Kilasara
JF-Expert Member
- Dec 21, 2008
- 577
- 116
Nakubaliana na MwanaJF Waberoya, kwamba Matusi ni Matusi, hata kama yanatolewa na supporters na wapenzi wetu. Kama Chama tusipoyakemea, tutaendeleza unafiki na hatimaye tutashindwa kutekeleza yale mema tunayonuia.
Chadema kilipozinduliwa, nakumbuka Mzee Edwin Mtei akisisitiza sana umuhimu wa kuelezea sera na misimamo ya Chama, kwa ufasaha na kwa lugha isiyo na matusi au maneno ya kashfa hadharani. Wakati huo CDM ilieleza utamaduni wa siasa za kisayansi na "kimantiki"! Wengi waliomsikiliza Mzee Mtei walisema huyu hakuwa "mwanasiasa"!
Hata hivyo sasa CDM kimekua na kwa kawaida ni chama kisichosheheni lugha chafu; na umakini na umahiri wa viongozi wake kuchambua matatizo na mustakabali ya taifa unajulikana. Kama ni Dk. Slaa, kama ni Freeman Mbowe au Zitto Kabwe, wote hawa sio tu wanajulikana, bali wanakubalika. Ni utamaduni wa kujivunia.
Kama kutokana na kasi ya CDM kukua na kupanuka, kuna vijana wasiotilia maanani utamaduni wa lugha safi ya Waasisi, huu ni wakati wa kutathmini mikakati ya kuwavunda. Hata hivyo ni vizuri tutambue kuwa wakati wa kampeni ni lazima mapungufu ya wagombea yatatajwa na wapinzani; kama wao wanavyojivunia ubora wao.
Lakini kwa maoni yangu mgombea anayedhani amekashifiwa au kudhalilishwa kwa mapungufu yake kutajwa hadharani, hana budi kujitokeza binafsi na kueleza korti. Kujitokeza kugombea nafasi ktk madaraka ya umma, lazima kutafsiriwe kwamba ni kukubali kuanikwa kwa mapungufu yako. Hii haimaanishi matusi na maneno yasiyotamkwa mbele ya watu wastaarabu e.g yale ya Lusinde yaruhusiwe.
Wakati mwingine, mapungufu yanaweza kutajwa kwa lugha ya kisanii, ili muhadhara ucheke au uelewe zaidi. Kwa mfano wavulana wa "kisasa" waliotoka ng'ambo wametoboa masikio, na wakiwa wagombea wanambiwa watalipiwa nauli kwenda Mombasa kwa shoga wenzao!!. Kama mgombea mvulana aliyetoboa masikio, anaona hilo ni tusi, basi, it is too bad!!