Matusi ya Lema na Matusi ya Lusinde ni Matusi Yetu na Unafiki Wetu!

kulinganisha ya Lusinde na ya Lema, na kama kuna mwandishi mzuri ama analyst anaelinganisha vitu basi angeweka hapa ni kipi alichokisema Lema (ambacho ni tusi) ukilinganisha na cha Lusinde. Lakini cha muhimu pia tujiulize na kuanalyze hicho alichokisema Lema (ambacho ni tusi) ndilo lililomvua Ubunge?

Nahisi hakuna haja ya kulinganisha matusi ya mtu na mtu. Binafsi siyajui matusi yaliyomvua ubunge Lema, lakini hatuwezi kuyalinganisha na ya Lusinde au yeyote kwa sababu kwanza ni mambo yaliyotokea katika nyakati tafauti na katika dhamiri tafauti. Ikiwa aliyoyasema Lema (hata kaCma si matusi ya ukubwa wa yale ya Lusinde) wapinzani wameyachukua hayo na kumwadhibu kwa kuenguliwa. Cha kufanya kwa CDM ni kukata rufaa kuinga hukumu hiyo, kukaa kimya na kukubali hukumu ni sawa na kukubali kuwa Lema alitenda makosa. CDM wamsafishe Lema kwa kukata rufaa.

Kwa mtazamo wangu, tusi ni tusi tu, liwe kubwa kama la Lusinde (kuolewa mahabusu, kuliwa, kumegwa) au dogo kama Mdee (Wasira uso kama sokwe); almuradi tu tamko hilo limemkwaza aliyeambiwa. Tukianza kutaka kulinganisha ukubwa wa matusi, tutakuja kuhalalisha dhambi kubwa na ndogo, wizi mkubwa na mdogo, rushwa kubwa na ndogo...wakati yote ni makosa.
 
Matusi ya lusinde kila mtu ameona.unaweza kutudhibitishia kuwa Lema ametukana?walalamikaji walidai hivyo lakini mimi sijaona uthibitisho wowote walioitoa kuithibitishia mahakama kuwa Lema alitukana?

matusi ni matusi tu,yafanyike chumbani,yafanyike sebuleni yafanyike hadharani yanabaki kuwa matusi
 
My take wote waliohusika kutoa matusi kinyume na taratibu za kampeni wafunguliwe mashitaka ili sheria ichukue mkondo wake na haki itendeke. Sio kosa hilolo wafanye watu wengi lakini akifanya mwingine lionekane kosa.
 
Back
Top Bottom