mtotomtamuu
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 602
- 1,454
Nianze kwa kulaani vikali kitendo cha kunyanyaswa kwa mwanzilishi wa Jf Mr Mexence Melo. Anachofanyiwa mexence ni dhahiri anaonewa mchana kweupe
Je kwanini mexence anaonewa?
1.Mtandao wa Instagram
Huu ni moja ya mtandao ambao kwa sasa umegeuka kuwa kijiwe cha matusi mazito. Katika mtandao huu kumeibuka Account nyingi ambazo zimefunguliwa kwa ajili ya kuchafua watu
Kuna watu wamekuwa wakitukana matusi mazito instagram na wengine wanaikosoa serikali hadharani kabisa
Na kati ya Account ya instagram inayoisumbua serikali ni ya Mange kimambi ambaye amegeuka mwiba mkali kwa serikali kwa kuikosoa serikali na kuingilia maisha ya faragha ya watu wengine.
Wakati hayo yote yakitokea sijawahi kuona Mark Zuckeberg mmiliki wa Facebook,Instagram,Whatsapp akitiwa nguvuni kutokana na watumiaji wa mtandao wake kuichafua serikali
Hata wawakikilishi wa Mark Zuckeberg hapa Tanzania sijawahi kusikia wamekamatwa kulisaidia jeshi la polisi kutokana na watumiaji wa insta au fb kuvunja sheria
Mara nyingi jeshi la polisi limekuwa likitumia Taharifa za "kiitelejensia" kama wanavyosema wenyewe. Kuwakamata wanavunja sheria fb na Whatsapp na kuna baadhi walifikishwa mahakamani na mwisho wa siku wakashinda kesi
My take
Kama waliovunja sheria fb,insta na whspp mliwatafuta bila kuwakamata wamiliki na wawakilishi wao hapa Tz
Kwanini Mexence mumkamate? Kama sio uonevu huu ni nini?
Na mkiifunga jf na Instagram nayo ifungwe kwani hiyo ndio imewashinda kabisa mmebaki kuonea dagaa
[HASHTAG]#freemax[/HASHTAG]
[HASHTAG]#freemelo[/HASHTAG]