Matusi ya kikwete, wasira na ccm hayakubariki hata kidogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matusi ya kikwete, wasira na ccm hayakubariki hata kidogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Jun 12, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Ilianza kama utani lakini sasa imefikia hatua ya kupewa nafasi ya juu kama hoja ya kisiasa, kwamba matatizo ya kiuchumi tunayopitia sasa watanzania yako nje ya uwezo wa serikali yetu sababu yako nchi nyingi duniani.

  Jumamosi Ndugu wasira alitumia muda mrefu sana kuelezea kwamba upandaji wa bei ya mafuta nchini unasababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia, hivyo ni makosa, sio sahihi, na watanzania hatuna haki ya kukisakama chama cha mapinduzi na serikali yake kwa matatizo haya. akaenda mbele zaidi na kudai kwamba nchi zote zenye uchumi kama wetu zinakabiliwa na matatizo haya.

  Siku hiyo hiyo kama sikosei, Kikwete akiwa adis ababa na yeye akatoa kauli ya namna hiyo, akidai watawala wa africa wanatakiwa kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ama sivyo litakuja kuleta machafuko, Kikwete ndio mhasisi wa hoja hii mwanzoni mwa mwaka 2011 baada ya CHADEMA kuanza kuhamasisha wananchi kuisukuma serikali kutimiza wajibu wake kwa kujielekeza kurekebisha hali ya uchumi baada ya kila aina ya bidhaa kuanza kupanda bei kwa kasi.

  Haya ni matusi kwa watanzania, na ni dhihaka iliyopita kipimo, naomba nitoe kauli kwamba, Watanzania ni watu wa kipekee, tunaserikali yetu, mipaka yetu, na tunahaki ya kuishi, au kutaka kuishi ndani ya nchi yetu kwa namna tunavyotaka sisi.

  Huu mchezo wa kutuambia tuwe watulivu wakati tunashinda na kulala njaa eti kwa sababu na huko kwenye mataifa mengine wanashinda na kulala njaa pia ni kauli za kiburi na fedheha kubwa sana kwa upande wetu.

  Ni matusi na ni ishara ya kuishiwa uwezo wa kuongoza, kwa kiongozi yeyote yule kutumia matatizo ya majirani kama sababu ya kujustify matatizo tuliyonayo sisi. Ni bora kama mmeshindwa kuendesha serikali muachie watu ambao wanadhani wanaweza kutuletea unafuu kuliko kutoa hoja mfu za namna hii. Inawezekana nyie mmekwisha kukata tamaa, lakini hiyo sio sababu ya kulazimisha watanzania wote wakate tamaa kizembe zembe namna hii.

  Nikiwa nimebeba mtoto wangu huku naangalia TV, Machozi yalinitoka, pale wakina mama waliovaa sare za CCM walivyokuwa wakimshangilia wasira huku wakisema waambie waambie, na yeye anajitutumia kusema kwamba hali yetu sisi ni bora kuliko wamalawi na wazambia.

  Kikwete, Wasira na CCM. Naomba mtambue kuanzia leo kwamba, hata kama mnatuchukulia sisi kama mbwa, lakini sisi sio mbwa koko. sababu tunakwetu (TANZANIA) na tunayebaba (SERIKALI YETU). Kama mmeshindwa kuongoza nchi ondokeni mkasimamie familia zenu.
   
 2. Robato

  Robato JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 375
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Wasira alisema eti kuna vita kati ya Marekani na Iran ndo sbb bei ya mafuta iko juu.
   
 3. N

  NANKY Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wasira is indirect terrorist as far as he fails to reason on how to overcome food,shelter and cloths insecurity rather preaches absurd speech that has no root from the bottom,ccm has foolish,stupid and idiotic politicians who fail to push ahead the tanzania development let it go to hell 2015
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Sangarara, siku zote Watawala wetu wanatoa majibu mepesi kwa maswala magumu. Sasa hivi wameshapata majibu, miaka michache ilopita JK alipoulizwa kule Ufaransa alisema hajui kwanini Tanzania ni masikini.
   
 5. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Kumbuka kuwa wote waliokuwa wanashangilia walilipwa posho kwa kazi hiyo! Na wala shangwe zile hazikuwa zinatoka mioyoni bali midomoni na wasingeshangilia posho zao zilikuwa hatarini!
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Na hili pia, tunaviongozi katika ikulu yetu ambayo hawaelewi kabisa kwamba kauli zao zinatakiwa kuaminika kwa watanzania dhaidi ya zile za viongozi wa dini, lakini wanaongea uongo uongo uongo mkubwa kwa sababu tu wametengua akili za wasikilizaji wao kwa rushwa.
   
Loading...