Ayatullah haliwezi kuwa ni suluhisho la ile hoja ya msingi..yaani kuokoa maisha ya wananchi kwenye barabara ya Morogoro.Kwanza Ayatullah hapo hapakuwa mahali pake kabisa hapana uhusiano wowote na ubaya wa matuta yaliyojengwa.

Kwa ujumla ukitaka kumkejeli Rais kutokana na utendaji wake neno hilo halifai,si mahali pake!
 
Nchi yangu Tanzania umekosa nini hadi kuchezewa kiasi hiki? Tangu lini kukawa na speed bumps kwenye Highways? Kwani kuna shida gani kwa Serikali kutengeneza flyovers kila baada ya kilometer moja kuwezesha watu kuvuka barabara? Au kuweka vivuko chini ya barabara? Hata siku moja huwezi kuniconvince kuwa speed bumps ni suluhisho la ajali. Barabara ziwekewe fense na ziwe pedestrian friendly. Hivi kweli katika karne hii unatengenza barabara ya highway ambayo magari yanatoka kila upande unategemea nini? Kupanga ni kuchagua, ni bora tukawa na barabara chache nzuri kuliko kuwa na barabara nyingi ambazo ni makaburi ya wananchi. Sioni ni kwanini kusiwe na two way road toka Dar hadi Mwanza/Arusha/Tunduma/mtwara na hata Sumbawang, na barabara hizi ziwe highway on its true sense. Tulete makandarasi wanaojenga barabara za kuhimili magari ya aina yoyote na kwa muda mrefu. Kuweka matuta barabarani ni kurahisisha tatizo gumu na kunasababisha hasara kubwa kwa serikali , wananchi na pia husababisha madereva kupita pemebeni na kuwagonga hao uliotaka kuwasaidia.

Naam,sasa hapa Jobo ameonesha njia ya kupata suluhu ya msongamano katika barabara zetu.Mchango wake umetulia kwenye hoja ya msingi.Hajatukana na kutumia title za kidini kumpa Mkuu wa nchi.
 
Wana JF msiangalie upande mmoja wa shilingi,sisi wakazi wa Morogoro road tunajua ni watu wangapi tulikuwa tunawapoteza kila siku kwa kugongwa kuanzia Ubungo hadi Kibamba.Kwa mfano pale Kimara stop over tulikuwa tunapoteza at least mtu mmoja kila baada ya siku mbili au tatu.
Mbona pale mikumi mbugani kuna matuta miaka mingi tu kama kilomita hamsini lakini hakuna anaeongea naile pia ni highway. Au kwakuwa pale kuna "wanyama ambao wanatuingizia fedha za kigeni"?
Tuangalie solution tunazozitoa maana maisha ya watu yanapotea ambayo ni muhimu kuliko hao wanyama wa mikumi.Mnaouzungumza mnataka kuwahi lakini pia maisha ya watu wanaoishi hapa katikati ni muhimu sana kama safari zenu zilivyo za muhimu.
Naomba kuwasilisha kuwasilisha,haya ni mawazo tu niko tayari kupokea mawazo mengine kutoka kwenu maana Tanzania yetu sote na tuna haki ya kikatiba ya kutoa maoni.

my tanzania laiti ungelipita hyo barabara asubuhi...au jioni....nimepita siku mbili tatu nikienda moro ni hatari..lazima ukute magari yaliyogongana kwa nyuma kwa sababu ya breki za ghafla..ni mengi...

wewe uliza kwa wiki iliyopita tu kuna ajali ngapi..zimetokea za magari..natoa changamoto mtu aende traffic akaangalie statistics ya ungezeko la ajali moro road..but anyway presida alisema .."....madereva akiendesha kazi kwenye bump wakigonga shauri zao....!!"..........nadhani zile patrol nissan zake na bmw zina springs za gesi hazisikii matuta...

pole sisi wenye vi corolla mkweche!!
 
Kwa uamuzi wa kuweka matuta kwenye highway naona Serikali inaanza kukosa uelekeo. Kila siku mkuu wa kaya anatembeza bakuli kuomba msaada wa kujinasua kutokana na miundombinu mibovu pamoja na huduma za jamii ambazo ziko chini ya kiwango. Rasilimali tulizo nazo ni haba na kunahitajika umakini wa hali ya juu katika kuzifanyia mgawanyo na kuzipa kipaumbele. Suala la kuweka matuta kwenye highway kwa dhana ya kuokoa maisha ya watu naona ni maamuzi yasiyokuwa na msingi wowote. Binadamu sio mnyama, itolewe elimu kuhusu matumizi sahihi ya barabara na sheria zinazohusu matumizi ya barabara ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni kwa madereva na ukaguzi wa magari zifuatwe. Alama za barabarani ziwekwe pale zinapotakiwa. Kuanza kuweka matuta ni utapanyaji wa hovyo na usio na mantiki wa rasilimali haba. Leo tunaambiwa hakuna hela kwa walimu lakini naamini kwa zoezi hili zitatumika bilioni nyingi ambazo zingeweza pia kutumika katika kukarabati barabara kadhaa ambazo ni mbovu na hata kujenga madaraja kadhaa.

Nakumbuka wakati Magufuli akiwa Waziri kwenye Wizara ya Miundombinu alishatoa maelekezo kuwa matuta kwenye highway hayatakiwi na yale yaliyokuwepo aliagiza yabomolewe. Mbona sasa kila mtu anatoa maamuzi kwa jinsi anavyotaka yeye? Je hii ndiyo dhana halisi ya kwenda sambamba na mabadiliko/maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayotokea duniani? Wanasiasa wajaribu kuwa serious na mambo yanahusu Taifa,
 
Heshima mbele wakuu..... Kwa kweli hii ni hoja nzuri lakini tatizo ni mleta hoja (PM, no offense intended), ameleta hoja husika kama rudio la hoja ambayo ilikuwa tayari discussed. Kwa kukumbusha tu hii ni thread husika started by PM:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...kijembe-tanroads-awatuhumu-kuwa-wabaguzi.html

Nirudi kwenye hoja nyingi zilizotolewa huko nyuma.

Hivi matuta ni ufumbuzi pekee wa watu kugongwa? Kwa nini JK aliamuru uwekwaji wa matuta?

Mkuu Roya Roy, Rais ni mtu wa kuamuru matuta? Hapana, kutokana na ukweli kwamba sisi wahusika (wahandisi, na wahusika wengine) hatujawahi kutoa mbinu muafaka ya kupunguza ajali barabara zetu, wahusika ambao ni raia wanaopoteza maisha kila siku wanajua mbinu zoelefu ni uwekaji matuta.... Kwa vile wao ndio mbinu pekee wanayoijua/tunayoijua ni hiyo na kwa vile Mheshiwa Raisi ni jukumu lake kusaidia wananchi wake alipoambiwa hilo yeye akasema ruksa, weka matuta. Sisi ambao ni "technical minded" individuals tulimshauri Raisi against mamtuta na kumpa alternative?? The answer is NO!!

Jamani, lawama nyingine ni za bure na hazina manufaa kwa kweli.... Hili la matuta limekuwa linazungumziwa lakini bahati mbaya sisi wataalamu hatujaumiza vichwa kulitatua na tunaishia kupoteza maisha ya watu mpaka/to an extent kwamba Mhe Raisi ameamua kufuata mbinu zoelefu ya kuweka matuta kwalo hili na to me HE IS VERY RIGHT!!

huu ni upuuzi wa hali ya juu. nimepita hiyo barabara this w'end nimeshangaa. waende nchi kama swaziland wakaone highway zinakuwaje na wapita kwa miguu inakuwaje. nchi ndogo kama swaz inatushinda?

Mkuu Ochu, tupo pamoja lakini kuna mengi ya kuangalia kuliko kufanya direct comparison. Kuna vitu kama majukumu ya nchi husika, aina ya barabara zenye kuzungumziwa, na vitu kama hivyo. So hilo la Swaziland kwa kweli naomba tusdiliweke kama mwongozo!!

Mwisho, wakuu naomba tufanye tofauti kati ya "Highways" na "Freeways" kimakini kwa kuangalia nchi husika!!

Naomba kuwakilisha!!!
 
matuta ni lazima kuepuka vifo vya wapendwa wetu, mpaka hapo tutakapokuwa na madereva wanapjali misha ya watu, taifa linalojali watu wake, na hizo flyover zijengwe, lakini hatuwezi kuendelea kuhubiri theory za ulaya na swaziland, huku watu wetu wakiendelea kuangamia.
 
Hata wakiweka matuta kila baada ya meta 100, ajali zitaendelea kuwepo kutokana na kwamba watanzania wengi tunapenda njia za mkato katika kila kitu. Leo hii ni wangapi wapo tayari kutumia vivuko maalum kuvuka barabara? Utakuta mwananchi anaswaga ng'ombe wake barabarani bila ya wasiwasi katika eneo la kwenda kasi ya zaidi ya kilometa 80 kwa saa, sasa kama baadhi ya watu wenyewe tuko hivi mtu unategemea nini tena?
 
Tatizo wataalamu wetu nao wanachukulia kila kitu anachosema rais kuwa ni halali. sheria yetu ya barabara hairuhusu kuweka matuta kwenye highway. kwa hiyo hata rais akisema, bado ni ukiukwaji wa sheria tu. nadhani hapa walipaswa kufikiria ushauri wa rais na kufanya kitu ambacho ni convinient kutekeleza aguizo la rais na kuwarahisishia watumiaji wa barabara maisha
 
Wana JF msiangalie upande mmoja wa shilingi,sisi wakazi wa Morogoro road tunajua ni watu wangapi tulikuwa tunawapoteza kila siku kwa kugongwa kuanzia Ubungo hadi Kibamba.Kwa mfano pale Kimara stop over tulikuwa tunapoteza at least mtu mmoja kila baada ya siku mbili au tatu.
Mbona pale mikumi mbugani kuna matuta miaka mingi tu kama kilomita hamsini lakini hakuna anaeongea naile pia ni highway. Au kwakuwa pale kuna "wanyama ambao wanatuingizia fedha za kigeni"?
Tuangalie solution tunazozitoa maana maisha ya watu yanapotea ambayo ni muhimu kuliko hao wanyama wa mikumi.Mnaouzungumza mnataka kuwahi lakini pia maisha ya watu wanaoishi hapa katikati ni muhimu sana kama safari zenu zilivyo za muhimu.
Naomba kuwasilisha kuwasilisha,haya ni mawazo tu niko tayari kupokea mawazo mengine kutoka kwenu maana Tanzania yetu sote na tuna haki ya kikatiba ya kutoa maoni.
kwa maoni yangu ni vitu viwili tu wanachoweza kufanya ni kujenga subway au flayover kama la pale manzese,kila polipo na kituo cha basi.
kisha sehemu zilizobakia za barabara wajenge uzio kuzuia watu kukatisha barabara ovyo.
 
Back
Top Bottom