Matusi ya Lema na Matusi ya Lusinde ni Matusi Yetu na Unafiki Wetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matusi ya Lema na Matusi ya Lusinde ni Matusi Yetu na Unafiki Wetu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waberoya, Apr 6, 2012.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  Kuna tatizo kuu la msingi ambalo nisiposema dhamiri yangu itanihukumu na sitakaa kimya kwa sababu wengine wameamua kukaa kimya.

  Jamii ya Tanzania iko kwenye ugonjwa mkubwa na tusipoudhibiti huu ugonjwa hakuna wa kutusaidia. Tunaiumiza jamii, tunaharibiu vizazi vijavyo kwa kisingizio cha mabadiliko!

  Sera ya chadema si matusi!! Sera ya chadema ni mabadiliko, sijawahi kuona Slaa akitoa matusi ya nguoni, sijawahi kuona Mbowe akitoa matusi ya nguoni, wala sijawahi kuona Zito akitukana, these people they are still high in their positions na popular kwenye siasa na wanaaminika kwenye jamii kwa kuleta mabadiliko

  Ila nimemsikia Mdee akitukana( personally nilimkataza) , nilimsikia Lema akitukana, tumeona Sugu akitukana mpaka kujirekodi!! Hawa ndio wabunge wetu, ndio tuliowapa dhamana ya kuongoza taifa letu kwa nafasi zao…ila wanatukana, wakitukana hawa ni sawa??

  Nani kasema?

  Kuna uwezekano mkubwa akina Mbowe, slaa hawawezi kuwadhibiti akina Lema, kwa sababu ya kuwaonea aibu!! Unapopagawa na siasa na kuona kila unachotukana kinashangiliwa, basi jamii nzima inakuwa imeoza! Msikilize Lusinde utaamini!

  ILA; Ukiwa mpinzani lazima uangalie zile nafasi/chances/ opportunities ambazo adui yako anaweza kuzitumia kukuangamiza!

  Kama CCM wametumia mahakama kumuondoa adui yao Lema, it is okay na wametumia karata yao vizuri sana.

  Lakini kama si CCM na mahakama, je matusi yanakubaliwa katika jamii yetu??

  Hivi Mdee, sugu, Lema na Lusinde tofauti yao ni nini??

  Na sisi wataka mabadiliko , ukweli wa mioyo yetu na matusi uko wapi? Kuwa tutukane tu kwa sababu kwa kufanya hivyo ndio tunahimiza moto wa mabadiliko??

  Matusi mangapi yanatukanwa humu ndani? Wanaotukana ni akina nani? Je wakipewa uongozi hawatatukana kwa sababu ni viongozi? Yaani uongozi una mechanism ya kuzuia matusi biologically? Matusi tumeyakubali, tunaishi nayo, tunalala nayo kila kona ya nchi yetu si kwa hao niliowataja, yako kila kona, kwenye madaladala, kwenye michezo name it!

  Lema ameadhibiwa na mahakama, Lusinde ameadhibiwa na wananchi-ambao wengi wao wanatukana, mwisho wa siku wote ni watukanaji! Ikifika hatua tukaona Lema ni shujaa tunakuwa tumevua akili zetu na utu wetu na kuuweka kando na sisi……..tunaishi kinafiki , tuna post kinafiki kwani usafi na intergirty is not part of our life!!


  In this case mahama iko clean..tena wanapongezana, hivi..juzi tu tumelia Lusinde anatukana-tukasema kila kona na kulaani, leo hii Lema anavuliwa ubunge kwa kutukana tunaona ubaya?? Kweli??
   
 2. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kwa hiyo kweli alimtukana Batilda ?
   
 3. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Well said.
   
 4. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,224
  Likes Received: 1,071
  Trophy Points: 280
  Umenena mkuu Waberoya!!!!
   
 5. G

  George Katembo Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli unafiliria mwanajamii
   
 6. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Matusi ya lusinde kila mtu ameona.unaweza kutudhibitishia kuwa Lema ametukana?walalamikaji walidai hivyo lakini mimi sijaona uthibitisho wowote walioitoa kuithibitishia mahakama kuwa Lema alitukana?
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  sisi kwenye hili jukwaa tusingependa habari ndefu na hotuba ndefu! tunaomba utupe ushahidi wa matusi ya lema,sugu na mdee! usiweke habari ndefu isiyo na vielelezo! tunakushuru kwa kuandika ujumbe mzuri ila tusaidie ushaidi uliyo nao!. Amani kwako
   
 8. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani hebu tuache ushabiki, matusi aliyotoa lema kwa batilida ni yapi? Kuuliza maisha yake kwa jamii anayoitumikia ndio matusi? hube tuache ushabiki wa kimagambamagamba.
   
 9. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  We need evidence for this accusation unless otherwise it's just nonsense. You can't defend Lusinde just because other politicians do the same.
   
 10. M

  Mgaza jm Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhhhh wote walipotoka maadili lakini Mh. Lusinde ana PHD ya mdomo mchafu
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Waberoya umeongea vizuri sana.

  Mdee, Sugu, Lema nao ni watukanaji na wenye kutumia lugha mbovu mbovu kwa wapinzani wao.

  Na kwa sisi kuwashangilia na hata kuwatukuza wakati mwengine kunaonyesha tu sisi Watanzania ni watu wa aina gani. Hatuna integrity.

  Mtu kama Mdee kumwita Wassira Sokwe-mtu ni aibu........kwa misingi yote iliyopo ya kibinaadamu
   
 12. c

  chilljuice Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kunya anye bata akinya kuku inakuwa nongwa! Lusinde, Lema, Mdee pamoja na Sugu wote ni mfano mbaya kwa jamii yetu kwa kuacha siasa na kutoa lugha za matusi! Mahakama kwa hili iko clean, Big up mtoa mada.
   
 13. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu wazee walianza hayo yalikuwa majibu yao.Sasa hivi kwa majority imekuwa ni desturi inabidi wabadilike kwa kweli hiki kitu hakitakiwi kabisa na wote wakome kutukana.
   
 14. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Zile zile mentality za ki-wareboya boya! Anataka kuhalalisha uhuni unaofanywa na Lusinde eti na wengine nao wanatukana. Kwanini usiweke hayo matusi tukayaona? Hivi yale yaliyosemwa na lusinde uliyasikia wewe? Ni lini ulimsikia Lema akisema upumbavu wa aina hiyo? Wacha usomi uchwara wako bwana.
  Wewe ni msaliti na mbinafsi mkubwa. Unataka upewe sifa. Wala humpendi Mbowe na Dr Slaa kama unavyotaka kutuaminisha.
   
 15. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Uliyosema ni kweli tunaishi na matusi,well said,kwa mchezo nani anajukumu la kuthibiti hali hiyo jawabu ni umma kama ulivyomdhibiti Lusinde,kwa kuwa tayari ilikuwa na ushahidi. Tunakuja swala la LEMA la kumtusi mshindani wake kweli matusi si haki.Hakika Mahakama kazi yake ni kutoa HAKI na KUONA HAKI ILE INATENDEKA.Hapa napata shida sana na hukumu ya LEMA na kesi yake nzima.

  Hivi HAKI NA UTEKELEZAJI WA HAKI ILE UNAMWENDEA NANI iwapo mwathirika wa matusi HAKUSHITAKI na WALA HAKUFIKA MAHAKAMANI kama shahidi japo yeye mwenyewe HAKUSHITAKI.Yani hata kama ni upofu na ujinga wa sheria hivi ni aina gani ya uendeshaji kesi mpaka inatoka judgement pasipo mhusika wa kutukanwa [victim] yeye binafsi kutia mguu kwenye mahakama hata kama ni kuwa shahidi wa upande wa mashitaka.Wanasheria watatusaidia sie tusio wajuzi wa sheria,hii ni aina gani ya mwenendo wa utafutaji wa haki na utekelezaji wake.

  Tutafute haki na utakelezaji wake kuithibitisha palipostahiki haki!!!!
   
 16. s

  stk Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sipati picha napanda jukwaani na shika kipaza sauti mbele ya umati wa watu ... Naanza we flani miguu kama naniii!duh huogopi?:ujafa hujaumbika worse still ukizaa ngedere?au mkeo akizaa nyani?tumuogope Mungu!ukiachana na hayo,mahakama haikufanya maamuzi ya kizalendo bora ingemtoza fain kumvua ubunge kwani kesi inahusu wizi wa kura?na hizo hela za kufanya uchaguzi kila siku asubuhi eeeh!
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Vifungu vya sheria vipo wazi kuwa ukitukana matusi ya jinsi kadha na kadha na ukapatikana na hatia utavuliwa ubunge

  Sasa mtu anapoamua kutukana ni ama hakujua kuwa sheria hiyo ipo ama ameamua kuidharau

  Hakimu hawezi kutoa adhabu nyengine wakati adhabu ya kosa tajwa imeainishwa wazi kisheria
   
 18. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  mama Zenji by night bado upo? Ile mitaa yako mbona hupatikani siku hizi?
   
 19. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Hii Habari ya Lema kila mtu anajifanya ni analyst na mwandishi mzuri,

  lakini aingii akilini kulinganisha ya Lusinde na ya Lema, na kama kuna mwandishi mzuri ama analyst anaelinganisha vitu basi angeweka hapa ni kipi alichokisema Lema (ambacho ni tusi) ukilinganisha na cha Lusinde

  Lakini cha muhimu pia tujiulize na kuanalyze hicho alichokisema Lema (ambacho ni tusi) ndilo lililomvua Ubunge?
   
 20. PERECY

  PERECY Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Nimerudia kusikiliza rekodi ya hotuba ya Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtera (CCM) wakati akimwaga MATUSI katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki, mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Ngarasero. Nimeandika zaidi ya sentensi 15, ambazo ni matusi au zina viashiria vya lugha ya matusi.

  Karibuni, Katibu Mkuu wa CCM, Mh. Mkama amesikika akitetea kwamba Lusinde alikuwa anajibu hoja za wapinzani wake, CDM.

  Aidha jana, tarehe 5/4/12, ubunge wa Mh. Godbless Lema (Arusha Mjini, CDM), umetenguliwa kwa kile kinasemwa kufanya kampeni bila kuzingatia maadili ya kampeni, ikiwepo matumizi ya lugha inayotafasiriwa kwamba ni matusi. Jambo zuri tu, kama kweli tunataka kulenga kampeni za kistaarabu!

  Katika dk 16:06 zilizorekodi hotuba ya Lusinde kama ilivyo katika mtandao, nimetambua mambo haya kama matusi au lugha ya matusi, wastani wa karibu sentinsi/tusi moja katika kila dk moja aliyotumia kuongea Lusinde:-

  1. Kuda-dada-deki (amerudia karibu mara sita).
  2. Wewe umekuwa ukiwachanja chale mpaka matakoni (akimlaumu Prof. Majimarefu).
  3. Hata wao ni mashoga basi, (akihusisha kutoga masikio na suala la ushoga).
  4. Nani hafahamu kwamba mbunge wa Arusha mjini aliolewa kule mahabusu/amepata bwana, (akihusisha Lema kuwa mahabusu na kwamba aliolewa), (ikiwa ni sodomization kwa tafsiri yangu).
  5. Dk. Slaa alitimuliwa uPadri baada ya kuwatia mimba wanakwaya. (akimtukana Dk. Slaa moja kwa moja)
  6. ***** huyu - Vicent Nyerere, ana akili mbovu. (akimtukana Mh. Vicenti Nyerere)
  7. Ameliwa -------- siye hatusemi. (ikimaanisha kuwa sodomized, iwapo sikujua anamtukana Vicent Nyerere au Godbless Lema).
  8. Acheni ushamba nyie. (akiwatukana wananchi, ambao wanaonyesha kuwa wafuasi wa CDM)
  9. Washamba wakubwa nyie x 2. (akiwatukana wananchi)
  10. Washamba wakubwa ----, Dk. Slaa mshamba mkubwa, akivaa kombati, anakuwa kama kajinyea. (akimtukana Dk. Slaa)
  11. Viongozi wa CDM vichaa wa kulogwa. (akiwatukana viongozi wa CDM)
  12. Dk. Slaa anatishia kujamba wakati anaharisha. (akimtukana Dk. Slaa)
  13. Sera ya CDM ni sera ya jogoo, jogoo linamuahidi kuku gauni, huku lenyewe hata chupi halina. (akikitukana chama kwa ujumla wake).
  14. Mbowe anasema ana uchungu, kwani ana mimba? (akimtukana Mbowe)
  15. Mbowe pigwa mimba! Slaa pigwa mimba! Nasari pigwa mimba! (akiwatukana Mbowe, Slaa na Nasari).

  Sasa, nimeambiwa kupitia vyombo vya habari kwamba watu 3 ndiyo waliomfungulia mashtaka Mh. Godbless Lema, kufanya illegal practices katika kampeni wala siyo aliyeshindana naye katika ubunge Batilda Burian, vema. NANI WATAMFUNGULIA MASHTAKA LUSINDE KWA KUFANYA ILLEGAL PRACTICES katika kampeni za Arumeru Mashariki kama kweli tunatendeana haki?

  Sentensi na maneno ya viashiria vya matusi niliyotaja mnaweza kuyafanyia uchambuzi zaidi, na kurudia kuisikiliza hotuba ile ili kujenga hoja vizuri. Najua kuna mdau alikwisha uliza hoja kama hii humu mtandaoni, lakini sijui hatua gani zimeendelea kuchukuliwa.

  Nasisitiza wanasiasa kujenga hoja za msingi wakati wa kampeni. Ushahidi unajionyesha wengi wamekuwa wanajikita zaidi katika kumshambulia mgombea kuliko kushambulia-kwa uchambuzi na mikakati mambo ambayo ni matatizo na changamoto katika maendeleo ya wananchi. Lusinde alitumia zaidi ya dk 15, kushambulia watu, sio kushambulia kwa uchambuzi na mikakati matatizo ya wanaArumeru Mashariki.

  Kwa mzaha kabisa, Katibu Mkuu wake anaunga mkono kwamba huko ilikuwa kujibu hoja za wapinzani wake. Hapa unajua unashindwa kutafsiri hekima na busara ya kiongozi mkuu wa chama, katika kukiwezesha chama chake kupaa na kuaminiwa. Sijui bwana, SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA!


  Perecy Ugula
  MwanaJF Mchanga,
  Email: ugulapp@yahoo.co.uk
  Simu: +255 766 082388
   
Loading...