matunda ya sullivan summit yaanza kuonekana

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
President Kikwete and Ambassador Carlton Masters re-open Mount Meru Hotel

GO9G2365.JPG

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete cuts the tape to officially re-open Mount Meru Hotel in Arusha yesterday evening. Flanking the president on the left is the new investor for Mount Meru Hotel, the Chairman of HODI Hotels Ambassador Carlton Masters. Third Left is the Minister for Natural Resources and Tourism Ezekiel Maige and on the right is Arusha Regional Commissioner Isidori Shirima.

GO9G2383.JPG

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete unveils a plaque to signal the official re-opening of the Mount Meru Hotel in Arusha last night. On the left is the new investor for the Hotel ambassador Carlton Masters who is also the Chariman of Hodi Hotels and Vice Chairman of South African Development Enterprise Fund) SADEF.

GO9G2407.JPG

The Chairman of Hodi Hotels Ambassador Carlton Masters take President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete to a tour of the newly refurbished boardroom at the re-opened Mount Meru Hotel in Arusha last night.

GO9G2509.JPG

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete addresses invited guests and dignitaries who attended the re-opening of Mount Meru hotel in Arusha last night. Photos by Freddy Maro of Ikulu.​

Baada ya balozi Masters kuanza biashara Tanzania kufuatia mkutano wa Sullivan ("summit of a lifetime") tunategemea kuona wabongo nao wanapewa nafasi kama huyo bwana kama ambavyo logo ya summit ilivyoonyesha daraja toka marekani kuja afrika.

Wao wameanza sasa zamu ya waafrika.
 
kwa bahati mbaya sana nikiwa kama mdau... sidhani kama ni matunda ya sullivan, its a strategic move mkuu and it was bound to happen
 
Tunajitajidi kwa uzuzu kweli that was a summit of a lifetime, jamaa kajiokotea bonge la hoteli
 
alipewa Mtanzania akawa hana hela ya kufanya renovation! sasa sijui alaumiwe nani?
 
alipewa Mtanzania akawa hana hela ya kufanya renovation! sasa sijui alaumiwe nani?
Mkuu geza

nadhani labda nimechanganya au tumechanganya... hilo la mbongo hakuna ujanja aliharibu tu hoteli kwasababu ya kuwa na uhusiano na bwana sumaye kwahiyo akaepwa dili... huyu wa sasa nimependa efforts alizoweka mno na ni good move

but one question je... pasingekua na sullivan, tusingepata the right investor? jibu ni no... tungepata tu,
 
Hamna kitu mtakachopata zaid ya ajira. Hiyo hotel niya mTz na haina husiano na Sullivan bla bla.
Andrew Young (Chairman wa Leon Sullivan) is a share holder in Barrick. Alileta mafisadi wenzake waje wafaidi tax holiday & 3% corporate tax wakiwekeza ktk migodi.
 
mkwere anazuga tuuu hapa ameenda arusha kulazimisha meya achaguliwe wa ccm, huu ni uzandiki kabisa udikiteta mpaka kwenye umeya?
 
Nimeona Itv news leo hao wenye hoteli wamepewa mkopo dola mil.24 na taasisi mbali mbali kwa ajili ya ukarabati ( crdb iliwapa dola mil.11 ).Ukarabati mzima umegarimu dola mil.25
 
Carlton Masters na Andrew Young wako pamoja ktk SADEF, Sullivan summit na uchafu mwingine...
 
acheni wivu nyie . hiyo hotel imezalisha ajira hapa arusha na pia imefungua uchumi kwa watu wa arusha . ni jambo la kufurahia .
 
Mkuu Bucho, asilimia kubwa ya waajiriwa wataishia kuwa wakenya .. utakuja kuniambia...
 
Mkuu Bucho, asilimia kubwa ya waajiriwa wataishia kuwa wakenya .. utakuja kuniambia...

mh susuviri watu walioajiriwa wengi sana ni wa bongo . itasaidia sana kiuchumi . vijana wengi wamelamba kazi pale na watu wengi wana order ya kupeleka aina mbalimbali ya vyakula pale . ina umuuhimu sana sana kufunguliwa tena hile hotel .
 
Acha masihara, watanunua nyanya za kuweka chini na kutandikwa kwenye magunia, wanunua kuku wanaolishwa ARV, watanunua kabichi iliyopandwa pembenimwa uchochoro ambao kila mlevi ana.....

Kazi wanazolamba wabongo ni uporter, laundry, housekeeping na jikoni basi kazi za maana wanchukua wengine.

Wageni watakaofikia hapo ni wa nje watakuja na hela za plastic ( crediti cards), faida kubwa itaenda nje ya nchi by way of dividends to shareholder.

Hamna kitu hapo
 
Wee bana ustutanie hapa, Sullivan haitoleta matunda wala mbegu kwa tz, hao wawekezaji wataendesha mitambo yao kwa mishumaa? Kwanza mshumaa haukuzimika wakti wa huo uzinduzi?
 
Napata ugumu wa majibu ya maswali kadhaa: kama carlton masters ni mwekezaji serious wa kutoka marekani inakuwaje aombe mkopo kwenye benki ya nchi maskini duniani badala ya kuja na ela toka kwao? Isije ikawa mambo ya richmond yanajirudia maana tuliambiwa kampuni ya marekani richmond ilikuja kuwekeza ktk umeme bado ikapewa mkopo na crdb kwa dhamana ya serikali ya tanzania. Isije ikawa carlton masters anatumiwa kama kivuli cha kumwakilishi mwenye hoteli wa kweli ambae ni mwanasiasa kigogo wa tanzania maana hapa ni shamba la bibi kijijini kila mtoto anafanya analotaka. Jambo lingine la kuzingatia ijulikane hata marekani kuna mafisadi pia kama bernard madolf, viongozi wa benki ya lehman brothers nk.
 
alipewa Mtanzania akawa hana hela ya kufanya renovation! sasa sijui alaumiwe nani?

Nani kakudanganya, unafikiri hata huyo mmarekani katoa hela yake? Kuna mkopo toka CRDB wa US22 million na pia hiyo development fund imetoa pesa ingine ndo maana wana shares 40%
 
Napata ugumu wa majibu ya maswali kadhaa: kama carlton masters ni mwekezaji serious wa kutoka marekani inakuwaje aombe mkopo kwenye benki ya nchi maskini duniani badala ya kuja na ela toka kwao? Isije ikawa mambo ya richmond yanajirudia maana tuliambiwa kampuni ya marekani richmond ilikuja kuwekeza ktk umeme bado ikapewa mkopo na crdb kwa dhamana ya serikali ya tanzania. Isije ikawa carlton masters anatumiwa kama kivuli cha kumwakilishi mwenye hoteli wa kweli ambae ni mwanasiasa kigogo wa tanzania maana hapa ni shamba la bibi kijijini kila mtoto anafanya analotaka. Jambo lingine la kuzingatia ijulikane hata marekani kuna mafisadi pia kama bernard madolf, viongozi wa benki ya lehman brothers nk.

CRDB aliyechukua mkopo ni mwekezaji wa kibongo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom