Mature-age entry to University inanipa wasiwasi

Baba Collin

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
456
58
Habari zenyu wana JF?

Nimekua nikipata shida na wasiwasi mkubwa kwa elimu yetu ya Tanzania hasa kutokana na namna mbalimbali zitumikazo kuwapata wasomi wa shahada mbalimbali za elimu ya juu.

Nafahamu kua zipo namna mbili zilizotumika kuwapata wanafunzi wa vyuo vikuu mwaka huu yaani 2011/2012 kua ni mfumo wa TCU na ule wa mature age entry.

Awali nilifahamu kua huwezi kujiunga na chuo kikuu pasipo kufaulu vizuri mtihani wa kidato cha sita au kufaulu katika ngazi ya diploma kutokana na aina ya course unayotaka kuendelea nayo.hapo sikua na wasiwasi kbsa kwakua hao wote hapo juu wanauwezo wa kuingia chuo kikuu na kusoma degree ya kwanza.

Napata wasiwasi baada ya kuona wapo wanaosoma degree huku wakiwa hawana elimu ya kidato cha sita au hata diploma.

Wapo walimu wa primary ambao hutumia certificate zao za grade A(ualimu ngazi ya cheti)pamoja na vyeti vyao vya kidato cha nne kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini kusoma degree ya kwanza.

Asilimia kubwa ya walimu hukimbilia njia hii kwani walishindwa kusafisha vyeti vyao vya kidato cha4(kuresit)na kukosa credit3 za O level ambazo ndio kigezo cha kuweza kufanya mtihani wa kidato cha sita.hvyo wao mature age ni njia rahic ya kupata degree kwani ukiwa na D tano za Olevel na certificate ya ualimu(grade A)unaweza kujiunga University.

Sasa ndugu wadau hivi kweli mtu ambae mtihani wa form4 umemshinda na kukosa sifa ya kufanya mtihani wa kidato cha sita anapopata udahili wa kusoma degree ya1 lets say ya education atakua na uwezo wa kufundisha hayo masomo ya sekondari?si tunatengeneza maafa kwa sekondari zetu za kata?
Ni wazi kua wapo walimu wengi wa sekondari na primary wasio na uwezo kutokana na mazingira yao waliyopita kupata
hizo nafasi.mbali na kuiba vyeti,kupata degree legelege(kupewa)nk nahisi na hili la mature age entry nalo litazamwe kwa namna ya pekee kabisa kwa manufaa ya watoto wetu katika shule zetu.

Naomba kuwasilisha!
 
Kuna watu wengi tu ninao wajua ambao walikuwa na uwezo mkubwa tu darasani lakini hawakufanya vizuri kwenye mitihani yao,ninachotaka kusema ni kuwa mature -age entry inatoa nafasi ya pili kwa wale ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani yao ya nyuma kujaribu tena..............after all,kama mtahiniwa wa mature age -entry atakuwa hana uwezo wa kimasomo(na hakutakuwa na aina yoyote ya upendeleo) si atafeli tu mtihani,na hivyo kukosa nafasi hiyo au hata kufeli baadae....................mimi nadhani mtu yoyote tu angekuwa anaruhusiwa kufanya mitihani hiyo,uwezo tu ndio ungekuwa unawachuja.......na hili linafanyika katika nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom