Matunda ya Lema yaanza kuonekana World Bank wahoji matumizi makubwa Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matunda ya Lema yaanza kuonekana World Bank wahoji matumizi makubwa Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Dec 26, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  SAKATAla ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, limeingia katika hatua nyingine baada ya Benki ya Dunia nchini, kutaka maelezo ya kina vinginevyo itasitisha kuendelea kutoa misaada katika Jiji hilo baada ya kubaini fedha zaidi ya Sh milioni 100 kutumika kukarabati ofisi nne za Jiji hilo.

  Vyanzo vya habari kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha vilisema kuwa fedha hizo ambazo katika mradi wa benki hiyo ujulikanao kwa jina la Tanzania Strategic Cities Programmes (TSCP) wa Jiji hilo, zimetumika kukarabati ofisi za Mkurugenzi, Biashara, Mchumi na Mhandisi.

  Habari za uhakika zilieleza kuwa kutumika "hovyo hovyo" kwa mamilioni hayo ya fedha, hakukuridhisha uongozi wa Benki ya Dunia kwani ulieleza kuwa ni matumizi mabaya ya fedha hivyo walitaka maelezo ya kina kwa maandishi.

  Uongozi huo wa benki ulimwandikia pia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo juu yahali hiyo na uamuzi ambao ofisi hiyo inataka kuchukua, ndipo mkuu huyo alipoingilia kati nakuiahidi Benki ya Dunia kuwa itafuatilia na kama kuna ulaji, hatua kali zitachukuliwa.

  Habari zilieleza kuwa baada ya ahadi hiyo, ndipo benki hiyo iliamua kuacha kwanza hatua yakehiyo mpaka watakapopata taarifa rasmi ya hatua za kuchukuliwa wahusika wa ubadhilifu wa fedha hizo.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha, Estomih Chang'a alipoulizwa juu ya kiasi hicho kutumika kukarabati ofisi nne tu, alisema taratibu zote za kutangaza zabuni zilitumika hivyo kampuni iliyofanya kazi hiyo ilipewa kazi hiyo kwa uamuzi wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi ya Jiji hilo.

  Chang'a alisema kazi ya kukarabati ofisi ilitangazwa zabuni, ikafanyiwa tathmini, ikapita zabunina kuzingatiwa Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa asilimia 100 na kama kuna lingine liko tofauti, aulizwe Mhandisi wa Jiji.

  Alipobanwa ili atoe ufafanuzi iweje yeye kama kiongozi wa Jiji la Arusha na Mdhibiti Mkuu wa matumizi ya fedha, akubali kiasi hicho kikubwa cha fedha kutumika kukarabati ofisi mbili, alisisitiza aulizwe Mhandisi huyo kwa madai ndiye aliyefanya tathmini ya awali kabla ya utangazaji zabuni.

  Mhandisi wa Jiji, Afwilile Lamsy alipoulizwa kwa njia ya simu, alisema na kupingana na Mkurugenzi wake kwa kueleza kuwa ofisi zilizofanyiwa ukarabati ni zaidi ya 10, hatua iliyoonekana kupingana na baadhi ya nyaraka zinazoonesha kuwa ukarabati huo ulifanywa kwaofisi nne tu.

  Lamsy alisema akiwa ni mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli zote za ujenzi, anachojuani kuwa ofisi zilizofanyiwa ukarabati ni zaidi ya 10, lakini alishindwa kufafanua kama bajeti yake iliruhusu kampuni kutenda kwa zaidi ya Sh milioni 100 kukarabati ofisi hizo.

  Mkuu wa Mkoa, Mulongo alipoulizwa kama anajua chochote juu ya utata wa matumizi ya fedhaza mradi huo, alikiri kuufahamu na kueleza kuwa kutumika kwa fedha hizo ni moja ya kazi za mradi huo.

  Ila alienda mbali zaidi na kueleza kwamba tatizo ni kiasi hicho cha fedha na ndio maana Tume imeundwa kuchunguza.

  "Kukarabati ofisi ni moja ya package (sehemu) ya mradi huo, lakini kuna tatizo katika utoaji wazabuni kwa kampuni kwa fedha hizo nyingi na ndio maana Tume ya Bodi ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) inachunguza kubaini ukweli," alisema Mkuu wa Mkoa.

  ::HabariLeo::
   
 2. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na bado,mpaka kieleweke
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  safi sana
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tuna uhakika ni influence ya lema pekee?
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Una-aleji na Lema wewe.....?
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sina allergy na LEma and he know it, tatizo ninachopenda ni kuwa realistic na facts tunazoweka ili kuondoa any kind of hey-way thinking kwani Arusha ni zaidi ya jimbo kwa nchi yetu, it is a strategic political centre by any standard na mara nyingi ni vyema kuwa na all cards right ili mambo yakae vizuri

  efforts zote za matumizi, mapitio ya matumizi na hata any interventions hupitia mfumo fulani na ndio maana nikahoji kama ni mtu mmoja as we try to portray,,,,

  vipi wewe unayo allergy na mtu anayetaka kujua zaidi hata pale usipotaka ahoji??
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Uwepo wa Lema unaweza kuwa factor mojawapo ya madudu kuanza kuanikwa wazi, Arusha kuna mauchafu mengi sana ndio maana wanafanya juu chini waendelee kuhodhi baraza la madiwani ili kuficha aibu kama hii isitokee. Big up Lema na Madiwani hasa wa CDM.
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nawapongeza WB kwa kufuatilia lakini ninawasiwasi na maelezo ya mkuu wa mkoa. Hivi hizi tume ndio zimekuwa organs za kuchunguza utendaji wa serikali. Hakuna watu wenye wajibu huo hadi kuendelea kupukutisha hela zetu "za dhamani" kwa kuunda vitume kwenye kila jambo! Something must be done!
   
 9. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mhs Lema komaa nao hao, kuna miradi mingi tuu hewa ndio maana wanangangania Umeya kuficha maovu yao!!!!!!! Kuna maovu ya sasa pia maovu ya nyuma, yote hayo inahitaji yafichuliwe tuu!!!!!!!! Zama na TANAPA kwenye fedha nyingi na matumizi ya ajabu ajabu, tujue hiyo budget ya TANAPA pamoja na mbuga zetu, mapato, matumizi na zinamnufaisha vipi Mtanzania na mwana Arusha kwenye mbuga hizo???????????

   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Unafikiri ni kwa nini wanangangania Umeya wa mji wa Arusha, si kwamba wanazo siri nyingi hawataki zifichuke?????????
  Lema ni catalyst wenye uchungu na nchi hii wanapata pa kusemea!!!!!!!!!!

   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kuna mchezo unataka kufanywa, mkurugenzi anasema wametumia mil. 100 kukarabati ofisi 4 wakati mhandisi anaema 10, nafikiri walikuwa anataka kuomba pesa zingine kwa ofisi 6 wanazoficha.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hizo tume ni ishara tu kwamba serikali ina very weak internal control na inahitaji msaada wa tume, unfortunately tume nyingi huandaliwa na walewale wanaotakiwa kuchunguzwa
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks alot mtumishi, uweiweka vyema.... tatizo hapa ni namna tunavyoripoti kishabiki kiasi cha kufanya as if one person is working alone

  At least umenielewesha kwamba Lema ni catalyst wa hayo mapambano which means he is not alone, na nasema hivi kwasbabu kazi ya makamanda wengine walio arusha ni kubwa sana na katu tusiizamishe chini ya blanket/carpet moja.... pia kuna watendaji ndani arusha ingawa ni wa serikali lakini nao wamchoshwa na unyang'au na sasa wanasaidia kuibua madudu

  one...
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Duh! Hao TANAPA wameanza kula ela zamani mkuu, yakifichuliwa yote mtashangazwa na itakuwa vigumu kuamini, yani i mean kiwango cha pesa...
   
 15. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapa Lemma ameingiaje mbona story nzima hamna panapo mtaja Lemma au Lemma alienda WB kuwaambia fedha hazifanyi kazi ili wazuie msaada huo mbeleni
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa hapa Lema anaingiaje? ..... Mbona mnakuwa na ushabiki wa kipuuzi?

  Ila tungejua mkandarasi ni nani, maana yule meya naye ni mkandarasi.

  Pia nao WB waache upumbavu, 100m kwa ofisi nne ni sawa na 25m kwa ofisi moja hivi 25m inatosha hata stationeries ukizingatia hela zetu za madafu?
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Usiwaite wapumbavu WB wanafuatilia pesa zao, Lema anaingia hapa kama diwani na mbunge wa jimbo la Arusha mjini.
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hujui Lema ni mmoja wa madiwani na mbunge wa jimbo la Arusha mjini.
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tulikionya CCM juu ya matumizi mabaya ya kodi zetu pamoja na hela za wahisani na wala hawakutaka kusikiliza kitu. Mwakani ni kilio kitupu!!
   
 20. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  Mungu awatie nguvu,enyi wabunge wa CDM!
  Viva kamanda LEMA.
   
Loading...