Matusi………………..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Labda leo niwaulize wana JF wenzangu.....................

1. Matusi ni nini?
2. Nani alikuambia kwamba kuna matusi, au ni nani alikufundisha matusi?
3. Matusi yana athari yoyote?
5. Zipi hizo? ni kwa nini mtani (Kuna makabila huitana watani) wako akikutukana hukasiriki?
6. Kwa nini kama siyo mtani wako unakasirika?

Lakini mimi nina mtazamo tofauti..................

Matusi, ninavyofahamu mimi, ni ukweli wa mapokeo (perceived truth). Ukweli halisi (real truth) ni kwamba hakuna matusi, ila kuna maneno yanayowakilisha sehemu za mwili wako, wazazi wako, majina ya wanyama, ndege, wadudu, majina ya mahali (eneo) fulani au kabila fulani. Mfano: mtu akikuambia mbwa, hupaswi kukasirika, ila unatakiwa umwambie kwamba amekosea, wewe siyo mbwa, ni binadamu. Ila ukikasirika, unakuwa mbwa kweli. Tatizo kubwa ni tafsiri iliyowekwa kwenye mawazo yako ya kina (kwenye akili yako)……………………!
 
Mtambuzi: nijibie hili swali kabla sijaanza kuchangia mada. Je umewahi kufanya MEDITATION?..
 
nitukane kuhusu mama yangu nikutoe ngeu ndo utajua kuna matusi,utani au hakuna matusi kabisa.
 
ukiwa mtoto mdogo ndio kuna matusi...
ukishakuwa mtu mzima hakuna matusi...

Angalau umeanza kunipa mwanga............. nakumbuka nilipokuwa mdogo, mdogo wangu alinikuta tunacheza ule mchezo wa baba na mama, (naamini hakuna ambaye hajawahi kucheza mchezo huo) yeye akaenda kumwambia mama kuwa ametukuta tukifanya mchezo wa matusi, nakumbuka nilicharazwa bakora na mama......... Ni tukio ambalo bado nalikumbuka.......
Kwa hiyo kuanzia hapo nikapata ufahamu kuwa ule mchezo wa wazazi wawapo chumbani ni matusi.............! huku ukumbwani nikakutana na maneno yanayoitwa matusi,, lakini baada ya kupata ufahamu, nimegundua kwamba huo ulikuwa ni uongo!
 
Duh mkuu kun asehem ambayo bado hata ukiwa mkubwa maneno mengine ni matusi
Maana ukimtukana mzazi wangu hata kama hilo unalosema wewe sio tusi linageuka kuwa tusi
Maana kuna maneno ambayo huwezi kuyatamka against mke au mzazi wa mtu au binafsi yeye kama yeye bado yanaonekana hayana staha
 
nitukane kuhusu mama yangu nikutoe ngeu ndo utajua kuna matusi,utani au hakuna matusi kabisa.

ha ha ha haaaaaa.......... Hata mimi nilikuwa kama wewe. kwa hiyo sikushangai.........
 
Duh mkuu kun asehem ambayo bado hata ukiwa mkubwa maneno mengine ni matusi
Maana ukimtukana mzazi wangu hata kama hilo unalosema wewe sio tusi linageuka kuwa tusi
Maana kuna maneno ambayo huwezi kuyatamka against mke au mzazi wa mtu au binafsi yeye kama yeye bado yanaonekana hayana staha

Lakini ukumbuke kwamba tulifundishwa hivyo tangu utotoni...............
 
kipi ni tusi na kipi sio tusi,ni maumivu kiasi gani utasikia ukitukanwa yote yanategemea sana tena sana na mazingira aliyokulia mtu.Ukitukanwa,ukiwa embarassed,ukisikia aibu,ukifadhaika,zote hizi ni hali zinazoathiri kitu kinachoitwa EGO.Hakuna binadamu asiye na EGO,ina react vipi kwenye hali tofauti hiyo inategemea na mazingara aliyozaliwa na kukulia mtu.Mfano mtu wa bara ukimwambia 'ms....nge wewe' au 'unaf.....rwa nini?' wallah atakukata na panga,lakini huku pwani usishangae hata mama mzazi akimtukana mwanae 'ku......nina wewe' na wala mtoto hashtuki.Hiyo ndiyo hali halisi.
 
Lakini ukumbuke kwamba tulifundishwa hivyo tangu utotoni...............

mkuu hili la wazazi au mke au ndugu yangu wa karibu sijui kama ni kufundishwa tangu utotoni
Mzazi wangu nampa heshima zote na maneno mengine siwezi yaruhusu yake kwake so kwangu yale maneno ambayo ni offesnsive bado nayaregard kama matusi
Na ndo maana abusive language dhidi ya mtu ni kosa kisheria pia
 
Kuna matusi bwana lugha chafu za kejeli na kudhalilisha utu wako

Nikuulize swali................ Kama nikukuita kwa lugha ya mahaba........ "hi fokochero Bebii how are you" Utakasirika?
 
Back
Top Bottom